Watanzania tujifunze na kujadili hatma ya vizazi vyetu, hali ya nchi ni mbaya sana

CONSISTENCY

Senior Member
Feb 16, 2023
135
307
Kuna mambo mengi ya hovyo yanaendelea nchini,
Bandari
Utalii
Madini
Mikopo ya kijinga
Ufisadi CAG report
Mfumuko wa bei n.k

Wanasiasa tumewapa dhamana kubwa ya kutuongoza ila nasikitika kusema wengi wa wanasiasa nchini Tanzania ni walafi, vibaraka na watumwa wa wageni.

Nasikitika kusema Rais ana uwezo mdogo sana wa kuongoza hii nchi, amezungukwa na wahuni wenye lengo la kunyonya nchi kadiri iwezekanavyo.

Inawezekana Rais hapendi haya yanayoendelea ila hana namna ya kutatua sababu wenye nguvu ya kuamua urais wake ndio wanaofanya kila namna kuinyonya hii nchi.

Wito wangu kwa watanzania wote, naomba tujadili namna kuikomboa nchi bila kutegemea wanasiasa, hatma ya vizazi vyetu ipo mikononi mwetu wote.

Wanasiasa wa sasa hawaaminiki na hata bunge haliaminiki.
 
Haya yote yatapita tu, niliwahi kukaa na mzungu mmoja Toka us hata huko kwao ujinga kama huu ulikuwepo ila watu waliparangana sana na kuuana sana usione mpaka wamefikia hatua hii Kila mtu kaamua kumheshimu mwenzake

Inasikitisha sana tulikua tunasoma vitabu vya historia mababu zetu Wanabadilishana madini na vioo, ila baada ya elimu yote tulizopewa huu upuuzi bado unaendelea, baada ya Miaka 50 watoto wetu na wajukuu zetu watatuona tulikua wajinga sana
 
CCM imejaa wahuni, wezi na walafi. CCM imeambukiza hii tabia mbaya kwa watanzania walio wengi, sasa hivi kila mtanzania anawaza kuliibia taifa, source ni CCM.

Hadi hapo hili dubwana litakapoondolewa, kukawekwa misingi mipya ya kuliongoza taifa, tukapanda mbegu mpya ya uzalendo, nadhani safari yetu ni ndefu sana.
 
Kuna mambo mengi ya hovyo yanaendelea nchini,
Bandari
Utalii
Madini
Mikopo ya kijinga
Ufisadi CAG report
Mfumuko wa bei n.k
Wanasiasa tumewapa dhamana kubwa ya kutuongoza ila nasikitika kusema wengi wa wanasiasa nchini Tanzania ni walafi, vibaraka na watumwa wa wageni.

Nasikitika kusema Raisi ana uwezo mdogo sana wa kuongoza hii nchi, amezungukwa na wahuni wenye lengo la kunyonya nchi kadiri iwezekanavyo.

Inawezekana Rais hapendi haya yanayoendelea ila hana namna ya kutatua sababu wenye nguvu ya kuamua urais wake ndio wanaofanya kila namna kuinyonya hii nchi.

Wito wangu kwa watanzania wote, naomba tujadili namna kuikomboa nchi bila kutegemea wanasiasa, hatma ya vizazi vyetu ipo mikononi mwetu wote.

Wanasiasa wa sasa hawaaminiki na hata bunge haliaminiki.
huwa najiuliza, hivi mtu wa pwani au zanzibar, anaweza kuwa na uchungu na mbuga zetu kweli? yeye mwambie samaki wa baharini, atakuona wa maana, hayo mawanyama kwake hata hayaelewi,no wonder kuna mtu alipoingia tu kwenye kiti alisema tuanze kuchimba madini hadi kwenye mbuga za wanyama. hawana uchungu. its time to wake up kuitetea Tanganyika.
 
Kuna rafiki yangu ni PHd holder tulikuwa tunajadiliana naye jana,sote tukakubaliana kuwa kutokana na Watanzania kulala usingizi wa pono inabidi apatikane Putin wa Tanzania wenye uchu na Nchi,mzalendo wa Nchi yake na mwenye akili awaamushe.
 
Viongozi wetu wapo safi sana na ni watu wakazi vizuri kabisa .. ila shida sisi wananchi ndo mizukule, maiti, haswa vijana . yani tumekosa uthubutu wa kufanya lolote hivyo viongozi wameona wanongoza maiti .. vizazi vyetu vikiwa timamu vitafukua maiti zetu na kuanza kuzicha bakora kwa uchungu sana,
 
Haya yote yatapita tu
Hayawezi kupita, tuache ubinafsi tufikirie vizazi vijavyo tuamke tuwapambanie.
Hivi walopigania uhuru wangekua waoga waoga na kusema yatapita sisi saivi tungekua tunaishije!?
Ifike sehem tukatae huu ushenzi wa wachache wao watoto zao wanawakimbiza nnje na kurithishana vitengo, watoto wetu ndo watakaumia zaidi na huu upumbavu.
 
Kuna mambo mengi ya hovyo yanaendelea nchini,
Bandari
Utalii
Madini
Mikopo ya kijinga
Ufisadi CAG report
Mfumuko wa bei n.k
Wanasiasa tumewapa dhamana kubwa ya kutuongoza ila nasikitika kusema wengi wa wanasiasa nchini Tanzania ni walafi, vibaraka na watumwa wa wageni.

Nasikitika kusema Raisi ana uwezo mdogo sana wa kuongoza hii nchi, amezungukwa na wahuni wenye lengo la kunyonya nchi kadiri iwezekanavyo.

Inawezekana Rais hapendi haya yanayoendelea ila hana namna ya kutatua sababu wenye nguvu ya kuamua urais wake ndio wanaofanya kila namna kuinyonya hii nchi.

Wito wangu kwa watanzania wote, naomba tujadili namna kuikomboa nchi bila kutegemea wanasiasa, hatma ya vizazi vyetu ipo mikononi mwetu wote.

Wanasiasa wa sasa hawaaminiki na hata bunge haliaminiki.
Watu siku hizi wapo bize sana na mpira.. mara simba mara yanga,, sijui liverpool sijui man city... Na kuwa macomedian wa kwenye social media... Kujifunza uchawa, kujipendekeza KWa ajili ya teuzi (sio mtu kutaka uongozi Ili alete mabadiliko kwenye sehemu fulani ambayo haiji Sawa) ila tu kwenye maisha yake aseme naye alikuwa kiongozi.. na ndio maana wenye nia ovu wakafurahi wanaendelea kuchafua........ Huku wabongo wakiendelea kukaziana mafuvu kwenye uchawa na mipila wao wanaendelea na yao....
 
Hayawezi kupita, tuache ubinafsi tufikirie vizazi vijavyo tuamke tuwapambanie.
Hivi walopigania uhuru wangekua waoga waoga na kusema yatapita sisi saivi tungekua tunaishije!?
Ifike sehem tukatae huu ushenzi wa wachache wao watoto zao wanawakimbiza nnje na kurithishana vitengo, watoto wetu ndo watakaumia zaidi na huu upumbavu.
Inasikitisha sana, magufuli alisema kupingana na mafisadi ni vita kubwa, tunaanza kumuelewa
 
Hayawezi kupita, tuache ubinafsi tufikirie vizazi vijavyo tuamke tuwapambanie.
Hivi walopigania uhuru wangekua waoga waoga na kusema yatapita sisi saivi tungekua tunaishije!?
Ifike sehem tukatae huu ushenzi wa wachache wao watoto zao wanawakimbiza nnje na kurithishana vitengo, watoto wetu ndo watakaumia zaidi na huu upumbavu.
Tulia mkeka wa ma DAS na DED ndio huo,wacha waendelee kulamba asali na kuuza nchi
FB_IMG_1686206790040.jpg
 
CCM imejaa wahuni, wezi na walafi. CCM imeambukiza hii tabia mbaya kwa watanzania walio wengi, sasa hivi kila mtanzania anawaza kuliibia taifa, source ni CCM.

Hadi hapo hili dubwana litakapoondolewa, kukawekwa misingi mipya ya kuliongoza taifa, tukapanda mbegu mpya ya uzalendo, nadhani safari yetu ni ndefu sana.
Kabisa mkuu....hilo 'dubwana' ndio adui wa nchi.
 
Back
Top Bottom