Bahati nzuri Dr Slaa ni mtumishi wa Mungu kwa cheo cha upadri na ni mtu anayejua nini maana ya siri na nini maana ya kutunza siri.
Gwajima naye ni mtumishi wa Mungu mwenye cheo cha uasikofu kama ilivyo kwa Dr slaa naye ana jua siri ni nini na namna ya kutunza siri.
Kwa pamoja wote ni watumishi wa Mungu wanaopaswa kutunziana siri pamoja na siri za watu wengine.
Kama kuna mtumishi mmoja kaamuwa kumwaga ugali hadharani,mwenzake kajibu kwa kumwaga mboga hadharani,huyu mtumishi wa pili aliyejibu kwa kumwaga mboga hadharani ana laumiwa kwa kosa gani?.
Na mimi hawanipati yaani upinzani huu wa kuwagawa waTz kwa gharams yoyote nimeanza kuwaogopa sanaPoint ya msingi:
WANAWATUMIA VIJANA KUWALISHA CHUKI DHIDI YA UTAWALA ULIOPO MADARAKANI.
Hii ni HATARI sana, na kuna vijana wenasa kwenye huu mtego, ila sio mimi.
Kweli hujafa hujaumbika...hizi ni salamu kwa jingalao!Ni muda mrefu jamii yetu imekuwa ikiwaheshimu na kuwaamini viongozi wa dini katika masuala mbalimbali ya kiroho na ustawi wa familia.
Ni jambo la kawaida sana kwa waumini wa dini zote kupeleka matatizo yao mbalimbali ya kifamilia kwa viongozi wa dini.
Ni dhahiri kwamba wengi wetu hupeleka masuala mbalimbali hata yale ya unyumba na siri nzito nzito za chumbani na familia kwa ujumla kwa kuwa tuna imani viongozi wa dini wana hulka ya kutunza siri na kusaidia kutatua matatizo yetu ya kiroho au kifamilia.
Hii ni tofauti kwa Gwajima ambaye ni mtomvu wa heshima ya kiongozi wa dini kwa kueleza siri za familia aliyoipa huduma za kiroho kisa tu kachokozwa kisiasa na yeye kajibu kwa kutoa siri za familia ya Slaa.
Angekuwa daktari angeweza kufutiwa cheti na kudaiwa fidia.
Lakini tukumbuke ni Gwajima huyu huyu aliyeshutumiwa kuvuruga ndoa ya Mbasha badala ya kutatua mgogoro wa familia hiyo.
Hii ni trend ya Gwajima anayejiita Bishop ambayo inatakiwa kuangaliwa kwa jicho la Tahadhari hasa hasa na waumini wake wanaompelekea siri za ndani.KWA HISANI YA MTU WA TANZANI!!