Tafuta fedha, elimu na cheo lakini usisahau kuwa maisha ni ubatili, acha kujitesa kwa vitu vipitavyo

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,980
37,027
• Kiasi cha fedha unachokisotea kuna watu walizishika na wengine ni fedha ya kuhonga au ya kufanyia birthday tu.

• Elimu unayoisotea kuna mtu atakupa karatasi kwamba umehitimu, maana yake yeye alishapita hiyo level na hakuridhika nayo.

• Cheo kikubwa duniani kwasasa ni Urais, ni cheo ambacho wengi wamekipata na wamekiacha. Zamani hizo kulikuwa na Rais wa Dunia yote, cheo ambacho sasa hakipo.

Ridhika na ulichonacho, acha kujitesa kwa vitu vipitavyo.
Maisha niliyonayo ukiniona wewe ambaye hujui nilikotoka unaweza kuona sijafanikiwa lakini akiniona mtu wa kijijini kwetu ambaye anajua nilikotoka atasema nimeganikiwa tena sana.
Godoro la kwanza kulalia ni lile la shule ya bweni form one , huko nyuma full kulalia mikeka chini au kwenye vitanda vya kamba.
Viazi pori nyumbani tumekula mara kadhaa ili kujikinga na kifo.
Sasa hivi nyumbani mpaka magodoro ya akiba yapo, nyama sometimes zinachacha.
Baada ya nafsi yangu kuanza kutaka maisha bora zaidi ya hapa ndipo nimegundua binadamu ni kama hana akili, anahangahikia mno vitu ambavyo havijawahi kumsaidia. Vitu vipitavyo, upepo, vanity.
Hakuna mtu aliyewahi kupata msaada wa kudumu kutoka kwenye cheo chake, elimu yake au mali yake.
Hivyo vyote vitakupa furaha ya muda mfupi, tena mfupi sana.
 
Maisha,kifo,pesa,kula kushiba,muda,kiama,maumivu,huzuni,hofu...nk..
Hivi vyote ni illusion tuu🤔🤔
Kuna siku ntakuja kutoa somo ila na amini wachache sana ndio watanielewa
 
Sawa tumekusikia
FB_IMG_1706443785213_1.jpg
 
Ndugu Kiboko ya Jiwe umeongea kitu kikubwa sana, lakini watu wengi hawataelewa hii kitu mpaka karibia na siku zao za mwisho.
Hawa watu ni wabishi.
Mimi nina miaka 37, godoro la kwanza kulalia ni lile la barding school.
Miaka ya 2001-2 tumekula sana viazi pori ili kuziokoa roho zetu nyumbani.
Leo hii kwangu nyama zinachacha.
Lakini naona maisha ni ubatili mtupu
 
• Kiasi cha fedha unachokisotea kuna watu walizishika na wengine ni fedha ya kuhonga au ya kufanyia birthday tu.

• Elimu unayoisotea kuna mtu atakupa karatasi kwamba umehitimu, maana yake yeye alishapita hiyo level na hakuridhika nayo.

• Cheo kikubwa duniani kwasasa ni Urais, ni cheo ambacho wengi wamekipata na wamekiacha. Zamani hizo kulikuwa na Rais wa Dunia yote, cheo ambacho sasa hakipo.

Ridhika na ulichonacho, acha kujitesa kwa vitu vipitavyo.
Maisha niliyonayo ukiniona wewe ambaye hujui nilikotoka unaweza kuona sijafanikiwa lakini akiniona mtu wa kijijini kwetu ambaye anajua nilikotoka atasema nimeganikiwa tena sana.
Godoro la kwanza kulalia ni lile la shule ya bweni form one , huko nyuma full kulalia mikeka chini au kwenye vitanda vya kamba.
Viazi pori nyumbani tumekula mara kadhaa ili kujikinga na kifo.
Sasa hivi nyumbani mpaka magodoro ya akiba yapo, nyama sometimes zinachacha.
Baada ya nafsi yangu kuanza kutaka maisha bora zaidi ya hapa ndipo nimegundua binadamu ni kama hana akili, anahangahikia mno vitu ambavyo havijawahi kumsaidia. Vitu vipitavyo, upepo, vanity.
Hakuna mtu aliyewahi kupata msaada wa kudumu kutoka kwenye cheo chake, elimu yake au mali yake.
Hivyo vyote vitakupa furaha ya muda mfupi, tena mfupi sana.
Tafuta hela jombaa acha kujifariji, lazima ujue kuwa kila eneo lina value yake. Kila mtu anatumikia kile alichowekewa ndani yake. Kwa mfano Bahressa sio kwamba anaamka asubuh kwenda kutafuta pesa chief ila Mungu kampa pesa ili azisimamie kulinda ajira za watu. Ni wajibu tu. Na usisahau kila kitu unachokiona mbele yako kilishaamuliwa na ulimwengu wa roho. Inawezekana huo ulimwengu ni wa giza au wa nuru so huu mwili ni box tu linalotekeleza kile kilichoamuliwa mahali.
 
Uko sahihi hata Mfalme Suleiman alipewa vitu vingi vizuri na alifanya mambo mengi mazuri ila mwisho wa siku alikiri kwamba yote ni ubatili na kujilisha upepo tu.
 
Ndio ni ubatatili ila hutakiwi kuishi kwa mateso ,kikubwa be kind usikubali maskini akupite ,usikubali kuwa mchoyo ,usijinyime ,mtafute Mungu sana thne ishi fear free ,usikubali kuona mtu anapotea kiroho na kimwili
 
Back
Top Bottom