Wakulima wa mahindi wanapenda wapate soko la mazao yao. Ila iwapo kutakuwa na vikwazo vingi kama lazima mauzo ya nje yawe unga, ushuru na tozo mbali mbali, matokeo yake, biashara ya nje itashindikana, hivyo kukosa soko jumla, mnatuumiza sana.
Ni kwanini ulazimishe unga, kama wao wanapenda kande inakuwaje. Pia ifahamike, unga unaharibika mapema kuliko mahindi, Mahindi yataendelea kulimwa kwa wingi tu, iwapo yataendelea kupata soko la uhakika.
Kwa kweli sijui kwa nini hamjifunzi makosa ya kuingilia mazao kama kwanye korosho, hadi leo baadhi ya watu hawalipwa korosho, na hata waliosafirisha korosho kutoka vyama vya msingi hadi maghala ya mnada baadhi wamepata malipo theluthi ya madai yao.
Mimi nikiwa mkulima sipendi uingiliaji huo, na sijali habari ya misifa ya sgr, ndege, bwawa la umeme wala elimu bure, na nawaangalia tu akina Mpoto misifa kibao, sisi huku sijui kwanini na asimwambie atulipe ndio aendelee na sifa zake.