Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,768
- 41,010
Naomba nitoe pendekezo moja kwa Rais Magufuli kabla hajamfikiria au hata kumteua mtu mwingine kushika nafasi ya Waziri Muhongo aliyefukuzwa kazi kufuatia kashfa ya makontena ya michanga yenye madini.
Pendekezo hili si geni kwani nililitoa pia mara baada ya uchaguzi na kabla hajaunda Baraza la Mawaziri. Msingi wa pendekezo hili ni ukweli kuwa Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ni sehemu ambayo ni ngumu watu kukaa lakini pia inagusa sana maisha na uchumi wa nchi kiasi kwamba kila inapotikisika au kunapotokea matatizo basi kuna mengine mengi yanaenda nayo. Kufanikiwa kwa nchi yoyote kunategemea sana kati ya mengi ni hili la madini na nishati.
Pendekezo langu ni kuwa ni wakati muafaka kutenganisha Wizara hii katika sehemu zake za kimantiki badala ilivyo sasa ambapo inaonekana wizara mbili zimelazimishwa kukaa pamoja chini ya mtu mmoja. Kila tatizo linapotokea upande mmoja basi upande mwingine nao unaathirika. Kwa mfano, sasa hivi kumetokea matatizo kwenye upande wa Madini na kusababisha Waziri kujiuzulu lakini upande wa Nishati nao unaenda kupoteza Waziri wake. Na hili linakuwa kweli ikiwa kinyume na hata kwa viongozi wengine wa kuu wa Wizara.
Pendekezo langu - na inawezekana wengine pia wamewahi kulitoa - ni kuwa ipo haja ya kuwa na wizara mbili ambazo zitaweza kusimamia vizuri sekta hizi mbili, chini ya Mawaziri wawili tofauti.
Kuwe na WIZARA YA MADINI, GESI NA UTAFUTAJI WA MAFUTA (Ministry of Mining, Gas and Oil Exploration); pale mafuta yatakapothibitika kupatikana na kuweza kuingizwa katika biashara basi wizara itakuwa ni ya Madini, Gesi na Mafuta. Na hii itahusiana na kazi zote za extraction ya madini, gesi na mafuta.
Hii ndio itakuwa ni wizara itakayohusika na masuala yote ya madini, gesi na mambo mafuta kabla raslimali hizo hazijaingizwa katika mifumo au mabadiliko yoyote ambayo yanaweza kusababisha yahame kwenda majukumu ya wizara nyingine.
Wizara ya pili ibakiwa kuwa ni WIZARA YA NISHATI (Ministry of Energy) ambayo kazi yake kubwa ni kusimamia sekta nzima inayohusiana na uzalishaji, usimamizi, usambazaji na matumizi ya nishati.
Lakini pendekezo langu linaenda mbali zaidi ya kutenganisha tu wizara hizi. Kwa wakati huu na kutokana na uzoefu wetu wa muda mrefu kuhusiana na sekta hizi mbili (Nishati na Madini) naamini si hekima, si vizuri, na si sawa kumteua mtu mwingine kusimamia Sekta ya Madini kwa wakati huu hadi pale mambo yatakapowekwa sawa vya kutosha kuweza kuaminiwa mtu mwingine. Tayari wizara hii imehangaika na watu wengi sana huko nyuma na kuendelea kumpa mtu mwingine basi itakuwa ni kuanza kutengeneza bangusilo mwingine huko mbeleni.
Ni kwa sababu hiyo naamini Wizara ya Madini ibakie kama majukumu ya Rais mwenyewe; yaani Magufuli mwenyewe achukue dhamana ya Sekta ya Madini hadi atakapojiridhisha kuwa mifumo, na misingi mizuri ya kusimamia sekta hii imewekwa. Hivyo, napendekeza amteue Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Madini) ambaye ndiye atakuwa msaidizi wake mkubwa wa kusimamia Wizara ya Madini hadi pale atakapoona ni vyema airudishe nje ya Ikulu.
Uamuzi huu unaweza kufanyika hata kwa mwaka mzima au kwa muda wote uliobakia wa awamu hii ya Magufuli. Uzuri wa kufanya hivi, ni kuwa utaondoa ulazima wa Marais kuwatoa makafara mawaziri lakini pia mawaziri kuona kuwa labda wameonewa. Lakini zaidi pia utampa nafasi Rais mwenyewe kuhusika moja kwa moja na hivyo kuweza kujua kwa ukaribu kinachoendeoea na kuchukua hatua mara moja. Wawezekaji na wafanyabiashara wa sekta hii watakuwa na ujasiri wa pekee wa kwenda kujaribu kutoa kitu kidogo Ikulu ili mambo yao yaende na kwa wale tunaomjua Magufuli kuna watu wanaweza wakageuza toka Ikulu wakiwa na pingu!
Kama Rais mwenyewe alivyosema hili ni jambo zito basi ni vizuri alipe uzito unaostahili. Haifai kabisa kumpa mtu mwingine kwa sasa eneo hili.
Sioni namna nyingine ya kuunda upya eneo hili zaidi ya hii.