Nyie ndo mafala. Watu haalali wakiimalisha biashara zao wewe uko mtandaoni kumdiscourage. Huna tofauti na aloandaa mkanda wa rwakatale
Habari Watanzania na Wasio Watanzania,
Jana nilinunua juice ya Azam ya "tropical mix" ya TZS. 2500,
Nilipofika home nikamimina kwenye glass ili ninywe, nikapiga funda la kwanza nikastuka kidogo, nikapiga la pili nikakutana na radha ambayo ni ya ajabu ajabu sana yani kama uozo ulochanganyika na mafuta ya taa, nikataka nimrudishie mwenye duka ila nikaona niachane naye, nikaenda kuitupa niki-assume labda mwenye duka aliiangushia mafuta ya taa.
Leo tena nikaamua kununua juice ya AZAM sehemu ya mbali kabisa na niliponunulia jana, this time nikanunua juice aina ya "APPLE", basi mida ya usiku hivi baada ya msoc nikaamua nichukue glass moja niipige, nimefika nusu kabla haijaisha nikaiwa nimeiweka ile glass kwenye meza ambapo inapigwa na mwanga direct ndani, OMG... nimeona mauchafu uchafu kibao aisee kwenye glass, nikaanza kujiuliza au glass ni chafu??? Ikabidi nichukue glass kubwa halafu nimimine ile ile iliyopo kwenye box niione nayo, daaaaaaahhhh, aisee ni mauchafu kibao yan.
Hapa nilipo hadi nahisi nishaanza kuumwa, nimeamua kuiweka hapa ili iwe ushahidi nikiumwa walau nikashtaki. (Mungu Aniponye kwa kweli).
Nawashauri wapenzi wa hizi juice kabla hujaibugia uwe unapenda kuangalia ikoje kwanza maana waweza dhurika kwa kweli.
N.B
Sijaweka bandiko hili ili kuvuruga biashara ya AZAM, nop, ninawatahadharisha wenzangu na nilichokiandika ni ukweli mtupu.
shukrani kwa taarifa,ingawa mashtaka yako itakuwa ngumu kwako kushinda kesi kutokana na mazingira yalivyo maana juice umeifungulia kwako,huo uchafu umeuona peke yako,watakuruka mita mia kama ujuavyo wafanyabiashara wanasema kitu kikifika nyumbani hawana imani nacho sababu waweza kuta ww ndo umefanya huo uchafuzi halafu unawatupia shutuma.
Unamaanisha brender?mkuu.nunua breder nunua matunda utengeneze juic yako nyumbani kwa kutumia matunda ya asili yamejaa kila kona.mtaendelea kunywa sumu hadi lini?
Safi sana. Tatizo wabongo tuna muda wa kutosha kukaa saluni, kuangalia mechi za soccer la ulaya baa lakini muda kidogo kwa ajili ya kuandaa diets kama hizo tatizo.Nishaacha kunywa juice hizo kitambo sana.Tunanunua embe tunasaga tunakunywa,nzuri sana ya kusaga mwenyewe na haina gharama. Tsh 2500 soko la Stereo unapata embe 15 zinatoa juice lita 5 mpaka 6 nachanganya na passion kidogo za sh 500
KABISA! HAKUNA KITU SIPENDI KAMA AZAM COLA, kwenye mabasi wanamtindo wa kuzigawa. Wakifika kwangu nawambia asante!Azam Cola ni bomu lingine!
tblj,Tatizo la Bakharesa amajaza wapakistani na Wahindi,trust me hawa ni mabingwa wa kuchakachua na wanasema tangu kawaleta hao faida imeongezeka maradufu kwani jamaa wamepunguza gharama za uzalishaji kwa kutumia industrial raw materialsa badala ya matunda halisi.Kama mmegundua ata test na texture ya Ice cream zake siku haiko sawa.
Unamaanisha brender?
dah! kwakweli leo mumenijuza zaidi juu ya juice ya azam man hata mimi nimpenzi hii bizaa ya juice .kuna ciku nilinunua juice yenye mchanganyiko wa mapera na machungwa nilishindwa kutambua kama ile ni juice au makange ya kuku.hata tumbo lilisumbua kwa mda wa weerk moja toka hapo cinywitena juice ya mapera .Inaingiaje shekhe wangu hapo ukafir tena? Au maji na juice za azam ni za msikiti?
Hoja hapa ni ubora na usalama wa bidhaa tuache udini mkuu.
dah! kwakweli leo mumenijuza zaidi juu ya juice ya azam man hata mimi nimpenzi hii bizaa ya juice .kuna ciku nilinunua juice yenye mchanganyiko wa mapera na machungwa nilishindwa kutambua kama ile ni juice au makange ya kuku.hata tumbo lilisumbua kwa mda wa weerk moja toka hapo cinywitena juice ya mapera .