Tahadhari: Lifts(Elevators) zinaweza kuua!

Tahadhari: Lifts(Elevators) zinaweza kuua!

Kuna siku tulikua semina dodoma ilifanyikia chuo cha mipango, ile asubuhi tumejazana kwenye lift kwenda juu kufika floor ya 8 ikagoma ikaazaa kurudi chini kwa kasi ikafika mahari ikasimama tuliganda pale kama dk 5 na milango haifunguki, vilio vya kina dada vilitawala mle ndani ikabidi tuwe tunawatuliza maana joto lilikua kali na hewa inapungua hadi mafundi walipokuja, kuanzia siku hiyo kuna watu waliamua wawe wanapandisha ngazi hadi floor ya 12

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaaa hii hali Mimi ilinikuta lakini sijawai fikiria kuacha tumia elevator

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku tulikua semina dodoma ilifanyikia chuo cha mipango, ile asubuhi tumejazana kwenye lift kwenda juu kufika floor ya 8 ikagoma ikaazaa kurudi chini kwa kasi ikafika mahari ikasimama tuliganda pale kama dk 5 na milango haifunguki, vilio vya kina dada vilitawala mle ndani ikabidi tuwe tunawatuliza maana joto lilikua kali na hewa inapungua hadi mafundi walipokuja, kuanzia siku hiyo kuna watu waliamua wawe wanapandisha ngazi hadi floor ya 12

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwaka fulani nikiwa nasoma Law School pale Mawasiliano nikiwa na rafiki yangu na mtu mwingine, jumla watatu..tukapanda lift ya jengo mojawapo..

Sisi tulikuwa tunaenda ghorofa ya 3 ambako ndiyo mwisho wa lift...sasa ikafika floor ya pili ikasimama, akashuka jamaa mmoja tukabaki mimi na rafiki yangu.

Hapo ndipo kizazaa kikaanza. Ikaenda mpaka floor ya 3, ila ikagoma kufungua mlango. Ikaanza mchezo wa kupanda na kushuka ground floor.
Ikafika wakati, zile taa za kuonesha umefika floor ipi zikazima...inapanda juu, ikifika haifunguki, inashuka chini, inapanda tena.
Tukajaribu kupiga simu, hazitoki, jaribu ku shout sauti haitoki.

Nikawa naona kabisa kuwa tunafia mle ndani. Tulikaa almost 6 to 7 minutes. Kijasho chembamba cha panick kimeshaanza kutoka.

Baadaye ikapanda tena hadi floor ya tatu, milango ikaanza kufunguka very slowly, upenyo ulipopatikana tu, tukatoka.

From that day, ile experience imebaki kichwani mpaka leo. Na sikupanda tena zile lift za pale chuoni. Na kila nikienda mahala pengine kabla ya kutumia lift, ile kumbukumbu hunijia.
 
Cajojo hiyo experience uisikie tu kwa mwingine ni hatari sana
Hyo experience ninayo mkuu ilinikuta nikiwa na husband na mtt wetu mdogo wa miezi 7. Lilikua tukio la dkk chache but lilinipa hofu ambayo sitakaa nisahau nawaza mtt wangu atakavyoanza kukosa hewa jamani Mungu mkubwa tulipojaribu kubonya kitufe ilifunguka. Ndo maaana nasema nimesisimkwa maana nikikumbuka najisikia vibaya
 
Halafu sehemu nyingine lift zinajaa balaa! Kama lile jengo la RITA pale karibu na Bilicanas. Unaomba Mungu lisitokee jambo baya maana inabidi hiyo rescue action isichelewe hata kwa dakika moja amasivyo itakua balaa kwa watu wanavyojazana
Kuna jaa plus joto ushuzi basi tafrani. Hapo round hawachukui wenye mioyo midogo kama mie tunaanza safr ya kwenda kwa baba kwa kuzimia kwanza
 
Umenikumbusha 2012 nikiwa intercontinental hotel Adis Ababa lift ilinizimikia ghorofa ya 8.Bahati nzuri lift zao ni za wazi na za vioo hata hivyo walio chini wanakuona.Nikaona kitufe cha emergency nikabonyeza king'ora kikalia sana kuwaona watu chini wanapiga kelele nisaidiwe.Baada ya chini ya dakika mbili nikaona ninashushwa ghorofa ya saba mlango unafunguliwa na mafundi.Kutoka wakaniomba radhi nikapewa dola 20 kama samahani.
Nilichoshangaa umeme ulikatika king'ora kililizwa na nini kuulizia wakaniambia umeme ukikatika emergency button ina umeme wake mbadala ndio unasababisha king'ora kilie.
BONGO TUJITAFAKARI

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo ndio standards tunataka ziwekwe na serikali kwa wenye majengo yote wanaopaswa kuweka lift
 
BBC HQ
bbcworldwide04.jpg
BBC-Worldwide-HQ-1-1.jpg
Mwendo wa escalators kwa kwenda mbele, nice building, superb architectural work
 
Back
Top Bottom