Wachangiaji wengi wa huu uzi hawamjui vizuri kunguru. Katika ndege ambao ni nadra sana kumuona akiwa kafa,mmojapo ni kunguru. Huwa mwerevu sna hivyo hata kufa kwake ni nadra. Hivyo, ule udogo wa mwili na sura yake mbovu vilimfanya mwanadamu asihangaike naye hivyo kifo kwake ni nadra.
Hili ni swali napenda tu kujua tafiti zinasemaje kuhusu ulaji wa nyama ya ndege huyu.
Amekuwa kero kila kona na walio wengi wanajua kero zake sasa sitaki kuzungumzia hilo ila napenda kujua kwa yeyote anayejua kama ulaji wa nyama yake una madhara yoyoye kiafya.
Ikiwa ina madhara kiafya basi tuendelee tu kuikabili adhaa ya ndege huyu, ila kama hana madhara basi tujuzwe tujifarij na nyama yake. Ni hayo tu
Panya tena!!!! Ngoja wenyew wakusikie.
Naokuomba tu usimwite nguruwe ati ni Scavenger. Huwezi mfananisha nguruwe na kunguru. Hivi unafahamu maana ya huyo Scavenger?? Kunguru, fisi, mbwa mwitu, tai... sasa nguruwe katoka wapi kwenye kundi hilo?? Ka huli acha wenzio wafurahie milo yao.Kunguru anachukiwa kwa sababu ni ndege jamii ya "scavengers" kwa wanyama jamii ya scavengers ni fisi na Nguruwe, scavengers ni wanyama wanaokula takataka, kama nguruwe analiwa vipi Kunguru asiliwe???, ni utafiti tu unaotakiwa kufanywa.
Kunguru ni ndege mzuri sana ukikaa naye karibu.Anafanya vitu vingi ukivifuatilia vinafurahisha.Sina muda wa kuelezea lakini nitaelezea baadaye
Nimekukubali sana. Wee ni msomi na hupendi uvivu. Umeandika insha mpaka hitimishoMkuu wewe unataka nani akujuze wakati wewe mwenyewe unaweza kufanya utafiti kujua kwamba nyama yake inafaa kwa matumizi ya Binadamu.
Fanya hivi; kamata Kunguru, chinja, muandae kwa kumnyonyoa jinsi vile kuku anavyoandaliwa na kisha mpe mbwa au paka, hao wanyama wakila basi hiyo itakuwa ni hatua ya kwanza, hakafu endelea hivyo kwa kama wiki 2-3 kukamata kunguru na kuwapa hao wanyama, baada ya muda huo angalia maendeleo ya kiafya ya hao wanyamaa,kama wanapenda sana kula hiyo nyama na hakuna madhara basi hiyo ni hatua kubwa sana.
Hatua ya pili ni kukamata kunguru na kuwaandaa halafu kupika nyama yao na kuwapatia tena hao wanyama na ufanye hivyo kwa muda fulani hadi utakaporidhika kwamba hakuna madhara yaliyojitokeza kwao.
Hatua inayofuata ndiyo hatua kubwa na ngumu sana, kamata kunguru, chinja, muandae na chukua nyama ya kidari ikaange na bizari na pilipili kichaa, ndimu na chumvi nk, basi hapo unaweza kula wewe mwenyewe kiduchu huku ukisikilizia kwa mbali kama kwamba unaonja sumu, kama ladha yake itakuwa muruwa basi kesho tena endelea kufanya hivyo kidogo kidogo hatimaye unaweza kujigundua kama kuna au hakuna madhara yoyote mwilini mwako-- hatua hiyo ndiyo itakuwa mwisho wa utafiti wako kwamba KUNGURU NI MBOGA AU SIYO MBOGA.
Ni katika kujitoa kwa aina hiyo ndipo watu tumeweza kujua kwamba kumbe hata mende, Panya,dagaa, samaki,nk ni vyakula bora kwa Binadamu.
Basi mkuu wakati ndiyo huu wa kufanya hilo jaribio.
Ungetangaza tuu ulaji wa nyama ya kunguru ni suluhisho la wenye tatizo la nguvu za kiume. Mbona hao kunguru wangepotea hadi wengine wangetunzwa kwenye jumba la makumbusho
Ukishaona kitu hakiliwi na mchina au mmakonde...usijaribu kula
Ungetangaza tuu ulaji wa nyama ya kunguru ni suluhisho la wenye tatizo la nguvu za kiume. Mbona hao kunguru wangepotea hadi wengine wangetunzwa kwenye jumba la makumbusho