Tafiti: Wanawake ni wachache wanaojifunza 'Coding'

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,017
9,885
1240334C-85FC-4828-9AAD-3B65E29CA05A.jpeg


FreeCodeCamp ni mmoja kati ya mtandao unaotoa elimu nyingi kuhusu kuandika ‘codes’ ili kutengeneza ‘projects’ mbalimbali ikiwemo kutengeneza ‘App’ za android, vikokotoo na tovuti

Hivi karibuni wamefanya tafiti kwa watu 65,000 na mtokeo yalionyesha kuwa wanawake 7.7% walikuwa wanajifunza, wakati wanaume wakiwa ni 91.7%

Mbali na matokeo hayo, pia tafiti hiyo imeonyesha kwenye ramani waliyoambatanisha na matokeo yao kuwa ni watanzania wachache wanaojifunza zaidi kuhusu mamb mengi yanayohusu mtandao

52156397-62ED-403C-8929-3D9FBFA980DA.png

C8368D30-94CC-4996-8D94-79CEB8C5F4FC.png


Soma matokeo ya utafiti freecodecamp
 
"... ni watanzania wachache wanaojifunza zaidi kuhusu mambo mengi yanayohusu mtandao."

💯 ni wachache sana! Mtandao ni sehemu ya teknolojia na future ya maisha kwa namna yake, lakini vijana (waTanzania) wameshindwa ku-cope na hii aspect.

Muda utadhihirisha haya, tayari wakiwa wamechelewa.
 
Hata vyuo navyo ni changamoto,mfano mkoa wa pwani pamoja na kuwa lelemama lakini vyuo vya ICT ni vyakulenga kwa manati sa watajifunzaje
 
Hizi kitu zinafaa sana kuanzia kwa vijana wadogo wanaokuwa na nafasi, muda na kuwezeshwa hawa wanaweza kufanikiwa na kuwa na upeo mzuri kuliko kijana mtu mzima ambaye anataka mafanikio ya haraka.

Ukizingatia umri wa maisha hapa duniani ni mfinyu sana kuliko unaotumika shuleni.



Swadktaa!! Get them while they are young! And I bet wakianza tangu utotoni wakike watakua wengi zaidi maana girls wako inquisitive sana. Ukubwani ni wanawake wachache sana wenye muda physically + mentally wa kupambana na haya madude!
 
Masomo ya sayansi kwa ujumla wanawake ni wachache,kiduchu.Darasa langu la a phys lilikuwa na wanawake 2/26tu hio ni digrii level kwenye masters huko sijui ikoje! Wanawake wanauwezo was kukariri na si kufikiri, ndio maana mpaka sasa ktk ulimwengu wa IT innovation nyingi ni za wanaume kuanzia Facebook,tweeter,window,wasap nk
 
Hapo wamenihesabia na mimi ambaye tangu nijiunge nimeitumia kama mara moja tu.
 
cha kushangaza ni kwamba coder wa kwanza alikua ni mwanamke. Nadhan ubongo wa mwanamke upo vizuri kwa coding lakini ni kukosa juhudi tu. Kwa mwanaume ubongo wake hauko adapted sana kwenye coding lakini ile hali ya kutia juhudi tu ndo inafanya wanaume wengi kuwa kwenye coding zaidi ya wanawake.

Chukulia mfano kipindi cha world war II kuna group la wamama walikua wanaitwa human computers. Vile vile akina Ada na yule mama
alieandika compiler ya kwanza. Inshort wanawake wakiamua kuingia kwenye coding wanaweza sana sema tatizo ni juhudi na majukumu fln fln
 
Coding inataka mda, na kusoma sana, ili uwe updated..

Sasa , unataka ufanye coding, huku unawaza kulipa kodi ya pango, kibongo bongo inakuwa ni ngum sana

Solution:

Haya mambo itabid mtu aanze akiwa mdogo, mpk anafika stage fulani, anakuwa ana uwezo wa kufanya project fulani.
 
Ukiongelea masuala ya coding nawaza tu jinsi ya kuipata coursework ya Programming.
 
Shida haya makomputer yanatuharibu macho mimi mwenyewe nilijifunza kwa miaka 2 kwa kufuatilia tutorials za Bucky Roberts lakini niliishia njiani baada ya haya macomputer ya kichina kuanza kuniumiza macho
 
Masomo ya sayansi kwa ujumla wanawake ni wachache,kiduchu.Darasa langu la a phys lilikuwa na wanawake 2/26tu hio ni digrii level kwenye masters huko sijui ikoje! Wanawake wanauwezo was kukariri na si kufikiri, ndio maana mpaka sasa ktk ulimwengu wa IT innovation nyingi ni za wanaume kuanzia Facebook,tweeter,window,wasap nk
Hamna ukweli wowote kwenye maelezo yako,zungumzia mambo mengine kama majukumu ya familia na vitu vingine ila issue ya intelligence wapo wanawake wengi tu wenye intelligence sawa na au hata kuwazidi wanaume. Kali linux kamzungumzia ada lovelace .programmer wa kwanza kabisa anaetambulika na alikua ni mwanamke.
 
Back
Top Bottom