Lowasa asituletee ya Sudan na Nigeria
Wana JF
Sikushangaa kabisa askofu Gwajima hakutumia hata dakika moja kumuonya swahiba wake lowasa kuhusu kauli yake ya kanisani tabora iliyokuwa na dhamira ya kuwagawa watanzania kwa misingi ya kidini. Badala yake gwajima katumia muda mwingi kusambaza chuki kwa dr slaa. Gwajima kama kawaida yake alifanya maigizo yaliyojaa uongo na chuki kwa lengo la kutuaminisha watanzania kwamba mke wa dr slaa ndo sababu ya dr slaa kuhama chadema. Kutuaminisha kuwa tatizo halikuwa lowasa kuingia chadema akiwa na mzigo wa tuhuma za ufisadi. Mungu anaipenda tanzania na kawaida mungu hamfichi mnafiki. Kule Tabora kanisani mungu kamuumbua lowasa na kutuonyesha watanzania sura halisi ya mtu anayedai anataka kuwaongoza watanzania. Kumbe lowasa anataka kuwa rais wa waluteli. Mungu mkubwa umetuonyesha waja wako. Siye waislamu kumbe tusingekuwa na chetu kwenye utawala wa lowasa, ingekuwa zamu ya waluteli!
Mungu umetuonyesha, na sasa tunajua cha kufanya oktoba 25. Watanzania tusipokuwa makini lowasa huyu atatuletea ya kule sudan na naijeria. Tunajua kuwa udini ulioletwa na wanasiasa ndio umekuwa chanzo cha mgogoro mkubwa baina ya watu wa sudan na kupelekea dhahma kubwa. Wasudan kule kusini wanaangamia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo chanzo kikuu ni udini. Ni kutokana na wasudan kugawanywa kwa misingi ya kudini na kikanda, kusini wakristo na kaskazini waislamu. Kule naijeria hivyo hivyo wamegewanika kikanda na kidini. Kaskazini waislamu na kusini wakristo. Boko haram ikazaliwa hapo hapo. Hapa kwetu tumeona chadema ikionyesha kuigawa tanzania kikanda na lowasa juzi tu kaonyesha na kidini pia. Eti nchi sasa itawaliwe kwa zamu zenye kufuata misingi ya kidini na kimadhehebu. Watanzania tukiikubali dhambi hii uchaguzi ujao atatokea mgombea ataesema ni zamu ya wasunni kwa vile waislamu nasi tumegawanyika kimadhehebu. Ewe mola twepushe waja wako na balaa la kuwa na rais wa aina ya lowasa.