Tafadhali Serikali uzeni mahindi Kenya, sio unga

chikambabatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
1,382
Reaction score
1,349
Wakulima wa mahindi wanapenda wapate soko la mazao yao. Ila iwapo kutakuwa na vikwazo vingi kama lazima mauzo ya nje yawe unga, ushuru na tozo mbali mbali, matokeo yake, biashara ya nje itashindikana, hivyo kukosa soko jumla, mnatuumiza sana.

Ni kwanini ulazimishe unga, kama wao wanapenda kande inakuwaje. Pia ifahamike, unga unaharibika mapema kuliko mahindi, Mahindi yataendelea kulimwa kwa wingi tu, iwapo yataendelea kupata soko la uhakika.

Kwa kweli sijui kwa nini hamjifunzi makosa ya kuingilia mazao kama kwanye korosho, hadi leo baadhi ya watu hawalipwa korosho, na hata waliosafirisha korosho kutoka vyama vya msingi hadi maghala ya mnada baadhi wamepata malipo theluthi ya madai yao.

Mimi nikiwa mkulima sipendi uingiliaji huo, na sijali habari ya misifa ya sgr, ndege, bwawa la umeme wala elimu bure, na nawaangalia tu akina Mpoto misifa kibao, sisi huku sijui kwanini na asimwambie atulipe ndio aendelee na sifa zake.
 
Kwenye hili swala la kuuza unga badala ya mahindi kwa jirani zetu wakenya bado ni utata mtupu sidhani kama wakenya watalikubali hili koz wao wanahitaji mahindi na sio unga wakati sisi tuna force kuwapa unga kama finished product. Wakenya ni wapenzi sana wa getheri (makande ) je serikali imeangalia hili kuwa unga hauwezi pika getheri? kwa upande wangu hili swala wakae chini wa tafakari zaidi
 
Ni kwanini ulazimishe unga, kama wao wanapenda kande inakuwaje. Pia ifahamike, unga unaharibika mapema kuliko mahindi,
Mahindi yataendelea kulimwa kwa wingi tu, iwapo yataendelea kupata soko la uhakika.
Kwa kweli sijui kwa nini hamjifunzi makosa ya kuingilia mazao kama kwanye korosho, hadi leo baadhi ya watu hawalipwa korosho, na hata waliosafirisha korosho kutoka vyama vya msingi hadi maghala ya mnada baadhi wamepata malipo theluthi ya madai yao.
Mimi nikiwa mkulima sipendi uingiliaji huo, na sijali habari ya misifa ya sgr, ndege, bwawa la umeme wala elimu bure, na nawaangalia tu akina Mpoto misifa kibao, sisi huku sijui kwanini na asimwambie atulipe ndio aendelee na sifa zake.
Mkiwapa masharti mengi kuwauzia unga tu mnakosea.nilowahi somesha mtoto Kenya ambapo chakula kikuu ilikua kande Githeri so mnawezaona mahiyaji yao yalivyo
 
Kabudi na Bashe wachangamkie fursa ya Mahindi Iran. Kwasababu Iran sasa hivi inasitisha kununua mahindi, nyama (beef) na soya kutoka Brazil baada ya Brazil kushikilia meli zake mbili.

Waende Iran siyo kukodoakodoa mimacho na kusifusifu kutolowa jalalani
 
hivyoo ni vikwazo ili mzigo usitoke mwingi nje ya inchi mkasaga unga kwa wingi na mkauza nje watapiga stop na huo unga.

kuna maeneo mengi nimeona wasafirishaji wa mahindi wakilalamika.
 
Kwenye hili swala la kuuza unga badala ya mahindi kwa jirani zetu wakenya bado ni utata mtupu sidhani kama wakenya watalikubali hili koz wao wanahitaji mahindi na sio unga wakati sisi tuna force kuwapa unga kama finished product. Wakenya ni wapenzi sana wa getheri (makande ) je serikali imeangalia hili kuwa unga hauwezi pika getheri? kwa upande wangu hili swala wakae chini wa tafakari zaidi
Mambo wayafanyayo sijui huwa wanakaa na kutafakari, na ndipo wamshauri, sababu wanafikiri kupata tu faida na sifa, bila kujali changamoto na mazingira na ukweli. Mwasho wanatutia mtaroni, wenyewe hawaathiriki hata kidogo.
 
Tusisahau hii nafasi ya kununua mahindi Tanzania haikuwa last option kwao, wakenya (wafanya biashara wa kubwa) walizozana sana na serikali yao wakitaka import mahindi toka Mexico kwa mda mrefu sana, ndipo mwisho Serikali ya Kenya ikatoa nafasi ya upendeleo kwa Watanzania. Sasa leo sisi tuna uza kwa maringo tena duuuh!!
 
Kabudi na Bashe wachangamkie fursa ya Mahindi Iran. Kwasababu Iran sasa hivi inasitisha kununua mahindi, nyama (beef) na soya kutoka Brazil baada ya Brazil kushikilia meli zake mbili.

Waende Iran siyo kukodoakodoa mimacho na kusifusifu kutolowa jalalani
Chonde chonde jamani! Bei ya unga wa sembe itakuja kufika sh2000+ hapa tuje tutafute mchawi ni nani?

Biashara ya kuexport bidhaa nje inataka tujipange katika uzalishaji na kudhibiti kiwango cha matumizi ya ndani itosheleze bila ya kumuathiri mlaji kutokana na mripuko wa bei. Tanzania bado hatijajipanga uzalishaji wa ku export na tukilazimisha kutakuwa na mripuko wa bei na tushindwe kumiliki hata mlo mmoja kwa siku
 
Ikitokea demand kubwa tutalima zaidi wakulima ndo wataneemeka
 
Sio kwenye staple food kaka yangu, tutakuja kutafuta mchawi nani. Ulimaji wenyewe huu wa jembe la mkono 80%? Kuneemeka wakulima ndivo tunavotaka.
 
Madalali imekula kwenu nendeni mkalime acheni kupenda mtelezo
 
hivyoo ni vikwazo ili mzigo usitoke mwingi nje ya inchi mkasaga unga kwa wingi na mkauza nje watapiga stop na huo unga.

kuna maeneo mengi nimeona wasafirishaji wa mahindi wakilalamika.
Ndugu yangu hapo sasa ni suala la takwimu. Bila takwimu hamna uwezo wa kupanga mipango ya maendeleo. Uwekezaji kwenye takwimu ili kujua tumezalisha kiasi gani na tuuze kiasi. Suala la vikwazo ni kutiana umaskini na hasira tu.
 
ukiona watu wanakimbiza mitaji kuwekeza nje ndo mambo kama haya serekali awamu hii haitabariki kabisaa ni kichomi.
 
Good point. Kulazimisha wakenya wanunue unga badala ya mahindi, huo ni Ubeberu.
Pia hii inamnyonya mkulima. Mkulima akiuza mahindi kwenye soko la nje hupata pesa mingi kuliko akiuza mahindi kwenye viwanda ambavyo husaga unga na ku export.
 
Kabudi na Bashe wachangamkie fursa ya Mahindi Iran. Kwasababu Iran sasa hivi inasitisha kununua mahindi, nyama (beef) na soya kutoka Brazil baada ya Brazil kushikilia meli zake mbili.

Waende Iran siyo kukodoakodoa mimacho na kusifusifu kutolowa jalalani
unadhani biashara ya kimataifa inafanywa kama unavuouza maharagwe soko la kariakoo?
 
Wakulima wa mahindi wanapenda wapate soko la mazao yao. Ila iwapo kutakuwa na vikwazo vingi kama lazima mauzo ya nje yawe unga, ushuru na tozo mbali mbali, matokeo yake, biashara ya nje itashindikana, hivyo kukosa soko jumla, mnatuumiza sana.

Ni kwanini ulazimishe unga, kama wao wanapenda kande inakuwaje. Pia ifahamike, unga unaharibika mapema kuliko mahindi, Mahindi yataendelea kulimwa kwa wingi tu, iwapo yataendelea kupata soko la uhakika.

Kwa kweli sijui kwa nini hamjifunzi makosa ya kuingilia mazao kama kwanye korosho, hadi leo baadhi ya watu hawalipwa korosho, na hata waliosafirisha korosho kutoka vyama vya msingi hadi maghala ya mnada baadhi wamepata malipo theluthi ya madai yao.

Mimi nikiwa mkulima sipendi uingiliaji huo, na sijali habari ya misifa ya sgr, ndege, bwawa la umeme wala elimu bure, na nawaangalia tu akina Mpoto misifa kibao, sisi huku sijui kwanini na asimwambie atulipe ndio aendelee na sifa zake.
Any processed food add value. Its a good strategy. Do analysis before creating threads like this. I hope you are not one of those from the other side opposing everything good the government doing to the Tzs. Think selling unprocessed/ processed cashewnut where there is more money?

Back to maize after processing there is animal feeds.
 
Tena zitatengenezwa ajira kwenye hivyo viwanda vya unga hawa wanaolalamika wote ni watu wa kati tu waliokua wananeemeka na kuwakandamiza masikini
 
Back
Top Bottom