Tafakuri chokonozi: Ni dengu, dengi, au ni propaganda?!

Tafakuri chokonozi: Ni dengu, dengi, au ni propaganda?!

Kuna haka ka ugonjwa ambako huenda kanakuja kufunika maswala mazito kwenye huu mchakato wa katiba na maswala mazito ya muungano tuliyokuwa nayo sasa, naanza kupata wasiwasi maana watawala wanawajua vizuri watanzania kuwa ni watu wanaobebwa na matukio. Likija tukio fulani na likapambwa kwa mapambo ya aina ya kuwatoa watu kwenye mstari basi watu wanahama.

Kama mnakumbuka baada ya serikali kubanwa kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na watu kuwa tayari kuingia barabarani kipindi kile ambacho pia kulikuwa na maandamano ya kuondoa utawala ulioshindwa kuleta tija kwenye nchi za uarabuni,ghafla likaja zengwe la kikombe cha babu wa Loliondo.

Kwenye kikombe cha babu wa Loliondo viongozi wa serikali wakawa wa kwanza kwenda kupata kikombe, inasemekana alianza MSAFIRI, akaja mtoto wa mkulima aliye pinda mgongo, orodha ndefu ikafuata, kibaya zaidi serikali ikaruhusu mpaka wagonjwa waliokuwa mahospitalini eti watoke na kwenda kwenye kikombe, baada ya hapo vikafuata vifo na adha zilizotokana na msusuru wa watu kule Loliondo.

Likapita la kikombe cha Loliondo watu wakawa wamehama kwenye kufikiria kupanda kwa gharama za maisha na uhaba wa umeme. Akili zikahamia Loliondo, Kila unaye mgusa, mwenye sukari, mwenye utamu, mwenye mafua, aliye jikwaa kidole wote wimbo wao ulikuwa mmoja "Loliondo" Kwa hili serikali ikapata ahueni, ikajipanga, ikafanikiwa kuwapumbaza watanzania, waliokufa wengine wakatupwa vichakani. Maisha yakaendelea watawala wagongena mvinyo..


Siku hazikuganda, Umekuja mchakato wa katiba, ukweli uliokuwa unafichwa umeanza kudhihiri, nondo zimeanza kushushwa, wasiotaka ukweli ujulikane wameanza propaganda za kufa mtu! Hawataki ukweli ujulikane, wanataka tuzidi kukaa kwenye nusu karne ya uwongo! Ghafla eti tunasikia Dengua, wengine wanaita Dengi, wengine Dengu, wengeni Dengelua yaani ngonjwa moja hata wataalamu wetu kila mtu anatamka anavyotaka yeye!


Wasiwasi wangu eti gonjwa hili limeanza na wasanii maarufu! Limeanza na Ray C akapata coverage front page kwenye magazeti, akaja Dr Cheni naye hivyohivyo! Halafu eti tunaambiwa umeua mpaka Daktari, na wanatajwa wagonjwa wengine kadhaa, wanasahau kuwa kwa tanzania ugonjwa hatari ni Maralia na vifo vya kina mama wajawazito, kila dakika 10 maralia huua si chini ya watu 5, na kila dakika 5 kuna si chini ya mama mjamzito mmoja anaye poteza maisha.Sio hili DENGE, Sijui DENGUA, SIjui DENGI, sijui DENGELUA.

Wanataka kututoa kwenye agenda muhimu hawa! Hii ni propaganda! Baada ya hapa utasikia mikusanyiko hairuhusiwi, Lakini hawatasema kuwa hata kwenye dalaladala na boti kuna mikusanyiko! Kuna watu wanalengwa kunyamazishwa hapa.

AKILI KUMKICHWA poleni watanzania wenzangu sijui kwa gonjwa gani vile?!... Ni Dengi, Dengu, Dengua au Dengelua?! Sikatai kuwa lipo, napata wasiwasi na gonjwa hili linavyopewa promo kana kwamba limekuwa tishio kuliko Maralia na vifo vya kina mama wajawazito.

Ulianza vizuri sana ila mwishono ulivyomalizia, umenisikitisha sana. Sasa sikiliza ndg yangu: inaonesha huamini kuwepo kwa huu ugonjwa na pili hata kama upo unaamini siyo tishio ukilinganisha na Malaria japo unatamka maralia. Kwa taarifa yako huu ugonjwa ndg yangu upo na ni HATARI kuliko hiyo Malaria unayotupa hizo takwimu sijui za mwaka gani. Na malaria kwa sasa siyo tishio kubwa kama unavyofikiria. Kwa ushahidi fuatilia ripoti ya TMHS au TDHS utaona. Mimi nimeumwa na hii Dengue na nimeponea tundu la sindano kakaangu. Hapa nilipo bado na recover, cjapona kwa 100%. Ni ugonjwa hatari sana, usiokuwa na tiba maalum wala chanjo. Ni viral disease, kwa wale wanaojua viral diseases are very severe na mara nyingi hazina treatment. Omba sana Mungu usikupate. Ukiugua maumivu yake hayasikii anti-pain kabisa. Daktari na wauguzi kupoteza maisha ilhali wapo ktk matibabu si kitu mchezo hata mara moja. Hivyo tambua kaka kuwa Dengue ipo na ni hatari kuliko malaria, mimi ni mtu a hospitali najua,
 
duh jamaa nadhani siasa inakuaribu....huu ugonjwa upo kweli na si propaganda km unavyosema...huyu dr wa temeke aliyefariki ni ndugu wa karibu kabisa wa rafiki yangu....si propaganda hata kidogo....labda ukikupata ndo utaelewa....kweli sisi watanzania ni wagumu sana kuelewa aisee

Si vizuri kumwombea mtu ugonjwa, ila huyu jamaa kuna haja angeupata ili aamini, na wengine wa sampuli kama yake. Maana inaonesha maisha yao yametekwa na siasa kiasi kwamba hata ktk issue serious kama hizi wanajua ni siasa! Hii hatari sana tukiendekeza siasa
 
Kweli kabisa Mohamed Mtoi maana nilitegemea hadi leo TBC ingekuwa imejikita kuelezea. Kuna watu jana mikoani hawajui na Dar pia hasa tiba. Dhaifu na legelege hii.
 
Na kwa kudhihirisha udogo wa hizo IQ, wewe ni mmoja wa watu hao tena ukiwa unaongoza kundi hili. Watu wanakufa kwa ugonjwa huu wewe unaona wanaigiza!!! Kweli IQ yako inatisha kama katika kila kinachotokea wewe unawaza kuwa ni propaganda za kisiasa tu. Watanzania wanakufa wewe unasema mnalala na mbu! are you serious!!! Ndg yangu tenganisha mambo ya siasa na facts, siyo kila kitu politics.
Nilipoona ile ripoti inayoonyesha Tanzania ni moja ya nchi kumi zenye IQ ndogo kabisa duniani, nilidhani ni hila tu za magharibi,

Lakini nilijifunza kuwa Kiongozi wa nchi ndiye hubeba taswira na aina ya watu wa taifa analoliongoza, Ikiwa taifa litampata kiongozi mpole basi nje ya taifa lake ataakisi upole wa watu wake,

Wakati ulaghai wa kikombe cha Ambilikile Mwaisapile kinaibuka, taifa lilikuwa kwenye mtafaruku wa kisiasa hasa madai ya katiba mpya na ufisadi mkubwa uliokuwa umeligubika genge la ccm na serikali yake, Kweli harambee ya serikali ilifanikiwa kuhamisha akili za Watz wote wakaelekea Loliondo isipokuwa mimi na wenzangu wachache tunaoona kwa jicho la tatu.

Leo ccm imebandwa na umma juu ya aina ya muungano wautakao, Umma unataka muungano wa serikali tatu, ccm na genge lake hawataki, wanataka taifa liendelee kutopea kwenye mauaji ya nashehe na mapadre pale Zanzibar, wanataka mfumo wa serikali mbili ulioshindwa kutatua matatizo ya muungano kwa miaka 50,

Na zaidi ccm na genge lake wameiba 200b katika akaubti maalumu ya Tanesco iliyopo BOT, hili ni tukio la wizi mkubwa zaidi kuliko ule wa EPA,

Lakini katika mkakati uleule wa kuzima kelele za umma, wameibuka na mzimu unaoitwa Dengue, unaotajwa kuwa ni ugongwa unaoambukizwa na mbu kwa lugha ya kikwetu ni 'suguni".

Haya ni maajabu ya tz, mbu huyu aibuke kuleta ugonjwa huo katika kipibdi hiki cha vuguvugu la ccm kukosa udhibiti wa nchi???

Mbu huyu mimi nimezaliwa kijijini kwetu namuoba, nimeishi nchi zenye baridi kali kama Urusi kwa miaka zaidi ya kumi nimemuona hasa kwenye mifugo aina ya kondoo wa sufi kule Kivey,

Nimeidmshi Uchina kwa miaka kadhaa mbu huyu yupo, na nimeng'atwa hasaa mitaa ya Suki, sijawahi kuona mtu kaugua na kuwa ni ni ugonjwa tishio kama propaganda ya ccm inavyotaka tuamini,

Nyumbani kwangu Mbutu Kiganboni hawa mbu ndio tunashinda nao na kulala nao kila kuchapo tangu na tangu,

Najiuliza hawa umbu wenye ugonjwa huo wametoka hapa wizara ya afya mtaa wa samora na shabani robert?

Inasemwa na inaaminika kuwa Watz ni wajinga na mazezeta kuliko nchi yoyote duniani, hili linajidhihirisha kuona tunatungiwa uongo eti kuna DENGUA, halafu 200b zinaibiwa, na kujaribu kuzima madai ya katiba ya umma inayotaka muungano wa Serikali tatu.
 
Yericko Nyerere na mwenzako Mohamedi Mtoi nendeni mkatubu kwa MUNGU wenu Kanisani na Msikitini....nje ya hapo nawaombea muugue huu ugonjwa tena ikiwezekana mlazwe hadi ICU ila msife...mkinusurika mje hapa JF kutoa ushuhuda. Poor you CHADEMA people mnakidharilisha chama.
 
MKUU kipi kinachokufadhaisha ukweli kwako ni mchungu sana?

hakuna kisichowezekana najua wengi mnasoma.kwa juu juu nakushindwa kufahama kipi has a hapa ni chaajabu.
kufa kwa watu sio sababu ya msingi yakutufanya tuamini kuwa huu Egonjwa kweli nitishio .
swali iweje huu ugonjwa ushike kasi saa hizi has a ukishikiwa kidedea na media??

hata mwanao anaweza kufa Leo Hi na maleria nakwakuwa ushaaminishwa nakupandikizwa kitu kichwani mwako juu ya dungua basi ni shida.

harafu walivyokuwa wauwaji wanatwambia hauna Tiba na ukiumwa usinywe dawa hivi wanajamvi hii inawaingia akilini kweli??

h

Kinachonifadhaisha ni kwamba baadhi ya watu wanaplay down umuhimu wa huu ugonjwa na kuaminisha wengine kuwa ni suala la kutengeneza. Magonjwa ya milipuko yamekuwepo Tanzania mara kadhaa bila kujali kama ni ugonjwa mpya au wa zamani.
Kwa hiyo tukubaliane kabisa kwamba mlipuko wa dengue dar sio fiction. Ni kitu kimetokea na watu wanaumwa na wanauguliwa. Watu wanakufa na wanafiwa.
Sasa kama kuna watu wanataka kutumia hili tatizo kudivert attention ya jambo jingine, that's another story. Lakini ni uhalisia kwamba huu mlipuko wa ugonjwa unahitaji kuchukuliwa na kashughulikiwa kwa udharura zaidi ya tunaouona sasa...
 
Kwa wale wapenda elimu, hebu tupime ukweli

Binafsi sihusianishi kabisa dengue na sababu za kisiasa.
Hii ni tabia ya watanzania kushadadia vitu bila hata kujua ukweli matokeo yake ni kujenga hofu hata zisizokuwepo.
Leo mtu akiibuka akasema kitu watu wengi hata wasomi hawajiulizi vizuri.
Hii dengue fever madaktari (MD) wanaielewa vizuri, kwa sababu si utamaduni wao kuwaeleza ukweli wagonjwa kuhusu magonjwa yao basi mtu akiambiwa dengue anafikiri dude gani sijui. (Au vile halina kiswahili chake)

Dengue ni ugonjwa upo muda mrefu sema hospitali zetu kawaida hazina vipimo vya kupimia tukathibitisha, hivyo vipimo sijui vimeletwa lini. Hata hivyo kwa kiasi kikubwa unashabihiana na magonjwa mengi ambayo yanasababisha homa na maumivu ya kichwa. Hata ukigoogle utakutana na magonjwa karibu ya mia. Madaktari huwa wanafikiria yale yanayoweza kusababisha homa hizo kutokana na eneo, majira, mfumuko na ufananio wa dalili. Sasa kama ambavyo kila siku watu huwa wakisikia ka uchovu tu wakanywa dawa za malaria ndo imekuwa hivyo kwa dengue, na uhakika wengine ni hofu tu kama huyu aliyelipia 50000 kipimo.

Dengue hadi iwe mbaya sana ndo shida kubwa. Kawaida ugonjwa wake ni kama homa ya mafua tu, ndani ya siku 3-14 hivi au kama matetekuwanga, inaisha yenyewe. Ni chini ya asilimia 3 ambao huwa mbaya na chini ya asilimia moja hufa. Kwa takwimu za CDC, watu 22 kati ya laki moja ya walioambukizwa hufa kila mwaka duniani, na sana sana watoto. Wakati huo kwa takwimu za CDC Malaria huua watu 301 kati ya laki moja ya waliombukizwa kila mwaka, hapa asilimia 90 kusini wa jangwa la sahara.
Mlipuko baada ya mafuriko ya eneo unaweza kutokea ila si hatari (kulingana na mafuriko) kama kipindupindu na mlipuko wa malaria. Dengue inawezekana kutokeza mapema kwa sababu yenyewe inawahi kuonesha dalili ukilinganisha na malaria (kama mbu wameongezeka),

Ushauri kwa watu wa dar, ukiumwa usinywe asprin au diclopar kwa sababu inaweza kukongezea kuingia kwenye kundi la asilimia 3. Kichwa kikiuma kunywa panadol, pumzika kunywa maji mengi hesabu siku kama umetokewa na matetekuwanga itapita.

Halafu fanyeni bidii mkaushe hayo maji nje ya nyumba zenu, uueni mbu kwa juhudi msisubiri selikali ije. Malaria inayokuja baada ya hayo mafuriko ndo hofu yangu, kwa uzembe wa kusingizia dengue wanaweza wasiwapime malaria wakawekea dripu mkafa kwa sababu ya kukosa tiba sahihi.

Wakati mwingine, kama wasomi wa sekondari na vyuo msikurupuke kushabikia kirahisi. C ajabu mmoja akiambiwa anahoma ya Chikungunya ataona ni mgonjwa sana kuliko hao wa Dengue.

Hii hapa kutoka WHO msome,
1.1.3 Dengue in the WHO African Region
Although dengue exists in the WHO African Region, surveillance data are poor.
Outbreak reports exist, although they are not complete, and there is evidence that
dengue outbreaks are increasing in size and frequency (16). Dengue is not officially
reported to WHO by countries in the region. Dengue-like illness has been recorded
in Africa though usually without laboratory confirmation and could be due to infection
with dengue virus or with viruses such as chikungunya that produce similar clinical
symptoms.
Dengue has mostly been documented in Africa from published reports of serosurveys
or from diagnosis in travellers returning from Africa, and dengue cases from countries
in Sub-Saharan Africa. A serosurvey (17) suggests that dengue existed in Africa as far
back as 1926--1927, when the disease caused an epidemic in Durban, South Africa.
Cases of dengue imported from India were detected in the 1980s (18).
For eastern Africa, the available evidence so far indicates that DEN-1, -2 and -3 appear to
be common causes of acute fever. Examples of this are outbreaks in the Comoros in various
years (1948, 1984 and 1993, DEN-1 and -2) (19) and Mozambique (1984--1985,
DEN-3) (20).
In western Africa in the 1960s, DEN-1, -2 and -3 were isolated for the first time from
samples taken from humans in Nigeria (21). Subsequent dengue outbreaks have been
reported from different countries, as for example from Burkina Faso (1982, DEN-2) (22)
and Senegal (1999, DEN-2) (23). Also DEN-2 and DEN-3 cases were confirmed in
Côte d’Ivoire in 2006 and 2008.
Despite poor surveillance for dengue in Africa, it is clear that epidemic dengue fever
caused by all four dengue serotypes has increased dramatically since 1980, with most
epidemics occurring in eastern Africa, and to a smaller extent in western Africa, though
this situation may be changing in 2008.
While dengue may not appear to be a major public health problem in Africa compared
to the widespread incidence of malaria and HIV/AIDS, the increasing frequency
and severity of dengue epidemics worldwide calls for a better understanding of the
epidemiology of dengue infections with regard to the susceptibility of African populations
to dengue and the interference between dengue and the other major communicable
diseases of the continent.
cc. Yeriko Nyerere Kiranga Tuko mohamed Mtoi @Liwa
 
Last edited by a moderator:
Mohamed mtoi hawezi kuielewa hiyo analysis, hata kidogo. Upeo wake bado ni wa kisiasa zaidi
 
ukukute uumwe ndio ujue kuwa DENGUE IPO mambo mengine hata siamini kuwa yanatengenezwa.
Kwa hili bora nimubali ni miongoni mwa wa Tz wenye IQ ndogo
 
Hiyo ndio historia ya Dengu kwa kifupi, kazi kwetu wana forum
 

Attachments

  • 1400040056171.jpg
    1400040056171.jpg
    11.4 KB · Views: 180
Kwani kasema haipo?
Amesema ipo na wanatumia hiyo kuficha uozo wa 200 billion!!! Ila ameshangaa tu!!! Na mimi nikashangaa pia kuwa hata media ya serikali haiipi attention ya kutosha hii hali!!! Kwa hiyo sasa Yericko Nyerere anashangaa kuwa ni kwa nini measures hazichukuliwi ili tu waendelee kuipa promo na kusahau issue kubwa.
 
haya ni magonjwa ya mlipuko kama ulivyo kipindupindu. kila kipindupindu kikiibuka kinakuwa special! Mtoa mada hajaweza kuleta hoja yoyote ya maana wala ushahidi kuwa hili jambo limetengenezwa.
Kuibuka kwa dengue fever kunazuia vipi kujadiliwa kwa katiba na hayo mabilioni yaliyoibiwa? sioni uhusiano wowote. Hizi ni hoja zingine dhaifu toka kwenye chama kilichodai kuna lori la kura zao limeonekana, lakini hawakuthibitisha, chama kikadai kuna mkanda wa mabomu arusha, lakini hawatuonyeshi, kikwete na timu yake walikuwa hotelini mwanza lakini hawawezi kuthibitisha, ridhiwani anamiliki malori 100 lakini hata chembe ya ushahidi hakuna, Mgimwa raia wa uingereza lakini hawawezi kuthibitisha......This is very simple, mtoa mada alete ushahidi kuwa kabla ya miezi hii miwili mitatu vifo kutokana na dengue fever vilikuwa kawaida tu, hapo nitakubali mara moja, otherwise siwezi kukubali huu uzombi!
ps: mimi sio CCM, maana hawachelewi....

kuanzia januari mpaka sasa kuna wagonjwa 400 na vifo vitatu katika kipindi hiki malaria imeua wangapi??....usifananishe dengue FEVER[ugonjwa unaotibiwa na panadol ili kudhibiti symptons na kipindupindu,kipindupindu kinakuondoa ndani ya 24hrs
 
Amesema ipo na wanatumia hiyo kuficha uozo wa 200 billion!!! Ila ameshangaa tu!!! Na mimi nikashangaa pia kuwa hata media ya serikali haiipi attention ya kutosha hii hali!!! Kwa hiyo sasa Yericko Nyerere anashangaa kuwa ni kwa nini measures hazichukuliwi ili tu waendelee kuipa promo na kusahau issue kubwa.

Inawezekana hujasoma mada

Hebu isome

Kama umeisoma hujaielewa!
 
Mwaka 2011, serikali ilitaka kubadilisha sheria ili iweze kununua vitu chakavu hasa hasa ikilenga kununua mitambo chakavu ya Richmond aka Dowans iliyokuwa inapigiwa kelele sana. Wakati watu walielekezwa kumjadili Babu wa Loliondo tu ili Sheria ile ilibadilishwe na mitambo ya Richmond/Downs vinunuliwe.

Wakati huo huo kulikuwa na kelele kubwa sana ya watu kudai mchakato wa katiba mpya uanze upya. Kila kukicha ilikuwa ni kauli za watu mbali mbali mbali za kuunga au kupinga katiba mpya. wanaounga wakiwa wengi dhidi ya Serikali (Mwanasheria mkuu na Waziri wa Katiba- Kombani) Serikali ilionekana kuibanwa sana kila kona.

Ghafla akaibuka babu wa Loliondo, vyombo vingi vya habari vikiongozwa na TBC1 kama ilivyo sasa vikaipa habari hiyo uzito mkubwa sana kila siku kwa muda mrefu sana. Viongozi wa Serikali wakaenda mpaka Loliondo kukoleza habari igonge vichwa vya habari kwenye vyombo vyote vya habari.

Babu wa Loliondo alisaidia serikali kubadili sheria ya kununua vitu chakavu na mitambo ya Richomond vikanunuliwa, kwa bahati mbaya babu hakuisaidia Serikali kuua mjadala wa madai ya katiba mpya.

Sasa mimi najiwazia tu mwenyewe (loudly thinking). Je, Dengue/Denge/Dengu ni kubwa kiasi hicho au ni mkakati wa kuzima mjadala wa Muungano na serikali tatu unaoilemea serikali kila kona kwa kiwango kikubwa sasa?? Nikitafakari hoja za Lissu kwenye Bunge la Bajeti sitashangaa kama Dengue imekuzwa kimakakati.

Nawasilisha.
 
Duuh,kama kweli vile,mana experience inaonesha haya mambo huja wakati hali ya kisiasa iko hot,
 
kweli wew chura kabisa, unalinganisha upuuzi wa wanasiasa na afya za watu,na baki kuamini akili zako ni nusu
 
Kama na wewe unafikiria hivyo we are doomed Kwa kweli si CCM wala UKAWA kote majanga
 
Back
Top Bottom