Tafrani Kimara: Msongamano kituo cha Mwendo kasi - Abiria wakiwemo wanafunzi wazimia!


Kosa kubwa sana lililofanyika wakati wa inception ya UDART ni kusitisha traditional routes ambazo miaka kwa miaka zimehudumia wakazi wa Dar es Salaam kwa kuamini kuwa UDART wange- substitute huduma hiyo at a satisfactory level. Monopoly hata siku moja haijawahi kuwa na ufanisi, kwa hiyo routes zote za zamani zilitakiwa ziende parrallel na UDART services ili wapeane changamoto
 
Mkuu hana haja ya kumpa onyo mtendaji wake. Aamuru mabasi yaliyopo bandarini yatoke yaingie barabarani huku kodi yake au tozo lolote linalodaiwa liendelee kulipwa. Kumbukumbu hazipotei tena siku hizi kwani tuna hifadhi nzuri.
Huu mpango wa kuzuia mabasi 70 miezi sita yakiwa hapo hapo darisalama ni upuuzi. Yaachiliwe mara moja yawe rodini huku mkikamatana mashati ya kodi mengine 70 yaingizane tena. Mnapoyazuia wasafiri ndo wanaumia
 
Pamoja ni kisa cha hizo bus 70, hivi kweli abiria wameongezeka kiasi hicho au kuna magari yameharibika au yamepaki kwa sababu nyingine yeyote?

Nakumbuka mwanzo wa mradi haya yaliyopo sasa yalikuwa yanatosha kiasi chake sio kama sasa.
Thats my question.

Iweje magari yapungue kwa kasi hivyo? Mwanzoni hakukuwa na hali kama hii.
 
Nadhani tatizo ni sheria zinazosimamia suala la kodi na sio TRA.

Hayo magari hayajazuiliwa kwa bahati mbaya. Kuna sehemu walitegemea upenyo na umezibwa.
 
Serikali ikisimamia ndo unakufa kesho yake.

Reli ya mwakyembe ipo juu ya mawe.
 
Sasa walinunua mabasi 70 halaf hawana hela ya kuyalipia kodi kwann?!kwani wangenunua mabasi 40 wakayalipia kodi yafanyekazi si ingekuwa bora zaidi..sasa mabasi yamekaa bandari tu si hasara kwao

Upuuzi mtupu wa hao watendaji
Nadhani walitegemea kupewa msamaha wa kodi.
 
Huo mradi wameaumua kuuvuruga maksudi kabisa.
Mwanzo walianza vzur mno.tarataibu wakaanza kupunguza mabasi na kuacha machache ili kujilikimbikizia faida tele huku wananchi tukiteseka.
Kama kawaida ya mchawi hatoishia kukupoga zongo tu atafika mbali wameenda wameua mfumo wa max uliokuwa unakusanya mapato kwa ufanisi alafu saizi wanalalamika wanahujumiwa?.
Viongozi wetu hawa ni vilaza wa hali ya juu wako kwa matumbo yao na kupeana tenda kindugu ndugu sana.
Warudishe dala dala waache ukiritimba wa kutesa watu.Mwendokasi ilikuwa ni mradi wa ukombozi lakin kama kawaida ya viongozi wa africa watafanya lolote lile wananchi wao waendelee kusota na kuishi kwa tabu hata kama kuna neema imeletwa.
Kuanzia miradi,madini,na rasilimali lazma wananchi muwe wahanga wa baraka mliozletewa.
Huyu simon kisena ni nani mpaka hagusiki hivi maana mwendokasi watu tunalia karibia mwaka na watu wameziba masikio?
Da tz hii n laana tupu.
 
Sheria za kodi lazima ziheshimiwe.
 
Naskia wfanyakazi hpo wamechezea kichapo toka kwa abiria

Ova
 
Sheria za kodi lazima ziheshimiwe.

Huo ukiritimba ndio umetufikisha hapa tulipokwamia. Sijasema kuwa wasilipe kodi. Nimesema, mabasi yatoke huku mkivutana kodi zenu watu wasiteseke. Huyo anayebishana miezi 6 bila mafanikio HATUFAIIIII. Peleka malalamiko yako huku huduma ikiendelea. Hata ipite miaka 10 utalipa hiyo kodi stahiki tu. Nyiye ndo mnaacha mganjwa afe kisa alisahau kadi ya kiliniki nyumbani. Nyie ndio mnaacha majeruhi abubujike dam hadi kufa kisa hana PF 3. Nyie ndo mnaacha mama anajifungulia kwenye kituo cha polisi kisa mume wake amekimbia polisi alipokwenda kukamatwa. Acheni huo ukiritimba utatumaliza
 
Sheria za kodi ziheshimiwe. Kwa nini alileta basi huku akijua kuzitoa lazima uzilipie?
 
Ukabila ndiyo unaosumbua mradi Huu, hakuna haki lawama anapewa mtu amabaye anatimiza maudhui ya mradi, wakati wasukuma wanaachiwa wapige pesa, ni mungu tuu atatutoa hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…