Tafakuri yangu wakati tunalalamika viburi vya watawala

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,509
2,000
Wakati tunalalamikia viburi vya watawala, naomba niwakumbushe ukweli huu:

Mwenyezi Mungu alietuumba, hakumpa mtu mmoja kila kitu kwani alijua hatari ya kufanya hivyo. Lakini sisi wanadamu, kwa udhaifu wetu, tumewapa watu/watawala mamlaka ya kuamua na kutenda karibu kila jambo linalotuhusu kinyume kabisa na mpango wa Mungu. Halafu bila kujua kosa letu la msingi, kila siku tunalalamika wanapojawa na viburi kumbe sisi wenyewe ndio chanzo.

Hivyo, kwakuwa katiba yenyewe teyari ni kinyume kabisa na mpango wa mwenyezi Mungu, kuapa kwa kutumia katiba ya aina hii ni kiapo batili mbele za Mungu tangu siku ya kwanza na haya ndio matokeo yake.

Mwenyezi Mungu ametupa akili hawezi kutufunulia kila jambo bali yatupasa kutumia akili na maarifa aliyotupa kuishi atakavyo tofauti na hapo lazima tuumie.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom