Tafakuri yangu kwa Mashtaka ya Ole Sabaya

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,693
2,000
Sasa ni dhahiri kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameshtakiwa kwa makosa ya jinai. Amefikishwa Mahakamani huko Arusha na kusomewa mashtaka sita. Ninaandika hapa nikiamini kuwa mashtaka ya Ole Sabaya bado ni tuhuma tu hadi pale yatakapothibitishwa mahakamani kupitia ushahidi. Yaani, ukweli au la kuhusu mashtaka yake utapatikana mahakamani. Sitarajii tena Mkurugenzi wa Mashtaka kuwasilisha Hati ya Kutokuwa na Nia ya Kushtaki kama alivyofanya kwenye kesi ya Sabaya iliyopita (natania).

Kimsingi, makosa katika mashtaka yote dhidi ya Sabaya yanadaiwa kufanywa naye wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Hapa ndipo tafakari yangu inapoanzia. Bila hata ufahamu wa kisheria, inafahamika kuwa Mkuu wa Wilaya pamoja na mambo mengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya yake. Ndiyo kusema, Mkuu wa Wilaya ndiye mlinzi kiongozi wa amani na utulivu katika Wilaya yake. Ndiye anayepaswa kuhakikisha kuwa wananchi wa Wilaya yake wanaishi kwa amani huku wakifanya shughuli zao za kimaendeleo katika kujitafutia mikate yao ya kila siku.

Haitarajiwi kuona Mkuu wa Wilaya 'akiwa kinara' wa uharibifu wa amani, utulivu na ustawi wa watu wake. Haitarajiwi pia kuona Mkuu wa Wilaya kutenda makosa ya jinai ambaye yeye mwenyewe ndiye anapambana nayo usiku na mchana ili wananchi wake wawe na amani, utulivu na ustawi. Haitarajiwi pia Mkuu wa Wilaya kutenda uhalifu ikizingatiwa pia yeye ni mwakilishi wa Rais katika Wilaya yake. Matendo yake na maneno yake yanawakilisha maono, maelekezo na taswira ya mamlaka yake ya uteuzi. HAIPENDEZI Mamlaka ya uteuzi kubeba taswira ya kijinai kwa wananchi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya.

NI PICHA YA KUOGOFYA kuona Mkuu wa Wilaya akipokea rushwa; akitakatisha pesa; akiongoza genge la kihalifu na kadhalika. NI MAMBO YA KUTISHA kusikia au kushuhudia Mkuu wa Wilaya akikandamiza ustawi wa watu wake na kulinda kwa nguvu zake zote 'genge' lake. Tuhuma dhidi ya Sabaya zinatoa picha ya kujisahau au kujiachia kulikopitiliza kwa wateule. Au tuhuma hizo zinaonyesha jinsi tabia halisi ya mteule inapojianika pale ambapo kunapatikana nafasi ya kufanya chochote mahali popote. Mashtaka yote ni ya Arusha, bado ya mahali pengine ikiwemo Wilaya yake ya Hai. Inafikirisha sana.

Mashtaka ya Sabaya yawe funzo kwa Mamlaka ya Uteuzi. Yawe funzo katika vya kuzingatia kabla, wakati na baada ya uteuzi. Mamlaka ya uteuzi ina mikono mirefu. Ina vyombo mbalimbali vya kiuchunguzi na kiutafiti. Inafurahisha na kuleta imani na amani kwa wananchi kuona Mamlaka ya Uteuzi ikifanya kazi kubwa kuchuja wateule wake ili 'makandokando' kama ya Ole Sabaya yaepukwe. Hata kama mashtaka yote hayatathibitishwa mahakamani, kutuhumiwa tu kama kiongozi inatosha kuchafua picha ya mteule yeyote yule awaye. Kila jambo hutokea ili kutoa mafundisho kwa yajayo.
 
Litro

Senior Member
Nov 18, 2018
160
500
Najiuliza is he married? Kama ndio basi mwanamke alishindwa kufit in kwenye nafasi ya usaidizi mpk mume kufika hapo alpofika. Had it been me ningemuona nashauri anazid kukaza shingo ningempigia goti la saa tisa usiku atumbuliwe mapeema tuishi kwa kidogo kitu ila kwa amani
 
mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,430
2,000
Aliyokuwa anafanya sabaya yanaakisi aliyokuwa anafanya bosi wake aliyemteua.
Mungu akasikia kilio cha watesi hao na kwa kuwa kulikuwa hakuna mamlaka ya kumtumbua jiwe (bunge lilikuwa linamuogopa) Mungu baba mwenyewe akaona heri amtumbue mwenyewe
Ukweli ni kwamba Magufuli alikuwa katili kama huyo sabaya
 
MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,727
2,000
Sasa ni dhahiri kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameshtakiwa kwa makosa ya jinai. Amefikishwa Mahakamani huko Arusha na kusomewa mashtaka sita. Ninaandika hapa nikiamini kuwa mashtaka ya Ole Sabaya bado ni tuhuma tu hadi pale yatakapothibitishwa mahakamani kupitia ushahidi. Yaani, ukweli au la kuhusu mashtaka yake utapatikana mahakamani. Sitarajii tena Mkurugenzi wa Mashtaka kuwasilisha Hati ya Kutokuwa na Nia ya Kushtaki kama alivyofanya kwenye kesi ya Sabaya iliyopita (natania).

Kimsingi, makosa katika mashtaka yote dhidi ya Sabaya yanadaiwa kufanywa naye wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai. Hapa ndipo tafakari yangu inapoanzia. Bila hata ufahamu wa kisheria, inafahamika kuwa Mkuu wa Wilaya pamoja na mambo mwngine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya yake. Ndiyo kusema, Mkuu wa Wilaya ndiye mlinzi kiongozi wa amani na utulivu katika Wilaya yake. Ndiye anayepaswa kuhakikisha kuwa wananchi wa Wilaya yake wanaishi kwa amani huku wakifanya shughuli zao za kimaendeleo katika kujitafutia mikate yao ya kila siku.

Haitarajiwi kuona Mkuu wa Wilaya 'akiwa kinara' wa uharibifu wa amani, utulivu na ustawi wa watu wake. Haitarajiwi pia kuona Mkuu wa Wilaya kutenda makosa ya jinai ambaye yeye mwenyewe ndiye anapambana nayo usiku na mchana ili wananchi wake wawe na amani, utulivu na ustawi. Haitarajiwi pia Mkuu wa Wilaya kutenda uhalifu ikizingatiwa pia yeye ni mwakilishi wa Rais katika Wilaya yake. Matendo yake na maneno yake yanawakilisha maono, maelekezo na taswira ya mamlaka yake ya uteuzi. HAIPENDEZI Mamlaka ya uteuzi kubeba taswira ya kijinai kwa wananchi kupitia kwa Mkuu wa Wilaya.

NI PICHA YA KUOGOFYA kuona Mkuu wa Wilaya akipokea rushwa; akitakatisha pesa; akiongoza genge la kihalifu na kadhalika. NI MAMBO YA KUTISHA kusikia au kushuhudia Mkuu wa Wilaya akikandamiza ustawi wa watu wake na kulinda kwa nguvu zake zote 'genge' lake. Tuhuma dhidi ya Sabaya zinatoa picha ya kujisahau au kujiachia kulikopitiliza kwa wateule. Au tuhuma hizo zinaonyesha jinsi tabia halisi ya mteule inapojianika pale ambapo kunapatikana nafasi ya kufanya chochote mahali popote. Mashtaka yote ni ya Arusha, bado ya mahali pengine ikiwemo Wilaya yake ya Hai. Inafikirisha sana.

Mashtaka ya Sabaya yawe funzo kwa Mamlaka ya Uteuzi. Yawe funzo katika vya kuzingatia kabla, wakati na baada ya uteuzi. Mamlaka ya uteuzi ina mikono mirefu. Ina vyombo mbalimbali vya kiuchunguzi na kiutafiti. Inafurahisha na kuleta imani na amani kwa wananchi kuona Mamlaka ya Uteuzi ikifanya kazi kubwa kuchuja wateule wake ili 'makandokando' kama ya Ole Sabaya yaepukwe. Hata kama mashtaka yote hayatathibitishwa mahakamani, kutuhumiwa tu kama kiongozi inatosha kuchafua picha ya mteule yeyote yule awaye. Kila jambo hutokea ili kutoa mafundisho kwa yajayo.
Kwangu hakuna kesi hapo.Sabaya atakapoanza kutoa voice clips akiongea na mtu mkubwa,atakapotoa slip za transcation ya baadhi ya pesa zilpokwenda hapo utasikia "kwa sababu za kiusalama hakuna wasikilizji katika kesi hii,ni chamber court".Haiwezekani yote yatokee RC ASIJUE,RSO ASIJUE,DGTISS ASIJUE,MAMLAKA YA UTEUZI ISIJUE,never!!
 
The Icebreaker

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
8,042
2,000
Siku hizi kila mtu ni mtaalamu wa kila kitu,kila mtu ni mshauri mzuri wa kila mtu,kila mtu ni mtafiti na ni mchambuzi wa masuala yote,kila mtu anajua majukumu ya mwenzake jinsi yanavyo paswa kutimizwa...

Unacho hitaji ni kua na smart phone,bando na kua na uwezo wa kuingia kwenye mitandao ya kijamii tu.

:D :D :D :D
 
Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,693
2,000
Siku hizi kila mtu ni mtaalamu wa kila kitu,kila mtu ni mshauri mzuri wa kila mtu,kila mtu ni mtafiti na ni mchambuzi wa masuala yote,kila mtu anajua majukumu ya mwenzake jinsi yanavyo paswa kutimizwa...

Unacho hitaji ni kua na smart phone,bando na kua na uwezo wa kuingia kwenye mitandao ya kijamii tu.

:D :D :D :D
Hakika. Nami ni mmoja wao...
 
Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,798
2,000
Siku hizi kila mtu ni mtaalamu wa kila kitu,kila mtu ni mshauri mzuri wa kila mtu,kila mtu ni mtafiti na ni mchambuzi wa masuala yote,kila mtu anajua majukumu ya mwenzake jinsi yanavyo paswa kutimizwa...

Unacho hitaji ni kua na smart phone,bando na kua na uwezo wa kuingia kwenye mitandao ya kijamii tu.

:D :D :D :D
Mkuu, unamfahamu vizuri mleta UZI!? Ni wakili mwandamizi wa mahakama kuu na mahakama ya rufaa so unachangia uzi wa proffesinal au expert wa sheria za bongo. Msome kwenye nyuzi zingine
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom