GE2025 Tafakuri ya Askofu Bagonza kwa yanayoendelea CHADEMA, CCM na Tume huru ya Uchaguzi Tanzania

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Askofu Bagonza ameandika tafakuri hii:

FIKIRI MPAKA UTOKE JASHO: Usihukumu na Usibariki.

1. Ukiona makatibu wenezi wa Upinzani wanapita nyumba kwa nyumba kukusanya kadi za wapiga kura na namba za NIDA wakati chama tawala kiko kimya ujue wapinzani wanataka kupiga kura kabla ya siku ya kupiga kura. Penye wapinzani weka CCM na maana itabaki ile ile.

2. Ukiikosoa Tume “Huru” ya Uchaguzi (INEC), ukanuniwa na CHADEMA, basi una haki ya kuamini makosa ya INEC yanaagizwa na CHADEMA. Penye neno CHADEMA, waweza kuweka CCM.

3. Ukivikosoa vyombo vya dola kwa kuipendelea CHADEMA na kuionea CCM, kisha ukaona CHADEMA ndiyo inayojibu tuhuma hizo, ujue kasoro za vyombo vya dola zinaagizwa na CHADEMA. Penye jina CHADEMA, waweza kuweka CCM.

4. Ukiona wagombea wengi wa CCM wameenguliwa, wakati wagombea wote wa Upinzani wameteuliwa, una haki ya kuamini kuwa fomu zote za wagombea wa Upinzani ZILIJAZWA na Tume ya Uchaguzi (INEC). Penye neno Upinzani waweza kuweka CCM.

5. Ukiona wagombea wengi wa Upinzani wamepitishwa bila kupingwa na bado wanaendelea na jitihada za kushawishi wagombea wa CCM wajitoe, huku wakiorodhesha na kununua shahada za kupigia kura, una haki ya kuamini kuwa Wapinzani hawana Imani na sanduku la kura. Penye neno Wapinzani waweza kuweka CCM bila kupoteza maana ya taarifa hii.

6. Wapinzani wanapenda Sana Amani. CCM wanapenda Sana Haki. Siku Wapinzani wakipenda Haki na CCM wakapenda Amani ndipo tutapata Tume HURU ya Uchaguzi. Penye neno Wapinzani unaweza kubadili na kuweka CCM bila kupoteza maana ya fungu hili.

7. Viongozi wa dini matapeli ndio wanahubiri haki tu. Viongozi wa kweli wanahubiri amani tu. Penye neno “matapeli” unaweza kuweka “wa kweli” na penye neno “wa kweli” ukaweka “matapeli” ukapata maana halisi ya fungu hili.

TURUDI MEZANI
TUMBO LA KUHARA LINATIBIKA

1757834156521.png
 
Kwa sababu zile zile mgombea wa ACT tarime anaenguliwa lakini kwa sababu hizo hizo mgombea wake wa Urais anapokelewa na tume hiyo hiyo, anapewa fomu, VX na ulinzi. Askofu Bagonza atatafakari mpaka achoke.
 
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Askofu Bagonza ameandika tafakuri hii:

FIKIRI MPAKA UTOKE JASHO: Usihukumu na Usibariki.
1. Ukiona makatibu wenezi wa Upinzani wanapita nyumba kwa nyumba kukusanya kadi za wapiga kura na namba za NIDA wakati chama tawala kiko kimya ujue wapinzani wanataka kupiga kura kabla ya siku ya kupiga kura. Penye wapinzani weka CCM na maana itabaki ile ile.
2. Ukiikosoa Tume “Huru” ya Uchaguzi (INEC), ukanuniwa na CHADEMA, basi una haki ya kuamini makosa ya INEC yanaagizwa na CHADEMA. Penye neno CHADEMA, waweza kuweka CCM.
3. Ukivikosoa vyombo vya dola kwa kuipendelea CHADEMA na kuionea CCM, kisha ukaona CHADEMA ndiyo inayojibu tuhuma hizo, ujue kasoro za vyombo vya dola zinaagizwa na CHADEMA. Penye jina CHADEMA, waweza kuweka CCM.
4. Ukiona wagombea wengi wa CCM wameenguliwa, wakati wagombea wote wa Upinzani wameteuliwa, una haki ya kuamini kuwa fomu zote za wagombea wa Upinzani ZILIJAZWA na Tume ya Uchaguzi (INEC). Penye neno Upinzani waweza kuweka CCM.
5. Ukiona wagombea wengi wa Upinzani wamepitishwa bila kupingwa na bado wanaendelea na jitihada za kushawishi wagombea wa CCM wajitoe, huku wakiorodhesha na kununua shahada za kupigia kura, una haki ya kuamini kuwa Wapinzani hawana Imani na sanduku la kura. Penye neno Wapinzani waweza kuweka CCM bila kupoteza maana ya taarifa hii.
6. Wapinzani wanapenda Sana Amani. CCM wanapenda Sana Haki. Siku Wapinzani wakipenda Haki na CCM wakapenda Amani ndipo tutapata Tume HURU ya Uchaguzi. Penye neno Wapinzani unaweza kubadili na kuweka CCM bila kupoteza maana ya fungu hili.
7. Viongozi wa dini matapeli ndio wanahubiri haki tu. Viongozi wa kweli wanahubiri amani tu. Penye neno “matapeli” unaweza kuweka “wa kweli” na penye neno “wa kweli” ukaweka “matapeli” ukapata maana halisi ya fungu hili.
TURUDI MEZANI
TUMBO LA KUHARA LINATIBIKA

Hahahaha fasihi imeeleweka kikamilifu!!! Hiii imeenda!
 
Hao wakutafakari hadi jasho litoke hawajazaliwa, siku watakapozaliwa ndio nchi itakuwa imekombolewa rasmi
 
Back
Top Bottom