Bawabu wa pili
Senior Member
- Nov 14, 2025
- 147
- 432
Binti aliyejulikana kwa jina la Tatu Mgeta (23), mwanafunzi wa Chuo cha Tabora Polytechnic College, amefariki dunia huku dereva wa bodaboda akijeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea wakati walipokuwa wamepakizana kuelekea chuoni,kugongana na treni ya abiria iliyokuwa ikitokea mkoani Tabora kuelekea mkoani Katavi.
Tukio hilo limetokea katika maungio ya reli yaliyopo Kata ya Isevya, Manispaa ya Tabora, Januari 20, 2025.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Maganga Peter na Abdallah Ismail, ajali hiyo ilitokana na bodaboda kushindwa kuzingatia sheria za barabarani, ikiwemo ishara ya bendera ya muongoza treni pamoja na honi iliyotolewa kwenye makutano hayo.
Mashuhuda hao pia wameiomba Serikali kuweka kingo na alama za tahadhari katika maungio hayo ya reli, ili kuwasaidia watumiaji wa barabara kutambua uwepo wa treni.
Wamesema changamoto hiyo inatokana na baadhi ya watumiaji wa barabara kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu alama za barabarani, pamoja na baadhi ya wengine kuzipuuzia.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Afisa Utawala wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora, Afisa Mnadhimu Omary Simba, amesema majeruhi mmoja ameelekwa hospitali kwa matibabu huku akibainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa bodaboda kwa kutokuzingatia sheria za barabarani.