Tafakari namna bora ya kuilinda nchi yako na usithubutu kumvua nguo Mama Tanzania

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
871
1,000
Tafakari ya Leo.

Walipofanya Warusi habari zikaenea ulimwenguni, walipofanya Waamerika vitabu vikaandikwa na tukavisoma sana na kufundisha vizazi vyetu kwamba hizo ni zama za Mapinduzi ya viwanda ulimwenguni. Tukajifunza na mengine juu ya ustaarabu wa binadamu.

Walipoibuka Wachina na wengine wimbo ukaendelea ule ule lakini sasa zikaongezeka aya nyingine za nchi zisizofuata haki za binadamu.

Afrika ilipoanza kuchomoza kwa kuacha kufikiria kuwa bila wao walioitwa wa dunia ya kwanza sasa wimbo umebadilika zikaongezwa aya za demokrasia uhuru wa vyombo vya habari, mapambano dhidi ya hili na lile na mengi kama hayo.

Tanzania ilipobadilisha msimamo wa kukaa wakati wengine wanaruka hoja sasa zinazoibuka ni fulani kasema hili leo BBC au VOA ilimradi tu tupoteze mwelekeo wa ujenzi WA SGR, mradi wa Stiglers Gorgle, utoaji wa elimu kwa watoto wetu kuboresha kilimo chetu n.k.

Ni Vyema basi Leo tukumbuke kuwa nasi sasa tunapita katika njia sahihi ili vizazi vyetu visiendelee kusikia mabaya tu ya nchi yao bali waone mema mengi ya mama Tanzania na kuyalinda Kwa gharama yoyote ile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naby Keita

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
4,149
2,000
Naomba kuuliza kipindi hizo nchi zinapita kwenye huo mpito kulitokea upotevu wa 2.4 Trillion?
hadi maisha ya raia wengi yalipotea sio pesa tu....tafuta historia za hao wa ulaya na huko marekani kabla hawajafikia hapo walipo sasa walipigikaje
 
mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
2,527
2,000
we acha siasa za kitoto hizo.Utoto unakusumbua tu.Hiyo mifano uliyotoa haiingiliani kabisa na Tanzania.Chini ya ccm.Miaka zaidi ya 50 ya uhuru hali mbaya.
Kwa upumbavu mtu anadhani SGR itapunguza umaskini,kama kaama walioua gesi mtwara wapo,reli ya Tazara wapo,reli ya kati wapo,viwanda vya magari na baiskeli bado wapo madarakani basi maendeleo subiri kwenye ndotoSent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo wewe ulitakaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
2,527
2,000
ninataka mabadiliko ya kimfumo katika kuendesha nchi.kuweka mbele miradi yenye kumwinua mtu wa chini.
mfano sera yaTZ ya viwanda kama ingekuwa serious kusingekuwa tena na wazururaji hovyo mtaani tena wenye nguvu na elimu zao,lakin sera imeshindwa.
Ukijikita kuendeleza maendeleo ya vitu badala ya watu huwa kuna athari mbaya.mfano,Ethiopia ina miradi mikubwa kabisa ya umeme,umwagiliani,shilika la ndege,Treni ya umeme n.k lakin raia wake ni masikikin sana.Hii ni kwa sababu hayo mavitu ni ya mkopo,pesa nyingi inayopatikana inaenda kurudisha madeni mbaya zaidi madeni hayalipiki.
Ukitaka maendeleo ya vitu anza na hatua chache angalau viwanda vidogovidogo then bidhaa zote zinazozalishwa kwa wingi nchi,za namna ileile zinazotoka nje unapiga pini.mfano vitu kama daftari,kalamu,sahani,juice,n.k .Hiibinakusaidia kukuza uchumi wa ndani.Lakin yeye huyu anaangaika na kugombana na matajiri wa TZ afu bado anaenda kuchota hela hazina na kufanya anachoona kinafaa bila hata kuangalia wataalam wanashauri nini.

Kwahiyo wewe ulitakaje

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
SirChief

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
2,850
2,000
Kwahiyo wewe ulitakaje

Sent using Jamii Forums mobile app
Tushirikiane pamoja kuijenga nchi yetu,hakuna tabaka lenye haki zaidi ya tabaka jingine hapa nchini.Kama mtu fulani anaeza kumdhuru/kumfanyia kitu kibaya mwenzake eti sababu tu wanatofautiana kimawazo na ideology za kisiasa sio sawa na hii siyo Tanzania tunayoitaka.Kama mtu leo akisimama akasema mradi wa Stiglers Gorge una alternative yake ambayo ni efective na cheap.Huyu mtu hatakiwi kuonekana ni adui wa Nchi,anatakiwa kupewa nafasi asikilizwe mawazo yake.Sio kumdhuru na kumuona adui.Hivi ndo tunatakiwa kujenga mama yetu Tanzania.
 
SirChief

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
2,850
2,000
ninataka mabadiliko ya kimfumo katika kuendesha nchi.kuweka mbele miradi yenye kumwinua mtu wa chini.
mfano sera yaTZ ya viwanda kama ingekuwa serious kusingekuwa tena na wazururaji hovyo mtaani tena wenye nguvu na elimu zao,lakin sera imeshindwa.
Ukijikita kuendeleza maendeleo ya vitu badala ya watu huwa kuna athari mbaya.mfano,Ethiopia ina miradi mikubwa kabisa ya umeme,umwagiliani,shilika la ndege,Treni ya umeme n.k lakin raia wake ni masikikin sana.Hii ni kwa sababu hayo mavitu ni ya mkopo,pesa nyingi inayopatikana inaenda kurudisha madeni mbaya zaidi madeni hayalipiki.
Ukitaka maendeleo ya vitu anza na hatua chache angalau viwanda vidogovidogo then bidhaa zote zinazozalishwa kwa wingi nchi,za namna ileile zinazotoka nje unapiga pini.mfano vitu kama daftari,kalamu,sahani,juice,n.k .Hiibinakusaidia kukuza uchumi wa ndani.Lakin yeye huyu anaangaika na kugombana na matajiri wa TZ afu bado anaenda kuchota hela hazina na kufanya anachoona kinafaa bila hata kuangalia wataalam wanashauri nini.Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa asipoelewa atakuwa mbishi tu.
 
Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
871
1,000
Tushirikiane pamoja kuijenga nchi yetu,hakuna tabaka lenye haki zaidi ya tabaka jingine hapa nchini.Kama mtu fulani anaeza kumdhuru/kumfanyia kitu kibaya mwenzake eti sababu tu wanatofautiana kimawazo na ideology za kisiasa sio sawa na hii siyo Tanzania tunayoitaka.Kama mtu leo akisimama akasema mradi wa Stiglers Gorge una alternative yake ambayo ni efective na cheap.Huyu mtu hatakiwi kuonekana ni adui wa Nchi,anatakiwa kupewa nafasi asikilizwe mawazo yake.Sio kumdhuru na kumuona adui.Hivi ndo tunatakiwa kujenga mama yetu Tanzania.
Ni nani kwa ushahidi aliewahi kudhurika kwa kusema jambo jema la kusaidia nchi?
Ama ni nani ambaye amewahi kukatazwa kusema jambo linalojemga uchumi wa nchi akafungwa mdomo?
Usiishi kwa kufuata maandiko ya watu kwenye mitandao
Fatilia mambo kisha sema unalojua. Kwa uelewa wako wewe ni kijana wa Taifa letu ambae tunakutegemea ulijenge taifa lako lakini sio kubomoa taifa lako kwa hoja dhaifu za kuokoteza kwenye mitandao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SirChief

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
2,850
2,000
Ni nani kwa ushahidi aliewahi kudhurika kwa kusema jambo jema la kusaidia nchi?
Ama ni nani ambaye amewahi kukatazwa kusema jambo linalojemga uchumi wa nchi akafungwa mdomo?
Usiishi kwa kufuata maandiko ya watu kwenye mitandao
Fatilia mambo kisha sema unalojua. Kwa uelewa wako wewe ni kijana wa Taifa letu ambae tunakutegemea ulijenge taifa lako lakini sio kubomoa taifa lako kwa hoja dhaifu za kuokoteza kwenye mitandao

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona unatoka mapovu tu,ongea kwa facts tutakuskiliza,acha vijembe na kujiona unajua....Idiot
Mifano hii hapa,usipokubaliana nayo,Idon't give a damn.
1."The best way to deal with makinikia saga ni kuanza kudeal na mikataba ya kimataifa kwanza inayokumbatia wawekezaji na kuwalinda"---(Tundu Lisu).Akala risasi 38.
2."Stieglers Gorge mbadawa wake ni umeme wa upepo na kutumia gesia asilia tulionayo"---(Zitto na Heche),Hawa mliwananga hadharani na kusema wanapinga kila kitu na hawalitakii mema taifa.

N.B wote tunajenga nyumba moja,tusigomanie fito na nguzo
 
dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,540
2,000
Hivi huyu mama hajafikia Menopause kweli au!!! Tusije kumvua tukazani binti kumbe kashafikia utu uzima
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom