Tahadhari: Huu ni msimu wa nyoka!

Tahadhari: Huu ni msimu wa nyoka!

Naomba wajuvi mtuambie ni dawa gani itasaidia kuwapunguza kama siyo kuwafukuza kabisa hawa wadudu?inatisha sana maana nyumbani watoto bado wadogo na ijumaa ya week iliyoisha nilipigiwa simu mchana kwamba wamemuona huyu nyoka wa kijani aki-survey maeneo ya nje ya nyumba.

Nimeuliza watu nilio nao karibu wananiambia oil chafu inasaidia sasa sijui ni kweli!
Watu wengi wamesema mafuta ya taa, oil chafu nk... ila kwa kawaida kama unatakiwa umwagie kwa kuzunduka nyumba nzima na hauwezi mwaga kila mahali... Mafuta yana harufu kali.. Na oil ni uchafu..

Njia rahisi ni kuchoma tairi la gari kwa kuhakikisha moshi umesambaa eneo lote la nyumba... Unaweza kufanya hivi kila baada ya miezi miwili au mitatu kama eneo ulilopo kuna nyoka nyoka
 
ukaota inakukimbiza?? Yesu wangu kama nakuona sijui ungezimia,, mimi mijusi tu naiogopa nikiiona kwa karibu roho inataka kunitoka sembuse minyoka

Yaani nilihisi washaingia tayari. Sasa sijui kwamfano inatokea nimewasha then nikamuona hali inakuwaje

Hadi usiku nimeota manyoka nyoka walah!! Mshana Jr sio mtu mzuri.
 
kUNA NYOKA MWINGINE HATARI wengi hawamjui. Ni kama mwoga ila ukimchokoza ndio asili yake hujionyesha. Green Mamba ni yule nyoka wa kijani. Sifa zake ni kama Black Mamba. Ila Wengi humuita nyoka wa kijani. Ni mpole na kama mwoga vile mana unaweza mkaribia yeye akakukimbia. Ila ukimfuatilia zaidi au akajua unataka kumdhuru ndio dhoruba yake huanzia hapo. Tabia yake inakuwa kama Black mamba.
Kijijini kwetu hua nawaona sana yani mmekutana tu ghafla yeye huyo anaondoka zake
 
Ahsante mkuu nimesoma kiundani kumbe neno MAMBA ni jamii ya nyoka flani ndio sasa kukawa na Black Mamba na Green Mamba.Sasa najiuliza hawa nyoka wa kijani wapole na wembamba tunaokutana nao majumbani ni green Mamba?
Mkuu kuna nyoka mwenye sifa ya hatari Tabora anaitwa Koboko je ndio black mamba.
Hongera wewe ni herpetologist mzuri
Ahsante kunijuza ila Black Mamba anatisha sifa zake kuwa anauma mara nyingi.
Ila anaonekana hapendi bugha ya binadamu bila hivyo wangekuwa wanaingia majumbani watu wangekufa sana
Black mamba ndio huyo ngoboko, Anakuwa mkali pale unapomuingilia kwenye makazi yake...Anaweza kung'ata mara nyingi kwasababu meno hake hayochomoki, na yuko chapu sana (Kuna nyoka wengine wakikung'ata wanakuachia meno, hawa mara nyingi hawana tabia ya kung'ata sana kwa kuhofia kupoteza meno yao)
Black mamba meno ya tunayaita (Fixed fangs) meno yake hayotoki, kwaiyo ukipita kwenye anga zake hakimbii bali anakung'ata kwanza)

Kuhusu hawa nyoka wa kijani tunao aina tatu wanaoweza kuonekana kwenye mazingira yetu

1. GREEN TREE SNAKE = Huyu ni mdogo mwembamba na hang'ati (Hana meno nadhani)

2. EASTERN GREEN MAMBA = Huyu ni mwembamba mrefu kidogo anafika 1.5m kwa urefu, Huyu ni nyoka mwenye sumu kali sana, pia anapendelea kukaa kwenye miti.. Rangi yake ni kijani sana imekolea.... Huwaga sio mchokozi na endapo ukimfata anakimbia... ila anapenda sana makelele... Kwaiyo sehemu mfano za kijijini wanapenda kuwa kwenye miti iliyopo karibu na makazi ya watu au shule

3. BOOMSLANG = Huyu dume ndio anakuwa wa kijani ila jike anakuwa na rangi ya olive au grey au brown....... Rangi ya dume haijakolea sana kama ya green mamba na ukimsogelea karibu ana mistari meusi kwenye magamba, pia ni mrefu kama mita 2 na ana sumu kali sana..... Hawa hawapo wengi kama Green mamba.. ila wapo wapo na kwa macho ya kawaida huwezi kuwatofautisha
 
NosradamusEstrademe
images%20(15).jpeg
Green tree snake
images%20(17).jpeg
Green mamba
images%20(16).jpeg

Boomslang
 
Ahsante mkuu nimesoma kiundani kumbe neno MAMBA ni jamii ya nyoka flani ndio sasa kukawa na Black Mamba na Green Mamba.Sasa najiuliza hawa nyoka wa kijani wapole na wembamba tunaokutana nao majumbani ni green Mamba?
Mkuu kuna nyoka mwenye sifa ya hatari Tabora anaitwa Koboko je ndio black mamba.
Hongera wewe ni herpetologist mzuri
Ahsante kunijuza ila Black Mamba anatisha sifa zake kuwa anauma mara nyingi.
Ila anaonekana hapendi bugha ya binadamu bila hivyo wangekuwa wanaingia majumbani watu wangekufa sana
Green mamba siyo wale tunaowaona kwenye bustani zetu. Wale green mamba hawana black dots na ni wakali hawa wamajumbani wenyewe ni mijusi na wadudu wadogo. Sumu yao unaweza kuishi siyo kama green mamba wana sumu kama cobra 20 min. you are agone..
 
ukaota inakukimbiza?? Yesu wangu kama nakuona sijui ungezimia,, mimi mijusi tu naiogopa nikiiona kwa karibu roho inataka kunitoka sembuse minyoka
Yaani nyoka mie hata picha yake sitakagi kuiona mwili unasisimka kabisa. Bora hata mijusi.
 
Dada kwa huku kwetu Africa ni ngumu
Ukimwona mfukuzie mbali halafu hakikisha unatembea ukiangalia chini usiku; Tunaishi nao na wao wana haki kuishi ila waoga kama sisi. Usimue mfukuzie mbali.
 
Mwaka juzi kipindi kama hiki aliniwahi mmoja... Ila nikumuwahi nikamuua lalijia alinilaza kitandani wiki.... Na hivi karibuni mwenzatu hapa JF naye akapata kasheshe kama yangu naye alilazwa karibia wiki... Hajasema hapa lakini kwa ruhusa yake nitamtaja
 
Watu wengi wamesema mafuta ya taa, oil chafu nk... ila kwa kawaida kama unatakiwa umwagie kwa kuzunduka nyumba nzima na hauwezi mwaga kila mahali... Mafuta yana harufu kali.. Na oil ni uchafu..

Njia rahisi ni kuchoma tairi la gari kwa kuhakikisha moshi umesambaa eneo lote la nyumba... Unaweza kufanya hivi kila baada ya miezi miwili au mitatu kama eneo ulilopo kuna nyoka nyoka
Nadhani na sina shaka hii itakuwa njia nzuri.
 
Back
Top Bottom