Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
Tafakari ya Leo.
Walipofanya Warusi habari zikaenea ulimwenguni, walipofanya Waamerika vitabu vikaandikwa na tukavisoma sana na kufundisha vizazi vyetu kwamba hizo ni zama za Mapinduzi ya viwanda ulimwenguni. Tukajifunza na mengine juu ya ustaarabu wa binadamu.
Walipoibuka Wachina na wengine wimbo ukaendelea ule ule lakini sasa zikaongezeka aya nyingine za nchi zisizofuata haki za binadamu.
Afrika ilipoanza kuchomoza kwa kuacha kufikiria kuwa bila wao walioitwa wa dunia ya kwanza sasa wimbo umebadilika zikaongezwa aya za demokrasia uhuru wa vyombo vya habari, mapambano dhidi ya hili na lile na mengi kama hayo.
Tanzania ilipobadilisha msimamo wa kukaa wakati wengine wanaruka hoja sasa zinazoibuka ni fulani kasema hili leo BBC au VOA ilimradi tu tupoteze mwelekeo wa ujenzi WA SGR, mradi wa Stiglers Gorgle, utoaji wa elimu kwa watoto wetu kuboresha kilimo chetu n.k.
Ni Vyema basi Leo tukumbuke kuwa nasi sasa tunapita katika njia sahihi ili vizazi vyetu visiendelee kusikia mabaya tu ya nchi yao bali waone mema mengi ya mama Tanzania na kuyalinda Kwa gharama yoyote ile.
Sent using Jamii Forums mobile app