Waleta Mabadiliko: Kutana na kizazi kipya cha wajasiriamali wa Kashmir

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
322
255
Makala hii ilichapisha
Mei 18 2022, kwenye gazeti la G.K

Huku kukiwa na ongezeko la janga la ukosefu wa ajira huko Jammu na Kashmir, vijana wachache wasomi wasio na ajira wamejitengenezea njia ili kuunda njia zinazofaa za ajira na kuwafanya kuwa ni waleta mabadiliko katika ukuaji wa uchumi wa J&K.

Wakati serikali ya Jammu na Kashmir ikidai kuwa imetoa miradi kadhaa yenye kuwagusa wajasiriamali wengi na vitengo vyao chini ya miradi inayofadhiliwa na serikali kuu, wajasiriamali wa ‘GenNext’ wa Kashmir wanatoa simulizi zao kwa hadhira ya kimataifa.

Kisa kimoja chenye kutia moyo ni kuhusu kijana anayependa sana shughuli za michezo. Adnan Ali Tromboo, mwenye umri wa miaka ishirini na sita kila mara alitamani kuendeleza maono ya baba yake.
“niliota kuendeleza historia halisi ya kazi za mikono mashuhuri za Kashmir, ili kwamba ieleweke na kuweza kutumika dunia nzima kwa ajili ya kusaidia wanasanaa kwa urahisi.

Nilikuwa na maono yaliyokuwa yakibeba nilipokuwa na nilipofikia sasa, imekuwa ni ndoto zangu za kila siku zilikokuwa zinakua kadri miaka ilivozidi kwenda” alisema Adinan Ali Tromboo.

Nyumba ya Adnani imekuwa ikibeba uhalisia na mandhari ya Kashmir, ijapokuwa ni mazingira ya tofauti. Wazazi wake walikuwa na uwezo wa kurithisha na kufundisha tamaduni hata katika mazungumzo yao na Imani ya kuirithisha tamaduni hiyo.

Mchanganyiko na muunganiko wa tamaduni mbali mbali ulimpa ufahamu wamasuala mtambuka

Baba yake Adnani aliaga dunia wakati Kiajana wake huyo akiwa bado hajakomaa katika uendeshaji wa biashara mazingira yaliyomfanya kubeba jukumu la moja kwa moja wa kuendesha biashara yaa familia

“Nikiwa na kazi iliyokuwa haijakamilika mbele yangu, jambo hili liliniogopesha . Lakini Imani kubwa kutoka kwa familia yangu, marafiki na wafanya kazi wenzangu ulinisaidia kuziba mapengo yote katika kujifunza maono ya kazi za ufundi za Tromboo na kufanya maono hayo kudhihirika na kuweka historia ambayo kila mtu angependa kuhusika nayo” alisema Adinan

Adnan alitaka kutengeneza urahisi wa kufikiwa kwa ulimwengu mzima kwa kila mtu mwenye mapenzi na kuhusika na kazi ya upendo unaohamishwa kwenda katika kazi nzuri za kisanaa.

“Ijapokuwa bado tulikuwa tukijihusisha na kufahamika kimataifa kupitia mitandao ya wateja wa muda mrefu wa reja reja, mabadiliko ya kimasoko yalifanya uwepo wa biashara za mitandaoni pamoja na zisizo za mitandaoni kuwa na umuhimu sawa ili biashara husika kuwa na mzunguko zidi, na hapa ndio nilipoanza safari yangu.

Niliokoteza pale baba yangu alipoishia na kuisukuma zaidi bishara yetu ili iweze kutambulika kitaifa na kimataifa pia,” alisema.

“Utambuzi huu ulitusaidia kupata mialiko na nafasi katika matamasha ya kisanii ya kimataifa ambapo tuliweza kuonesha kazi zetu za kitamaduni za Kashmir. Tumeacha alama katika maonesho ndani ya Australia, USA ikiwa imeungana na inchi kama Oman, UAE, Qatar na mataifa mengineyo” aisema Adnan

Wakat mabadiliko ya thamani ya fedha mwaka 2016 na utekelezaji wa GST mwaka 2017 ulipolikumba soko bila kutarajiwa mwaka 2018 ilikuwa ni kazi za Sanaa za Tromboo zilizotuinua kwa kupata kwenye kazi za kisanaa 22 zilizoendeshwa katika mji wa Noida, NCR na EPCH ( Export Promotion Council for Handicrafts).

“Kazi zetu zimeendelea kufahamika na kuonekana kuwa moja ya kazi nzuri India ndani ya miaka ya 2018,2019,na 2020,” alidai

Kikundi cha Kashmir cha Amerika ya kaskazini

Aliendelea kueleza kuwa 2018 waliweza kuhusika katika mkutano wa tatu wa kikundi cha Kashmir kilichopo Amerika Kaskazini (KGNA) kilichofanyika Los Angeles,CA. mamia ya wana Kashmir wanaoishi Amerika ya Kaskazini pamoja na Canada walikutanika kusherehekea, kuelimisha na kuendeleza mila na desturi za Kashmir.

Kikundi cha Sanaa cha Tromboo kilikuwa moja ya wafanyabiashara wakubwa waliosaidia KGNA kuweza kuweka historia nzuri ya urithi na tamaduni za Kashmir kama kumbukumbu kwa wote waliohudhuria ambao walitoka katika jamii tofauti tofauti na umri tofauti tofauti ndani ya Kashmir,”Adnan alisema na kuongeza

“Ndani ya mwaka huo huo tuliweza kuingia katika soko la Australia kwa kujumuika katika mkutano mkubwa wa 9 wa kimataifa wa Australia mwaka 2018, uliofanyika mji wa Melbourne, Victoria.

Hili tukio la B2B ni moja ya matukio makubwa yanayojulikana yanayofanyika kila mwaka ndani ya Australia yanayotoa na kuonesha mavazi mbali mbali. Matukio kama haya yamesaidia kukuza uelewa wa masoko na kusaidia kujenga jina la bidhaa zetu Zaidi.” alisema.

Kufuatana na mfululizo wa kuacha alama katika masoko yaliyoendelea, tulifanya maonesho katika nyumba ya Sanaa ya Torrance na kituo cha mkutano cha Torrance, California.tulikuwa na muda mzuri tukihusiana na watu mbali mbali katika maonesho pia tukibadilishana na kutoa historia ya Sanaa ya kwetu.

Japokuwa kikundi cha Sanaa cha Tromboo kilikuwa kimejipanga kupeleka mbele zaidi Imani yao ya biashara, kilikutana na changamoto katika utengenazaji wa umoja wa himaya ya Jammu na Kashmir baada ya kufutwa kwa sheria ya kifungu 370. Baada ya sheria za uviko-19 kuwekwa iliathiri sana mzunguko wa biashara yao.

Vizuizi vilikuja wakati wafanyabishara na wanasanaa wanahangaika kutengemaa baada ya matokeo ya mafuriko ya mwaka 2014 na mabadiliko ya fedha ya mwaka 2016 na GST,” alisema

“kama wanavosema, palipo na nia pana njia. Hapa katika kikundi cha Sanaa cha Tromboo, tulitumia mda huu kujitegemeza na biashara za mtandaoni pamoja na kujenga uhusiano na watu mbali mbali kwa kuendelea kutoa historia ya Kashmiri katika mitandao ya kijamii.

Tulipokuwa tunafanyia kazi utengenezaji wa jina kwa kazi yetu, Ilitujia kwamba tuna kila kitu kilichopaswa,kilichokuwa kinahitajika ni muongozo wa muelekeo sahihi. Zoezi zima lilichukua mda, lakini matokeo yake yalileta bidhaa zenye muunganiko wa Sanaa za kitamaduni and dhana ya usasa pia.

Kila bidhaa ilikuwa na historia nyuma yake kitu ambacho kilileta upekee na utofauti wa ununuzi wa kila bidhaa kwa upekee wake. stori hizi ndizo zilizotutofautisha na kutupa upekee na pia kutusaidia kuonesha kila moja kwenye mitandao ya kijamii.

Anasema katika kuendana na njia zetu za ufanyaji kazi ilikuwa kwa njia ya kibanda cha Pernia ambapo tulikuwa moja ya kazi za kisanaaa kutoka bonde letu kuwekwa kwenye maduka yao na tovuti yao.” Adnan alisema

“Tuliamua kubadilisha mfumo kwa haraka ilivowezekana baada ya masoko kufunguliwa baada ya janga la uviko-19. Kikundi cha Sanaa cha Tromboo kilikuwa tayar kimekuwa kuwa kampuni kwenye rekodi na kilichohitajika ilikuwa ni utambuzi. Kwakuwa uwepo wetu wa kwenye mtandao ulikuwa umeshafanyika, tulichukulia kama nguvu yetu na tukaweza kuandikishwa kama chapa halisi.

Nembo na jina letu linabeba historia ya urithi wetu pamoja na ahadi yetu ya kuwa halisi kwa kila mtu tutakaegusa maisha yake kupitia kazi zetu za Sanaa.”Adnan alisema

Kikundicha Sanaa cha Tromboo kilikuwa na kitaendelea kufanya kazi kwa muendelezo kitu ambacho kitampa motisha Adnan kuendelea na maono mapya na kuzidi kuweka malengo ya juu zaidi na kufanya kazi kwa bidii kuyatimiza juu ya kuonesha sanaa na ufundi wa Kashmiri katika ramani ya Dunia.

‘uzaliwaji wa udugu na urafiki wa milele wa Kashmir’

Kila mwaka, Jammu na Kashmir huona baadhi ya historia za kusisimua- zikichua nafasi muhimu. Kwenye moja ya matukio, marafiki watatu waliosoma wote- ambao kama wapambanaji wengine katika miaka yao ya 20-25 walikuwa wakijaribu kutengeneza njia kwa ajili ya kazi.

Muda mrefu wa sheria za Uviko-19 ulikuwa umeanza kusihia, ndipo watatu hao walipoamua kukutana baada ya muda mrefu wa miaka mitatu wa kuwa katika majimbo tofauti wakati wa masomo yao ya kupata shahada.

Kwa Mehr Shaw, Daheem Amin na Shoaib Gutto,’Chai pe Charch’ walikuwa wakikumbushia miaka yao ya ubora ndani ya DPS,Srinagar kama wanafunzi wa biashara, jinsi siku zao za chou zilivyopita na hatimaye nini kilichofuata?

Kulikuwa na wasiwasi baada ya kutokea COVID -19 na kubadilisha mwelekeo wa hali ya maisha, uchumi na elimu kuwandivyo sivyo

Jioni ilipofika marafiki watatu wakaunganisha akili zao kwa matumaini na kuanza kutafakari juu ya uchaguzi mpya

Baada ya siku 3, Mehr aliwapigia simu, akiwa mwenye furaha sana na akawataka wakutane mapema zaidi.

Alinunua kwa chupa ya glasi iliyotiwa rangi na kwa haraka akawamiminia marafiki zake kinywaji cha rangi ya dhahabu.

Kwa kawaida, walianza kunywa kutoka kwake na kutoa pongezi za kweli juu ya ladha na upya wa juisi yake.

Voila! NI watu hawa! Na hivi ndivyo Juice ya Maiden ilivyopewa jina katika Kashmir
Ikiwa ni Juisi ya Tufaha ya kwanza iliyozalishwa kwa mazingira ya baridi ya Kashmir bila viungio au vihifadhi.

Kutoka katika historia ya miaka 50 iliyopita ambapo babu wa Mehr, Muft Abdul Gani, aliyekuwa akisifika kupenda asili na akifanya shughuli za kutafuta matunda maeneo ya mbali ya Ladakh mji usiokuwa na bandari suala la kupata Matunda mapya ilikuwa ni ndoto isiyowezekana

Lakini sasa Juisi hii ya Tufaha, imeleta matumaini mapya kwa kuchanganya ujuzi wa uzoefu wa wazee, wakulima na watendaji na kufanya adha ya kutopatikana matunda kuwa historia

Akiwa na historia ya ugonjwa wa kisukari, Mufti alibainisha kuwa mfumo wa juice yake hauna sukari bali ni glucose iinayoipa Juisi hiyo ladha ya kipekee ya kibiashara

Anasema sasa imeshapita vizazi vitatu kutoka kwa baabu yake na familia yao imekuwa ikipendwa kwa zaidi kwa kuzalisha virutubisho vyenye faida kiafya

“Hata hivyo, ili kuileta kwa watumiaji, tulilazimika kufanya utafiti kuanzia mwanzo; ujuzi wa sekta ya Chakula na Vinywaji, kufanya upembuzi yakinifu na kuandaa ramani ya barabara.

Kadiri ilivyokuwa rahisi zaidi, ndivyo mchakato mzima uliofuata ulivyokuwa wa kutisha. Juisi ililazimika kupitia maabara mbalimbali za majaribio ndani na nje ya Kashmir ili kufikia viwango vilivyowekwa na Mamlaka ya Usalama wa Chakula na Viwango vya India (FSSAI.)

"Hapa tulianza kufanya mabadiliko machache katika juisi kwa udhibiti wa ubora na kusawazisha wakati huo huo tukifanya kazi kwa leseni," anasema Mehr.

"Kwa hili, tulitafuta usaidizi kutoka kwa SKUAST na mwongozo wa kitaalamu kuhusiana na kilimo cha bustani na usindikaji wa chakula."

Safari hii pia, ilijaa kukata tamaa na matumaini, ya mara kwa mara na vile vile katika nyanja kadhaa, kwa kuwa wakati mwingine matokeo hayaakuwa sawa

Anaeleza kuwa mara kwa mara kulitolewa maoni kuhusu jinsi bidhaa zetu zingeanguka kwa sababu ya mwonekano wake usio na mvuto, usio na unyevu na ukosefu wa vihifadhi.

“Unaona? Hiki ndicho kiwango ambacho tumekuwa tegemezi sana katika usindikaji wa bandia kiasi kwamba bidhaa asilia inaweza kuonekana kama mradi ngeni au ubatili”.

Anasema kwa kuwa walidhamiria timu yao ilifanya kazi kwa bidii katika kufanikisha mradi huu na hivi karibuni iliongeza Siki ya Apple na Asali kwa bidhaa zao huku zikwa na ubora wa juu.

Kile kilichoanza kama kinywaji cha kuongeza nguvu mwilini, wapenda michezo sasa ni bidhaa inayopendwa sana na kila aina ya wanunuzi wanaofahamu.

Safari ya MK.kwenye maduka ya reja reja

Maiden anasema bidhaa zao zinaendelea kupendwa kutokana na ubora wake na sasa zinaingia kwenye maduka ya reja reja kwenye miji yote ya Kashmir na Delhi

Kwa nini hawakuchagua njia ya kawaida ya kutafuta kazi za serikali, Ushirika.

Wanasema wakati mwingine, maisha yanamuelekeza mtu ni wapi anaweza kufanya vizuri zaidi na kueleza ushirika wao watatu ilikuwa ni jaambo kubwa zaidi

Anasema siyo kwamba hawakufaanya kitu kabisa juu ya kutafuta kaazi kaatikaa makampuni bali muda mfupi waliofanya kazi walikuwa wamkirudi wanajikuta wanachoka na kukata tamaa”anasema Daheen

Sio kwamba tuna kitu dhidi yake au hatukujaribu, tulifanya! Tulikuwa na muda mfupi katika makampuni, na kurudi tu, tukiwa tumechoka na tumekata tamaa, "anasema Daheem.
"Bila shaka, usalama wa kazi unaotolewa katika ajira za Serikali ni wa thamani na hivyo ndivyo ingekuwa manufaa lakini hisia ya kupotea katika hali hii katika miaka yako ya mapema ya 20 inaua zaidi", anasema Shoaib.

Mehr, ambaye ana shahada ya ya kwanza ya Saikolojia, Mafunzo ya Mazingira na Ujasiriamali kutoka Chuo Kikuu cha Ashoka, mojawapo ya vyuo vikuu vikuu nchini India, ana maoni tofauti i

"Nimebarikiwa kuwa katika mpangilio mzuri wa elimu katika maisha yangu yote". Ninawashukuru walimu wangu kwa kunijenga kujiamini walijitolea kwa mioyo yao wote hasa DPS Srinagar kwa moyo wake chanya na shauku.

"Hamu yangu ya kuchukua masomo tofauti na juhudi zangu za ujasiriamali zilinituma huko Ashoka, haswa. Nilijifunza vitu vingi vilivyoniongezea uzoefu mbali na uoeo wa macho yangu

"Nilitaka kufanya kitu ambacho ningeweza kuweka katika ubora wangu. Kwa Shoaib, ambaye ni mhitimu wa Masomo ya Biashara kutoka chuo kikuu huko Bangalore,anasema kwake haikuwa rahisi hata baada ya kuhitimu. "

Sikutuma maombi ya nafasi za chuo kikuu, kwa sababu nilijua wazi hata kama mambo ya kawaida yangetokea, ujuzi wangu wa ubunifu au ungesimama

Tulijua tunaweza kushindwa katika uanzishaji huu au hata kufanikiwa lakini hatua ya kutojaribu ingekuwa ya kutisha zaidi kuliko kutofaulu. Kila mtu ana safari zake za kutalii ndani na nje.

"Ninaamini sana tutaweza tu kuchagua kazi inayorufaa kila wakati ikiwa tutatambua sisi ni nani Kila kazi au kazi inaweza kuwa ya kufurahisha mradi tu ujue kuna wito kutoka kwayo na unaendelea kuisikia,” anasema Daheem.

Kuanzisha uanzishaji sio rahisi kama inavyoonekana. Kulikuwa na awamu ngumu ambazo bado tunapitia. Sekta ya chakula inakuja na changamoto na ahadi nyingi. "Licha ya kukokotoa kwa uangalifu, masuala yanaweza kutokea bila kutarajia, na kukufanya uamini kuwa uko kwenye mteremko na huna wakati wowote wa kutafakari tena na wakati huo huo kudai hatua za haraka," anasema Daheem.

Kwa bahati nzuri, kama timu wanaweza kusaidiana katika nyakati hizi ambazo hazijawahi kutokea.

Hapo ndipo wanapokabiliana na hali ambazo hakuna elimu au mshauri angeweza kuwatayarisha kukabiliana nazo.

"Hali hizi zimetufanya tutambue kwa kina ukosefu wa usalama ambao biashara inaweza kukuweka ndani. Hata hivyo, hatujawahi kuhisi haja ya kuahirisha au kukumbushana kuhusu njia nyingine mbadala za kitaaluma.”

Tuanhisia ya kufanikiwa zaidi na kuwa juu kwa kutumia uzoefu wetu kama washirika.

"Uongozi na Jambo la Wanawake"
Kwa Mehr, kufanya kazi na wanaume hasa iwe timu yake au nyanja inayotawaliwa na wanaume ya ujasiriamali imekuwa ni sehemu yake ya kuendesha gari kwa kasi.

"Wakati wa mafunzo ya kuwa mwanasaikolojia ambayo ni taaluma yangu ya kitaaluma, nina uzoefu mkubwa wa kufanya kazi katika mipangilio kadhaa, uzoefu wangu katika uwanja wangu wa nyumbani umekuwa tofauti".

Wakati nilikuwa nimejiandaa kiakili kwa hilo, kumekuwa na mambo ya ajabu ya sekta ya biashara, ujasiriamali ambayo ninajaribu kushughulikia kwa ufasaha,” anasema.

"Kumekuwa na wakati ambapo juhudi na sauti ya mtu haikubaliki au kuwekwa kando haswa katika tasnia inayotawaliwa na wanaume, lakini bidii yangu daima imekuwa ikinifanya nishinde

Ninahimiza kwa dhati juhudi zaidi na kuhimiza ubia zaidi wa ujasiriamali kutoka kwa wanawake na kuwa wadau katika uwanja huu kwa kuwa itasaidia kuthibitisha uwezo wao
Nikiwa nimetoka katika familia ya wanawake wenye nguvu, waliojitengenezea wenyewe ambao wote walijiwezesha kiuchumi katika uwezo wao wenyewe, kutokana na ufumaji wa shela hadi wasomi na biashara tangu vizazi vitano vilivyopita, sikulazimika kutafuta nje mifano yangu ya kuigwa.”

Anasema kwamba mahitaji yake ni kuunda nafasi yake mwenyewe, uhuru wa kifedha na kuwezeshwa kwa uwezo wake mwenyewe linatoka ndani yake tangu allipokuwa akijifunza kutembea.

Kuwezeshwa kunatoa aina tofauti sana ya uhuru na msisimko kwa kila mwanamke, iwe katika ufundi, kilimo, taaluma au ulimwengu wa biashara.
"Kama jumuiya iliyounganishwa kwa karibu, kuna haja kubwa zaidi ya kuunda nafasi salama na mazingira mazuri ambapo watendaji wanawake wote wanaojishughulisha wanaweza kukua na kuendeleza kikamilifu maeneo yao wenyewe na kutimiza sehemu yao katika kuimarisha uchumi wa eneo hilo," Mehr anasema.

'Wanawake na Ustawi wa Kiuchumi'

Hali halisi ya Kashmir ina changamoto na vikwazo vyake lakini kwa bidii na matumaini, mtu anaweza kushinda vikwazo na kuogelea kuvuka.

"Kwa muktadha wetu wa kipekee, kuna hitaji muhimu la kutambua ushiriki wa wanawake katika shughuli zote za kiuchumi kutoka kwenye kilimo hadi kilimo cha bustani, katika kushughulikia viwanda vyetu vya chakula, ambapo kwa kiasi kikubwa wamechukua jukumu lisilokuwa maarufu na nyuma ya pazia," anasema.

"Maiden Kashmir kwa sasa inashirikiana na maduka makubwa makubwa huko Srinagar, Kashmir na kuchukua oda za mtandaoni kupitia tovuti yao pamoja na mtandao wa Instagram.


greaterkashmir_2022-05_904a9dc2-44bf-4141-b86e-ada666f90dbf_33.jpg
 
Back
Top Bottom