Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Sasa ni dhahiri kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameshtakiwa kwa makosa ya jinai. Amefikishwa Mahakamani huko Arusha na kusomewa mashtaka sita. Ninaandika hapa nikiamini kuwa mashtaka ya Ole Sabaya bado ni tuhuma tu hadi pale yatakapothibitishwa mahakamani kupitia ushahidi. Yaani, ukweli au la kuhusu mashtaka yake utapatikana mahakamani. Sitarajii tena Mkurugenzi wa Mashtaka kuwasilisha Hati ya Kutokuwa na Nia ya Kushtaki kama alivyofanya kwenye kesi ya Sabaya iliyopita (natania).
Kimsingi, makosa katika mashtaka yote dhidi ya Sabaya yanadaiwa kufanywa naye wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Hapa ndipo tafakari yangu inapoanzia. Bila hata ufahamu wa kisheria, inafahamika kuwa Mkuu wa Wilaya pamoja na mambo mengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya yake. Ndiyo kusema, Mkuu wa Wilaya ndiye mlinzi kiongozi wa amani na utulivu katika Wilaya yake. Ndiye anayepaswa kuhakikisha kuwa wananchi wa Wilaya yake wanaishi kwa amani huku wakifanya shughuli zao za kimaendeleo katika kujitafutia mikate yao ya kila siku.
Haitarajiwi kuona Mkuu wa Wilaya 'akiwa kinara' wa uharibifu wa amani, utulivu na ustawi wa watu wake. Haitarajiwi pia kuona Mkuu wa Wilaya kutenda makosa ya jinai ambaye yeye mwenyewe ndiye anapambana nayo usiku na mchana ili wananchi wake wawe na amani, utulivu na ustawi. Haitarajiwi pia Mkuu wa Wilaya kutenda uhalifu ikizingatiwa pia yeye ni mwakilishi wa Rais katika Wilaya yake. Matendo yake na maneno yake yanawakilisha maono, maelekezo na taswira ya mamlaka yake ya uteuzi. HAIPENDEZI Mamlaka ya uteuzi kubeba taswira ya kijinai kwa wananchi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya.
NI PICHA YA KUOGOFYA kuona Mkuu wa Wilaya akipokea rushwa; akitakatisha pesa; akiongoza genge la kihalifu na kadhalika. NI MAMBO YA KUTISHA kusikia au kushuhudia Mkuu wa Wilaya akikandamiza ustawi wa watu wake na kulinda kwa nguvu zake zote 'genge' lake. Tuhuma dhidi ya Sabaya zinatoa picha ya kujisahau au kujiachia kulikopitiliza kwa wateule. Au tuhuma hizo zinaonyesha jinsi tabia halisi ya mteule inapojianika pale ambapo kunapatikana nafasi ya kufanya chochote mahali popote. Mashtaka yote ni ya Arusha, bado ya mahali pengine ikiwemo Wilaya yake ya Hai. Inafikirisha sana.
Mashtaka ya Sabaya yawe funzo kwa Mamlaka ya Uteuzi. Yawe funzo katika vya kuzingatia kabla, wakati na baada ya uteuzi. Mamlaka ya uteuzi ina mikono mirefu. Ina vyombo mbalimbali vya kiuchunguzi na kiutafiti. Inafurahisha na kuleta imani na amani kwa wananchi kuona Mamlaka ya Uteuzi ikifanya kazi kubwa kuchuja wateule wake ili 'makandokando' kama ya Ole Sabaya yaepukwe. Hata kama mashtaka yote hayatathibitishwa mahakamani, kutuhumiwa tu kama kiongozi inatosha kuchafua picha ya mteule yeyote yule awaye. Kila jambo hutokea ili kutoa mafundisho kwa yajayo.