Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 14,597
- 18,414
Wewe unaishi wapi ?Chonde chonde jamani! Bei ya unga wa sembe itakuja kufika sh2000+ hapa tuje tutafute mchawi ni nani?
Biashara ya kuexport bidhaa nje inataka tujipange katika uzalishaji na kudhibiti kiwango cha matumizi ya ndani itosheleze bila ya kumuathiri mlaji kutokana na mripuko wa bei. Tanzania bado hatijajipanga uzalishaji wa ku export na tukilazimisha kutakuwa na mripuko wa bei na tushindwe kumiliki hata mlo mmoja kwa siku
Na unauhakika unachokisema.
Nenda Songea, gunia la mahindi wakulima wanauza Hadi 20,000/= TSH.
Wakulima waneacha kulima mahindi wakajaribu kunde mbaazi, nazo zikaachwa shambani kwa kukosa soko lake.
Sehemu kubwa yaTanzania ni eneo zuri kwa kilimo.
Watu tumeamua kuja mjini kutafuta pesa BAADA ya mazao kukosa soko.
Serikaki ikiruhusu mauzo huria ya mazao yetu wengi tutarudi kulima mazao ya chakula kwa ajiri ya chakula na biashara.
Songea Gunia la mahindi watu wanauza Hadi 15,000/ na wanakosa wateja.
Wacha serikali iruhusu soko la mahindi na unga wake ili wakulima wapate uwanda mpana wa kuuza mazao yao hayo.
Nakushauri kama utakumbwa na njaa Njoo Songea mjini ulizia Kijiji cha Lugagala, utakula na kushiba maisha yako yote, huko hakuna njaa unayoihofia.
TUNATAKA KUUZA MAHINDI NJE, KENYA, MALAWI ZAMBIA, ZIMBABWE, SUDANI, SIMALIA WANAYAHITAJI SANA.
TUMECHOKA KUKIMBIZANA NA MGAMBO HAPA MJINI.