Tafadhali Rais Magufuli Kabla Hujateua Waziri Mwingine wa Madini na Nishati

nchi hii hatujielewi mkuu ushauri wako ni bora kwa mustakabali wa nchi tatizo ni pale raisi atakapoifanya sekta ya madini kuwa chini yake wajinga watamuita dikteta!!
Athubutu kama hajaenda mwenyewe na maji, mchawi mpe mwana alee. Hakuna wajinga bali u kweli ndio utamuita dikteta athubutu aone.
 
Mzee Mkijiji.. Kuna mada uliwahi kuleta hapa miaka ya nyuma ukiuliza kwanini tunaacha mlango wazi alafu tunatudi kulalamika kua tumeibiwa? ilikua kipindi cha JK.
Nashangaa leo unarudi kulalamika wakati mlango umeiacha wazi, hivi wadau mnaelewa sababu ya kupeleka mswada bungeni kwa hati ya dharura utafikiri ni mswada wa kutipisha nchi kuingia vitani?

Siwezi kutoa mapendekezo kwa sasa make Jirani yangu anapiga Pesa kupitia hizi loophole za mikataba zetu najua akitosheka atanigawia mie jirani yake.

Tumekua wapumbafu sana waTanzania.

Mpumbavu mwenyewe, mmekuwa mkijpa uongozi kwa kujuana na ubaguzi mnapofeli mnataka kutuhusisha Watanzania wote? Mnachagua wa kwenu, wenzenu bila kuzingatia weledi sasa jifunzeni kuwajibika pia.
Watanzania wenye sifa, wazalendo, wajuvi, weledi wako tele mnawatosa kwa kuangalia know who.
 
Mbona hata katika hizo wizara unazopendekeza kuna overlap kubwa sana? Yaan gesi ambayo nayo ni nishati iwe wizara tofauti na wizara ya nishati? Kumbuka, tuna gesi tayari-hatupo ktk exploration stage.

Mimi nadhani wizara hii inaweza kufanya kazi yake vizuri sana hata bila kugawanywa. Kilichokuwa kinakosekana ni nia njema na political will ktk mikataba mbali mbali ya wizara hii. Ndiyo maana Sheria zake nyingi zilipelekwa bungen chapchap kwa hati ya dharura na kupitishwa usiku tukiwa tumelala. Kwakuwa sasa kuna political will, tumshauri rais na Bunge sasa wafumue Sheria na mikataba ya sekta hiyo ili ijadiliwe kwa kina kwa maslahi ya taifa. Kila mtu ajue tunapata nn kwenye madini. Kukiwa na Sheria na mikataba mizuri, yoyote anaweza kuongoza wizara hiyo.
Sidhani kama umenielewa. Karibu sekta zote zinq overlap lakini haina maana ziunganishwe ziwe moja.
 
Mimi Nadhani Paulo Makonda atafaa sana kwenye wizara ya Nishati na Madini

Ni msomi..Ni mtu makini..mzalendo na mchapakazi...Zaidi ni kipenzi cha magufuli..Anajua mambo ya kimikataba

Wengine mko mnamuwaza sana Makonda na kumpa umuhimu mkubwa kuliko anaoustahili. Haiwezekani watu wanamtaja yeye kwenye kila mijadala ili kumpa jina zaidi. Ni vizuri watu wakakubali hili limetoka hiyo wafikirie mambo mengine.
 
Asipojua umuhimu wa bunge kuwa bunge na mahakama kuwa mahakama hata angechukua wizara zote kuwa chini yake hakuna hatua tutakayo piga...tuimarishe mifumo ya kuongoza nchi tusitegemee mtu mmoja kutuvusha....
 
Chazo cha kashfa katika sekta ya madini na nishati ni UTAIFA WA RASLIMALI (RESOURCE NATIONALISM)
Kkwa hiyo tufanye sisi wenyewe kazi hiyo sekta binafsi iondoke.
Twendwe London na NewYork Stock Exachages tununue makampuni yote ya kigeni ynayofanya kazi hapa ili hizo mali ziwe zetu kama taifa.
 
Mtu pekee anaweza kutoa ushauri na ukafanyiwa kazi na kaka mkuu ni Daudi Bashite wengine tunapiga kelele na hataki tumahauri.
 
Naomba nitoe pendekezo moja kwa Rais Magufuli kabla hajamfikiria au hata kumteua mtu mwingine kushika nafasi ya Waziri Muhongo aliyefukuzwa kazi kufuatia kashfa ya makontena ya michanga yenye madini.
....

Pendekezo langu - na inawezekana wengine pia wamewahi kulitoa - ni kuwa ipo haja ya kuwa na wizara mbili ambazo zitaweza kusimamia vizuri sekta hizi mbili, chini ya Mawaziri wawili tofauti.

.

Wengine wanasema Rais Magufuli hasikii ushauri sijui kichwa ngumu sijui nini; kumbe ukijenga hoja vizuri, kwa heshima na ikamshawishi ni msikilizaji mzuri. Ushahidi ndio huo... Thanks my president! Ila ongeza hilo la Gesi na Mafuta pleaseeee
 
Wengine wanasema Rais Magufuli hasikii ushauri sijui kichwa ngumu sijui nini; kumbe ukijenga hoja vizuri, kwa heshima na ikamshawishi ni msikilizaji mzuri. Ushahidi ndio huo... Thanks my president! Ila ongeza hilo la Gesi na Mafuta pleaseeee
Vijana wa humu jamvini wanafaa kuiga mfano wako...nimekaa miaka sita hapa jamvini sijawahi kusikia umepigwa ban wala kumtukana mtu.

Hoja hujibiwa kwa hoja...Ujinga wanaoufanya wapinzani ni kama vile kumchokoza Magufuli ili waone atafanyaje...

Siasa za wapinzani ni za kuviziavizia badala ya kujenga hoja kwa facts...

Najaribu kumkumbuka Slaa anbaye alijenga hoja panapohitaji hoja na alifoka panapohitaji kufoka.
 
Wengine wanasema Rais Magufuli hasikii ushauri sijui kichwa ngumu sijui nini; kumbe ukijenga hoja vizuri, kwa heshima na ikamshawishi ni msikilizaji mzuri. Ushahidi ndio huo... Thanks my president! Ila ongeza hilo la Gesi na Mafuta pleaseeee

Vipi kuhusu bunge live?

Vipi kuhusu uhuru wa vyama vya siasa kufanya siasa zao kama sheria inavyoruhusu?
 
Exactly MM
"yaani Magufuli mwenyewe achukue dhamana ya Sekta ya Madini hadi atakapojiridhisha kuwa mifumo, na misingi mizuri ya kusimamia sekta hii imewekwa. Hivyo, napendekeza amteue Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Madini) ambaye ndiye atakuwa msaidizi wake mkubwa wa kusimamia Wizara ya Madini hadi pale atakapoona ni vyema airudishe nje ya Ikulu".
 
Amazing. Jamaa naona kasikiliza hii hoja yako. Obviously kuna vijana wake wanaosoma humu na kumpelekea au kumshauri.

Sasa kama ni ndivyo ilivo basi kuna jambo jingine la kumshauri. Nalo ni swala la kustimulate mzunguko wa hela na biashara katika nchi. Kama kuna wajuvi wazuri wa uchumi, wanaompenda na kumheshimu na wanajua kujenga hoja basi wajitokeze kumwambia kwamba inawezekana kutengeneza mazingira yanayostawisha biashara na mzunguko wa hela bila kuruhusu ufisadi. Baadhi ya hatua alizochukua zina nia njema ili pesa ya walipa kodi isitumike vibaya (mfano pesa zote za umma kupelekwa central bank) lakini kwa kiasi kikubwa zimeathiri mzunguko wa hela. So wajuvi wa uchumi jitokezeni na anzisheni threads zenye ushauri mwanana.
 
Back
Top Bottom