TAHADHARI: Kwa watumiaji wa juice za AZAM

watu wengine ubongo wao umeoza kwa udini, yaani mtu analalamika katoa pesa yake kanywa uchafu, mwingine anakuja kuleta sababu za udini,mijitu mingine bwana sijui ina kuwaga vipi?hii ndiyo kila watoto wao wakifeli shule inasema wameonewa ata kama watoto hamna kitu kichwani
 
Nishaacha kunywa juice hizo kitambo sana.Tunanunua embe tunasaga tunakunywa,nzuri sana ya kusaga mwenyewe na haina gharama. Tsh 2500 soko la Stereo unapata embe 15 zinatoa juice lita 5 mpaka 6 nachanganya na passion kidogo za sh 500
 
Aisee umenipa somo sinunui tena. Wauzaji wengi vile vile hawatunzi bidhaa zao vizuri na wakati mwingine wanauza bidhaa zilizomaliza tarehe ya kutumika yaani zimeexpire.
 
Nyie ndo mafala. Watu haalali wakiimalisha biashara zao wewe uko mtandaoni kumdiscourage. Huna tofauti na aloandaa mkanda wa rwakatale

Kwa hiyo huyo "----" alitakiwa afanye nini baada ya kuona tatizo linalohatarisha afya za watu wengi? Badala yakuja kutukana watu hapa, hata kama wewe ni kibaraka wa Saidi ilibidi uutafute ukweli kimyakimya kisha umjuze kama kuna tatizo arekebishe, TUNAJENGA HATUBOMOI MKUU! Mimi namuunga mkono SSB kwa sababu ametoa ajira nyingi kwa watanzania, lakini tuhuma zinazomwandama kwa sasa inanifanya nianzekuogopa kuwanywesha wanangu juice za AZAM.
 
kalikenye huenda una matatizo ya akili, yaani mimi niko tunduru nimenunua juice dukani nikasoma expire date iko mbali, nikikuta uchafu nipande basi kwenda Dar kwa SSB kumwonesha uchafu wake? hapa JF wanapita jamaa zake Saidi wengi tu, na hata yeye huenda anaingia sana tu humu, UJUMBE UMEFIKA ATEKELEZE WAJIBU WAKE SASA!
 
Last edited by a moderator:
Habari Watanzania na Wasio Watanzania,

Jana nilinunua juice ya Azam ya "tropical mix" ya TZS. 2500,
Nilipofika home nikamimina kwenye glass ili ninywe, nikapiga funda la kwanza nikastuka kidogo, nikapiga la pili nikakutana na radha ambayo ni ya ajabu ajabu sana yani kama uozo ulochanganyika na mafuta ya taa, nikataka nimrudishie mwenye duka ila nikaona niachane naye, nikaenda kuitupa niki-assume labda mwenye duka aliiangushia mafuta ya taa.

Leo tena nikaamua kununua juice ya AZAM sehemu ya mbali kabisa na niliponunulia jana, this time nikanunua juice aina ya "APPLE", basi mida ya usiku hivi baada ya msoc nikaamua nichukue glass moja niipige, nimefika nusu kabla haijaisha nikaiwa nimeiweka ile glass kwenye meza ambapo inapigwa na mwanga direct ndani, OMG... nimeona mauchafu uchafu kibao aisee kwenye glass, nikaanza kujiuliza au glass ni chafu??? Ikabidi nichukue glass kubwa halafu nimimine ile ile iliyopo kwenye box niione nayo, daaaaaaahhhh, aisee ni mauchafu kibao yan.

Hapa nilipo hadi nahisi nishaanza kuumwa, nimeamua kuiweka hapa ili iwe ushahidi nikiumwa walau nikashtaki. (Mungu Aniponye kwa kweli).

Nawashauri wapenzi wa hizi juice kabla hujaibugia uwe unapenda kuangalia ikoje kwanza maana waweza dhurika kwa kweli.

N.B

Sijaweka bandiko hili ili kuvuruga biashara ya AZAM, nop, ninawatahadharisha wenzangu na nilichokiandika ni ukweli mtupu.

Kwenye biashara michezo kama hii ni rahisi mtu kuifanya ili kuharibu biashara za watu, zamani sijui siku hizi kama bado upo. Watumiaji wa soda walikuwa wanakumbana na uchafu kwenye Pepsi au Coca cola! Lakini kwa hili la Azam ni vyema kama mtumiaji si wa Azam pekee bali juisi na vinywaji vingine hasa vya viwandani kagua expiring date na mambo mengine.Lakini kuacha ni juu yako ila kama sie wengine vijoti tunavipiga sana toka vimeanza na hakuna madhara yoyote.
 
shukrani kwa taarifa,ingawa mashtaka yako itakuwa ngumu kwako kushinda kesi kutokana na mazingira yalivyo maana juice umeifungulia kwako,huo uchafu umeuona peke yako,watakuruka mita mia kama ujuavyo wafanyabiashara wanasema kitu kikifika nyumbani hawana imani nacho sababu waweza kuta ww ndo umefanya huo uchafuzi halafu unawatupia shutuma.

hauko sahihi. Uchafu wa siku moja na wa muda mrefu ni viti viwili tofauti.
 
Nishaacha kunywa juice hizo kitambo sana.Tunanunua embe tunasaga tunakunywa,nzuri sana ya kusaga mwenyewe na haina gharama. Tsh 2500 soko la Stereo unapata embe 15 zinatoa juice lita 5 mpaka 6 nachanganya na passion kidogo za sh 500
Safi sana. Tatizo wabongo tuna muda wa kutosha kukaa saluni, kuangalia mechi za soccer la ulaya baa lakini muda kidogo kwa ajili ya kuandaa diets kama hizo tatizo.
 
tblj,Tatizo la Bakharesa amajaza wapakistani na Wahindi,trust me hawa ni mabingwa wa kuchakachua na wanasema tangu kawaleta hao faida imeongezeka maradufu kwani jamaa wamepunguza gharama za uzalishaji kwa kutumia industrial raw materialsa badala ya matunda halisi.Kama mmegundua ata test na texture ya Ice cream zake siku haiko sawa.
 
tblj,Tatizo la Bakharesa amajaza wapakistani na Wahindi,trust me hawa ni mabingwa wa kuchakachua na wanasema tangu kawaleta hao faida imeongezeka maradufu kwani jamaa wamepunguza gharama za uzalishaji kwa kutumia industrial raw materialsa badala ya matunda halisi.Kama mmegundua ata test na texture ya Ice cream zake siku haiko sawa.

Hao viumbe wa hiyo ngambo ya dunia nawavulia kofia kwa uchafu....
 
Inaingiaje shekhe wangu hapo ukafir tena? Au maji na juice za azam ni za msikiti?
Hoja hapa ni ubora na usalama wa bidhaa tuache udini mkuu.
dah! kwakweli leo mumenijuza zaidi juu ya juice ya azam man hata mimi nimpenzi hii bizaa ya juice .kuna ciku nilinunua juice yenye mchanganyiko wa mapera na machungwa nilishindwa kutambua kama ile ni juice au makange ya kuku.hata tumbo lilisumbua kwa mda wa weerk moja toka hapo cinywitena juice ya mapera .
 
dah! kwakweli leo mumenijuza zaidi juu ya juice ya azam man hata mimi nimpenzi hii bizaa ya juice .kuna ciku nilinunua juice yenye mchanganyiko wa mapera na machungwa nilishindwa kutambua kama ile ni juice au makange ya kuku.hata tumbo lilisumbua kwa mda wa weerk moja toka hapo cinywitena juice ya mapera .

Naona unaka wivu kakike kwa mbaaaaaalii
 
Nawashauri ukitaka kunywa Azam juice kunywa ya Embe (Mango), coz hiyo ndo inatoka zaidi so it means haikai sana dukani kama hizo brand nyingine
 
Nimewahi kukutana na kadhia hiyo miezi miwili ilopita. Nilinunua juice ya pera, loh! Imeoza. Na exp date ilikuwa Jan 2014!
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom