Tahadhari: Lifts(Elevators) zinaweza kuua!

Pole sana Mkuu..This is Simba.. Oooh sorry this is Africa..
 
Pole sana mkuu
Saa kama tatu hivi zilizopita nilikua Kariakoo kwenye jengo moja la ghorofa saba ambalo hutumika kama makazi ya watu na ofisi pia. Ofisi niliyokua naenda ipo ghorofa hiyo ya saba ambapo ilinilazimu nipande lift

Nilipobonyeza kitufe cha namba ya floor ninayoenda akawa amekuja dada ambaye kwa mavazi yake nikahisi alikua ametoka au anakwenda kwenye mazoezi (nadhani kwenye jengo lile ipo gym) hivyo ikanilazimu nibonyeze kitufe cha kumsubiria akapanda tukaondoka

Sekunde chache tu baada ya kuondoka tukiwa tunapita floor ya tatu taa zikazimika ndani ya ile lift, ikatoa mlio kama imegonga kitu halafu ikawa kama inarudi chini kisha ikasimama kabisaa! Yule dada akapiga yowe la ku panik. Nilipomwambia asiwe na wasiwasi tutatoka akanisogelea na kunikumbatia huku anaendelea kupiga kelele

Changamoto kubwa ni ile milango ya lift yenyewe ilivyokua mizito mpaka unahisi kabisa hata hizo kelele hazifiki popote. Nilinyoosha mkono na kubonyeza kitufe cha emergency bila kuondoa mkono(continuously) lakini hatukuweza kupata msaada kwa haraka

Hali ilikua ya taharuki kubwa maana kile kichumba cha lift ni kdogo, milango ni minene sana na joto lilikua linaongezeka. Tulikaa mle kama dakika saba au nane ambazo zilikua kama mwaka ndipo zikasikika sauti za watu kwa nje wakiwa wanashughulika kutufungulia mlango na muda walipofanikiwa kutufungulia yule dada niliyekua nae alikua amelala chini kwenye sakafu ya lift na akawa kama anaeelekea kupoteza fahamu!!!

Namshukuru Mungu tulitoka salama ingawa yule dada ilibidi apelekwe hospitali kwa hali aliyokua nayo maana hata mambo yake mengine ya kiuanamke (tafsida imezingatiwa) yalimuharibikia na ukizingatia mavazi aliyokua amevaa hakutarajia pengine mambo yamtokee wakati huo!

Wito wangu kwa watengeneza elevators, watengeneze lifts za milango transparent ili mtu aweze kuona nje angalau pressure inapungua kuliko hizi lift zenye milango utadhani gereza au kaburi aisee! Mtu unapokua unawaona watu nje unajua muda wowote unatoka. Amakweli kifo kwa binadamu ni sekunde tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilinitokea jengo la Treasurer Dodoma. Tulikaa kama Dakika tatu, umeme ukarudi. Ndani ya lift tulikuwa wawili tu, Mimi na Mdada mmoja ndugu yangu, sikujua cha kufanya ikabidi niwe namtuliza tu kuwa asiwe na waswas watafungua soon maana shida wanaijua.

From that day, lift huwa nazikwepa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi pia ni mhanga, jengo la Mega complex Arusha, floor ya tano Kenyatta University.
Tulikuwa watatu vidume wote, jamaa yangu akaanza kulipiga ngumi, mlango mgumu balaa, Dakika kama Tano, Jenereta likawashwa hapo tushaanza onja joto ya jiwe kijasho.
Ni ombea mtu tu akusimulie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saa kama tatu hivi zilizopita nilikua Kariakoo kwenye jengo moja la ghorofa saba ambalo hutumika kama makazi ya watu na ofisi pia. Ofisi niliyokua naenda ipo ghorofa hiyo ya saba ambapo ilinilazimu nipande lift

Nilipobonyeza kitufe cha namba ya floor ninayoenda akawa amekuja dada ambaye kwa mavazi yake nikahisi alikua ametoka au anakwenda kwenye mazoezi (nadhani kwenye jengo lile ipo gym) hivyo ikanilazimu nibonyeze kitufe cha kumsubiria akapanda tukaondoka

Sekunde chache tu baada ya kuondoka tukiwa tunapita floor ya tatu taa zikazimika ndani ya ile lift, ikatoa mlio kama imegonga kitu halafu ikawa kama inarudi chini kisha ikasimama kabisaa! Yule dada akapiga yowe la ku panik. Nilipomwambia asiwe na wasiwasi tutatoka akanisogelea na kunikumbatia huku anaendelea kupiga kelele

Changamoto kubwa ni ile milango ya lift yenyewe ilivyokua mizito mpaka unahisi kabisa hata hizo kelele hazifiki popote. Nilinyoosha mkono na kubonyeza kitufe cha emergency bila kuondoa mkono(continuously) lakini hatukuweza kupata msaada kwa haraka

Hali ilikua ya taharuki kubwa maana kile kichumba cha lift ni kdogo, milango ni minene sana na joto lilikua linaongezeka. Tulikaa mle kama dakika saba au nane ambazo zilikua kama mwaka ndipo zikasikika sauti za watu kwa nje wakiwa wanashughulika kutufungulia mlango na muda walipofanikiwa kutufungulia yule dada niliyekua nae alikua amelala chini kwenye sakafu ya lift na akawa kama anaeelekea kupoteza fahamu!!!

Namshukuru Mungu tulitoka salama ingawa yule dada ilibidi apelekwe hospitali kwa hali aliyokua nayo maana hata mambo yake mengine ya kiuanamke (tafsida imezingatiwa) yalimuharibikia na ukizingatia mavazi aliyokua amevaa hakutarajia pengine mambo yamtokee wakati huo!

Wito wangu kwa watengeneza elevators, watengeneze lifts za milango transparent ili mtu aweze kuona nje angalau pressure inapungua kuliko hizi lift zenye milango utadhani gereza au kaburi aisee! Mtu unapokua unawaona watu nje unajua muda wowote unatoka. Amakweli kifo kwa binadamu ni sekunde tu!
Naunga mkono hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia ni mhanga, jengo la Mega complex Arusha, floor ya tano Kenyatta University.
Tulikuwa watatu vidume wote, jamaa yangu akaanza kulipiga ngumi, mlango mgumu balaa, Dakika kama Tano, Jenereta likawashwa hapo tushaanza onja joto ya jiwe kijasho.
Ni ombea mtu tu akusimulie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiingia kwenye lift za huko lazima uombe sala ya mwisho
Lakini kwa mimi bora nifanye mazoezi hata kama ni 20

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lift za vioo labda majengo mapya na kwenye malls.
Kuna siku nimeenda ubungo plaza kuingia kwenye lift nikawa nasali isizime maana hapo tu lift haina hata ac unawaza ikizima si ndo mnakufa humo humo
Halafu sehemu nyingine lift zinajaa balaa! Kama lile jengo la RITA pale karibu na Bilicanas. Unaomba Mungu lisitokee jambo baya maana inabidi hiyo rescue action isichelewe hata kwa dakika moja amasivyo itakua balaa kwa watu wanavyojazana
 
Ndio hapo unajua roho ya binadamu kutoka ni kitu cha sekunde tu mkuu
Sisi mwanzo tulipanic sana ila tukasema tupige zile namba za dharura, zote hata haziiti hata, tukaanza kutaniana tunakufa wote taratibu kwa kukosa hewa, tunacheka lakini ukipima mapigo ya moyo kila mmoja ana wasiwasi balaa.
Yaani dakika tano au saba utadhani mwaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu sehemu nyingine lift zinajaa balaa! Kama lile jengo la RITA pale karibu na Bilicanas. Unaomba Mungu lisitokee jambo baya maana inabidi hiyo rescue action isichelewe hata kwa dakika moja amasivyo itakua balaa kwa watu wanavyojazana
Yani hapo wenyewe tulikua kibao. Hewa hamna na lift haina ac. Nilivyokua nashuka nikapanda za upande mwingine ndio ziko automated kidogo
 
penda sana kuwaza nje ya "box"

Mimi nina wasiwasi kama Anaomba ushauri Angemuomba PAPUCHI "she"

Nawaza kwa sauti tu
kajamaa kadogo wakati maisha yako yapo hatarini hakuna kingine kitakachoingia akilini mwako na kwenye hisia zako zaidi ya kuomba uokolewe/uokoke na janga hilo tu. Tena utaweka ahadi za kila aina kwa Mungu wako kua ukitoka salama utaacha dhambi zote 😀😀😀
 
Lift za vioo labda majengo mapya na kwenye malls.
Kuna siku nimeenda ubungo plaza kuingia kwenye lift nikawa nasali isizime maana hapo tu lift haina hata ac unawaza ikizima si ndo mnakufa humo humo
Huo wasiwasi ulonao siku Mimi imenipata kama ungekuwepo nadhani ungetabasamu tu kwa kuwa tulianza kutaniana japo hewa hamna.
Kwakweli yake ni makaburi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom