Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 18,052
- 25,098
1. Hiyo ya Miongozo ya Chuo hatupingi, ndiyo maana kuna vyuo vyenye ubora ambavyo mingozo yao ni thabidi na viongozi kama UDOM ambao miongozo yao ni kama hivyo.Kutegemea na miongozo ya chuo, kuna aina tatu ambazo wanawapa phd. Wanaweza kupata kwa kuandika monograph, publishable manuscript, na published manuscript thesis. Sasa kama ametumia monograph anaweza kuwa amefanikiwa. Pia kama ni published manuscript thesis anaweza kufanikiwa pia ka paper zake amepeleka kwa open access journals zinazolipiwa kuanzia dol elfu mbili. Hawa wanafanya kazi kwa haraka na wanatools nyingi za kumsaidia mwandishi/mtafiti.
Najaribu kutafuta wema katika utaratibu huu wasasa.
2. Elewa kua thesis nyingi huishia kuwa Monograph pia. Academic monographs zote hupitia peer review process kabla ya kuwa published. In fact hata Ph.D zinazotolewa kwa watunzi wa muziki pia hupitia peer review process. Ninajua kuwa Marehemu Dr Mgandu alichelewa sana kupata Ph.D yake kwa sababu ya peer-review ya tungo zake ilichukua muda mrefu, na tungo kadhaa zilikataliwa hata kama zilikuwa nzuri masikioni mwa wasikilizaji, ikabidi aongeze tungo nyingine zinazokidhi vigezo.
3. Kama amepeleka kwenye open access journals ambazo unalipia na kuwa published kesho yake, halafu chuo kikakubali, inabidi turudi kwenye item ya kwanza hapo juu kwa sababu credibility ya publisher huangaliwa sana (impact factor, peer review process, editorial board na vitu kama hivyo). Hiyo ya UDOM kupublish kwenye journals za vitivyo vyao ambapo wao wenyewe ndio ma-reviewer ndio upuuzi wenyewe huo.