Tafsiri ya neno 'mpumbavu' kadiri ya kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI

GHULA

Member
Mar 3, 2013
77
66
Mpumbavu nm(wapumbavu) Mtu anayeshindwa kuelewa jambo hata akielezwa, juha, zuzu, jura, nyange, baghami, bahau, hambe, maarasi, zebe, mbumbumbu.

**************************************************************************
Amevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoapa kuilinda na kuitetea

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 13(2) inasema: "Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka sharti lolote ambalo ni la kibaguzi ama wa dhahiri au taathira yake."

Kifungu cha nne cha ibara hiyo hiyo kinasema: "Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi."

Katiba Ibara ya 13 (6) (e) inaonya kuwa: "Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha, pia Ibara ya 16 ya Katiba inasema: "Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi ya nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na pia heshima na hifadhi ya maskani na mawasiliano yake binafsi."

KAULI:

…………………WAPIGWE TU, TENA NAMI NASEMA PIGA, TUMECHOKA…………………..

Pinda akishinda mahakamani hawezi kushinda kwa Mungu. Yeye amesema wamechoka; je, yeye na nani wamechoka? Mbona wengine tunafurahia changamoto za kisiasa zenye mwelekeo wa kuizindua jamii kwa elimu ya uraia? Time will tell!
 
Pinda ni wakuuliwa mara moja kwa risasi anazoshabikia hawezi kuanzisha na kutangaza vita kati ya polisi na wananchi haiwezekani anyongwe bila kusubiri tukamalizana
 
Mpumbavu nm(wapumbavu) Mtu anayeshindwa kuelewa jambo hata akielezwa, juha, zuzu, jura, nyange, baghami, bahau, hambe, maarasi, zebe, mbumbumbu.
 
Mh. Joseph Mbilinyi alikuwa sahihi kusema Pinda ni mpumbavu, Pinda by professional tunaambiwa ni mwanasheria lakini amekuwa ni mtu wa kwanza katika uvunjaji wa sheria inawezekana ana hang over ya madaraka. Hakishindwa kutumia busara na hekima ku overcome challenge za ushindani wa kisiasa basi ajue lazima akutane na majibizano makali kutoka kwa wapenda mabadiliko kama Sugu.
 
Serukamba wala hakukamatwa au at least kukemewa kwa lile neno la kiliberali!

Ndani ya bunge, Serukamba alitukana tusi ambalo kumbukumbu zote zimeonyesha kuwa halija wahi kutolewa na mbunge yoyote kwenye mabunge yanayo fuata utamaduni wa jumuiya ya madola lakini kwa kuwa yeye ni mccm hakuguswa wala kukemewa.

Neno Mpumbavu si tusi ndio maana hata kamusi sanifu ya kiswahili haijalitafsiri kuwa ni tusi, labda tuelezwe kuwa linakuwa tusi linapo tumika na wapinzani dhidi ya watawala walio vimbiwa madaraka.

Sasa hivi kwa jinsi ccm walivyo kwenye state of panic lolote kwao linalo toka kwa wabunge wa chadema wanalitafsiri kama tusi au uchochochezi.

Kesho huenda hata Tundu Lissu akakamatwa kwa kupiga sana chafya kwenye viunga vya bunge kutokana na kuwa na mafua, hiyo itaitwa uchochezi kutoka kwa maadui wa nje.
 
Ijapo kiburi . ndipo ijapo aibu ,mkemee mjinga katika ujinga wake maana atakusikia na kujisahihisha,lakini usimkemee mpumbavu katika upumbavu wake asije akakudhuru , ukitaka jua umemkemea mpumbavu .atakudhuru tumeanza kusikia shika shika zimeanza
 
Je kwa tafsiri hiyo Pinda ni mpumbavu au la? Mie nasema siyo mpumbavu je wewe unasemaje ni mpumbavu? Je kama ni mpumbavu nani aliyemteua? Je unaweza kuteua mtu mpumbavu? Hapana Pinda siyo mpumbavu, Pinda aseme na kukiri mwenyewe kwamba hapana yeye si mpumbavu, pumbavu, pumbafu hapana!
 
Ndani ya bunge, Serukamba alitukana tusi ambalo kumbukumbu zote zimeonyesha kuwa halija wahi kutolewa na mbunge yoyote kwenye mabunge yanayo fuata utamaduni wa jumuiya ya madola lakini kwa kuwa yeye ni mccm hakuguswa wala kukemewa.

Neno Mpumbavu si tusi ndio maana hata kamusi sanifu ya kiswahili haijalitafsiri kuwa ni tusi, labda tuelezwe kuwa linakuwa tusi linapo tumika na wapinzani dhidi ya watawala walio vimbiwa madaraka.

Sasa hivi kwa jinsi ccm walivyo kwenye state of panic lolote kwao linalo toka kwa wabunge wa chadema wanalitafsiri kama tusi au uchochochezi.

Kesho huenda hata Tundu Lissu akakamatwa kwa kupiga sana chafya kwenye viunga vya bunge kutokana na kuwa na mafua, hiyo itaitwa uchochezi kutoka kwa maadui wa nje.

Mkuu, bado msimamo wako kuhusu upumbavu ni ule ule?
 
habarini wakuu wa jukwaa hili la lugha yapo maneno ambayo kwa hakika yamekua yakiitumika kwenye jamii yetu na kuonekana ni matusi ila kwa upande meingine yakionekana sio matusi. Mwenye kujua maana halisi ya maneno haya na matumizi yake naomba anitoe kwenye utata huu
1.Mpumbavu
2.----
3.Mjinga
4.Lofa
 
1. Mpumbavu- ni mtu asiye jua kitu na hataki kufundishika na anaamini yeye yupo sahihi hata akielekezwa haelekezeki

2. ???

3.mjinga - huyu yeye hajui kitu lakini ni mwepesi kujifunza na anafundishika na anakubali kufundishika

4. Lofa- huyu nu mtu ambaye hana kitu kwa maana ni maskini mali na akili na hana mawazo ya maendeleo , hajitumi karidhika na hali yake ,kakata tamaa na maisha,
NDIVYO NIJUAVYO MIMI.
 
Back
Top Bottom