Tabora Badilikeni nyie wanyamwezi

Tabora Badilikeni nyie wanyamwezi

kwa hakika wanatabora wote wanaopenda maendeleo hawana budi kurudi na kusaidia ndugu zao katika ukombozi, ukiachilia sifa ya upole, ki ukweli watu wa tabora ni wapiga majungu, wanafiki na rahisi sana kurubuniwa kwa vitu vidogo vidogo, nahitaji uamsho hao, kukaa kwa mwarabu hapo inaweza kuwa chanzo pia ingawa utafiti wa kina unahitajika
 
yaani wanyamwezi mnashindwa hata kuiga ndugu zenu wasukuma, hata kabla ya cdm walikuwa wanakufa na cheyo wao (bwana mapesa), hivi katika mikoa yote ya tanzania yenye historia kubwa, nyie ccm imewafanyia nini cha maana, anzeni kujitambua kuwa hata ccm yenyewe inawaona mazuzu tu
 
Jamani msitulaumu tu moja kwa moja wanyamwezi bila kuangalia mambo yenyewe kwa undani.Haya leo kweli mkoa mzima wabunge ni wa CCM hebu niambieni ni chama gani cha upinzani kiliweka mikakati ya dhati kutaka kuchugua jimbo lolote tabora?Chadema iliwetenga fedha kiasi gani kufanya kampeni tabora 2010?(Tena kuna majimbo mengine ya Tabora hata hawakuweka wagombea kabisa).CUF ilifanya nini katika kuhimiza watu wawachague 2010?Huu mkoa wetu ni kama watanzania wote mmetuzila kuanzia CCM mpaka vyama vya upinzani!Mliona wenyewe mambo yalivyokwenda Igunga pale CDM ilipoamua kugombea kwa dhati,je kwa kampeni ya namna ile kweli Tabora mjini mbunge wake angekuwa ni yule ponjoro?Wanyamwezi ni kweli tuna matatizo yetu hilo sikatai lakini kiukweli hata upinzani hawapo serious na mkoa wetu kwa ujumla!Mnasema Tabora kuna vijiwe vya kahawa na majungu,uvivu kwa sana sawa ni kweli nakubali lakini je mmefika Lindi na Kigoma?Mbona wanasifa hizo pia mlizozisema lakini wanawabunge waupinzani kwenye mikoa yao?MWISHO KABISA:Naomba kutoa Rai kwa vyama vya upinzani hasa CDM na CUF hebu viweke malengo ya kweli kuutwaa mkoa wa Tabora then tuone kama kweli sisi wanyamwezi tunayakataa mabadiliko!!
 
Wana JF na Wanyamwezi wenzangu popote pale mlipo.

Kumekuwa na lawama nyingi sana kwetu sisi Wanyamwezi na haswa Wadakama wa Mkoa wa Tabora kuwa tumekuwa kichaka cha CCM kuja kujificha. Sisi tumekuwa ndiyo kimbilio la CCM kuja kupata kura za bure na kuchakachua matokeo. Sisi ndiyo tumeonakana kuwa tumekuwa Muhuli wa kuiingiza CCM madarakani na Rais wake kumuweka Ikulu.

Nakumbuka kusoma makala za wana JF kadhaa zikihimiza vyama vya upinzani kuhamia Tabora mara kwa mara na kutoa shule/somo la Utaifa au Uraia. Ombi hili lilikuwa likikubaliwa ila kutekelezwa imekuwa ni shida. Labda kwa sababu gharama ni kubwa, sijui maana mie sipo ndani ya chama.

Kwa mfano tuangalie uchaguzi wa mwaka 2010, nilisubiri sana kuona Dr. Slaa akienda Sikonge kuwaona Wanyamwezi wa huko. Nikashangaa kumuona Kikwete tu na huku ikiwa mara yake ya ngapi sijui kufika huko. Tabora umeme wenyewe wa shida na hivyo mawasiliano inakuwa ngumu. Pia media nyingi za Tanzania tunajua jinsi wanavyotangaza kile kinachotakiwa kusikilizwa na Watu wa Chama na Serikali ya CCM.

Tuangalia matokeo ya Uchaguzi mdogo wa Nzega wa mwaka jana na mwaka 2010 mtagundua kuwa kuna tofauti kubwa sana. Rostam Azziz alikuwa kama Mungu huko Igunga ila Chadema walipoenda huko na kujikita kisawasawa, basi mambo yamebadilika kabisa. Nafikiri mmeona jinsi Igunga ilivyopata Mwamko ghafla na kuwa sasa moja ya ngome imara ya Chadema ingawa uchaguzi Chadema ilishindwa kwa kuchakachuliwa.

Si kweli kuwa ni Wanyamwezi tu ndiyo wajinga kiasi hicho. Ukiangalia hata uchaguzi wa Arumeru ambako watu wamepata somo la Uraia kwa siku nyingi, wameona kwenye TV na kusikia kwenye Radio na uzuri wa wenzetu wa huko hata kipato chao kipo juu zaidi na Mwamko wa Kisiasa na maisha yapo juu zaidi, bado watu zaidi ya 26,000 wameichagua CCM. Watu pamoja na ugumu wa maisha na kuonyeshwa kabisa mbaya wao ni nani na kushuhudia matusi ya akina Mkapa, Lusinde nk lakini bado 26,000 wamekichagua CCM.

Sasa mnategemea nini kwa watu wa kijiji changu nilipozaliwa cha Mkolye (katikati ya Tutuo na Sikonge) wamchague Slaa ambaye hawajawahi hata kumuona zaidi ya kumsikia? Wanamsikia tu Zitto Kabwe, Sugu, Mnyika, Lema nk. Kwao wao, ni heri wamchague Kikwete na CCM yake maana mara moja moja wanakuja na Magari yao makubwa mazuri, wamependeza na kunawiri. Wanatuahidi na sisi tunaweza kupendeza tukiwachagua na kwa sababu kila mtu anapenda KUOTA ndoto za alinacha, basi walau tunakuwa tumeshaona kuwa ukiota basi ota na wewe umekuwa Dereva wa gari zuri la Kikwete au hata Tarishi ofisini na kwenye msafara maana upo ndani ya suti nzito.

Lawama nyingine kwa upande fulani ntaomba tuzielekeze kwa Chama cha Chadema na upinzani kwa ujumla kwa kuiacha Tabora na Wanyamwezi kama Mwana mpotevu. Kama kweli Chadema inajiandaa kuchukua nchi, basi labda niseme tu jambo moja fupi na muhimu sana:

Wanyamwezi ni kama Maharage ya Mbeya. Si wagumu kiasi hicho kubadilishwa. Ukiwaweka sana na kuwaonyesha jinsi wanavyoibiwa na KULIWA SANA wakati wao wakila kidogo au kutokula kabisa, basi watabadilika. Ningelisisitiza Chadema wahahamishe kambi walau kwa wiki mbili mkoani Tabora na kushusha shule ya kufa mtu wakati wa kiangazi ukifika. Uzuri ni kuwa kidogokidogo, watu wameanza kuamka na kudai haki zai ila woga bado ni mkubwa sana. Serikali za mitaa na vijiji zina nguvu sana na vitisho kwa mtu yeyote aliye nje ya CCM. Na mbaya zaidi ni pale unapohamia UPINZANI, hapo unakuwa umejipalia moto.

Kama mnavyozunguka mara kwa mara, Arusha, Mbeya, Mwanza, Moshi nk basi mjitahidi na Tabora muwe mnafika mara moja moja. Nina imani kabisa kwa wimbi la mabadiliko linaloendelea sasa, mgomo wa Madaktari, huduma mbaya za afya na maendeleo zinazochangiwa na ukosefu wa fedha serikalini, Chadema ni mtaji mkubwa kabisa wa kuwaambia Wanyamwezi mambo haswa yalivyo na kuwakumbusha kuwa wanaibiwa na wabadilike.

Hebu fikiri ni mikutano mingapi ya hadhara imeshafanyika huko Tabora tangu uchaguzi ufanyike. Ukiacha Igunga ambapo kambi ya Chadema ilihamia, sijawasikia wakija na lile gari lao la kuhutubia mkoani Tabora na kuzungukia walau TARAFA zote za Tabora.

Nafikiri sababu nyingine kwa nini vyama vya upinzani havijali sana Tabora ni idadi ndogo ya watu. Wilaya mbili kubwa za Arusha, zinaweza kuwa na watu wengi zaidi ya Tabora kwa ujumla. Sasa hapo linakuja swali, je kuna haja ya kupoteza muda huko? Kwa kura za Rais, ndiyo hakuna haja ila kwa Wabunge, ni kuwa Chadema inapoteza sana.

Kutokana na idadi kubwa ya Waislaam, CUF ndiyo ilikuwa na uwezo mkubwa sana kushinda Tabora ila CUF ni chama ambacho wenye nacho wameamua kuhakikisha kinakufa taratibu na kuzikwa na ndiyo maana sijakitaja hapo juu na kuachia tegemeo kubwa kwa CHADEMA.

Tafadhali tafadhali uongozi wa Chadema, nendeni Tabora na mkashushe somo la Uraia sasa. Watanzania wanazidi kuamka na si kweli kuwa Wanyamwezi wote wamelala. Mkijipanga vizuri, Mwaka 2015, Chadema inaweza kusinda uchaguzi wa Rais na Bunge. Zimebaki miaka 3 ikiwa na maana muda hautoshi. Fanyeji juhudi kwa kutafuta watu mapema kujenga vyama huko Tabora na mwaka 2015 kuwasimamisha kama Wagombea Udiwani na Ubunge wa Majimbo yote ya Tabora.

CCM ni chama kizuri sana ila kimepotea njia. Inabidi mtu akisimamishe, kirudi sehemu kilipoanza kupotea na akirudishe kwenye njia sahihi. Kitapendeza sana kikiwa chama cha upinzani na nina imani ndipo wengi wataona haswa uwezo wa chama cha CCM. Ila kwa leo, hiki chama kimekuwa mbali kabisa na dira ya Nyerere.

Mwisho niseme kuwa MSITUTUKANE WANYAMWEZI kwa kutufunga wote kwenye pakacha moja. Tabora ni zaidi ya Wanyamwezi. Kuna wanyamwezi tumebadilika zaidi ya wale Wameru 26,000 na kuna Wameru wamebadilika zaidi ya Wanyamwezi wanaoichagua CCM. Hata kama ntakuwa Mnyamwezi pekee wa Mkolye ninayechagua mabadiliko, ukitutukana Wanyamwezi, basi utakuwa unafanya makosa. Nafikiri neno zuri la kutumia ni WANA TABORA BADILIKENI maana Tanzania haina mipaka ya ndani na kuna makabila kibao yanaishi Tabora.
 
Tabora maendeleo duni, barabara mbovu, maji mtihani, elimu imekufa, nyie wanyamwezi nani amewaroga? Yani CCM imewaroga kabisa. Ebu upeni heshima mkoa wa Tabora mbele ya watanzania wenzenu. Yani CCM wamewasusa kimaendeleo nyie mnajipendekeza, Shame on you Nyamwezi people.


Copy that!
Mama yangu leo ameshangilia sana Ushindi wa Joshua, na alipiga makofi sana, too bad hakuna technolojia yet ya kuyaingiza kwenye TV Pronto, otherwise mngeyasikia; and she is woman who is 67yrs old.
We are coming, kama alivyoshauri kaka hapo juu, nendeni Tabora mkahamasishe; ni kukata tamaa tu si kingine kinachowasumbua wanyamwezi na watanzania wengi.
 
Copy that!
Mama yangu leo ameshangilia sana Ushindi wa Joshua, na alipiga makofi sana, too bad hakuna technolojia yet ya kuyaingiza kwenye TV Pronto, otherwise mngeyasikia; and she is woman who is 67yrs old.
We are coming, kama alivyoshauri kaka hapo juu, nendeni Tabora mkahamasishe; ni kukata tamaa tu si kingine kinachowasumbua wanyamwezi na watanzania wengi.

kazi ngumu mpe mnyamwezi wamezoa hao any way prof lipumba ,sita ,kapuya mmmmmhhawa vip michango yaoo?
 
kazi ngumu mpe mnyamwezi wamezoa hao any way prof lipumba ,sita ,kapuya mmmmmhhawa vip michango yaoo?

I have reservation kwa hao watu; they are more waswahili kuliko wanyamwezi. Na katika kabila ambalo halina ukabila, nafikiri tunaongoza. Yaani kama ni graph tungekuwa kwenye negativu ya X axis. Tumerundikana kumpwani (Dar, Tanga na Zanzibar); mimi sijajenga Tabora though nimejenga Dar, na ni wengi kama mimi. Kinywamwezi nikiongeacho ni cha kuombea maji tu.

Now about Kapuya, yule ni muha zaidi kuliko mnyamwezi; na sidhani kama ana uchungu whatsoever wa Tabora, Sitta ambacho ameona ni muhimu kwa wanyamwezi ni ofisi ya Spika tu, Lipumba ni mswahili kuliko mnyamwezi.

Ni maoni yangu tu
 
Kaunga ni kweli kabisa maneno yako.

Miaka ya zamani, ilikuwa huwezi kwenda kujenga nyumba nzuri kwenu labda familia yenu ipo imara sana na hamuogopi kulogwa. Wengi waliofanikiwa walikuwa ni wale ambao wanatoka kwenye familia ya wasomi wengi kama Yongolo huko Chabutwa, Kapya hapo Sikonge na wengine kadhaa.

Nilishashuhudia Mnyamwezi mmoja kaweka jengo lake zito Morogoro na akakiri kabisa kuwa hata nusu ya hilo jengo angelijenga nyumbani, basi au wazazi wake wangelikuwa matatizoni au yeye mwenyewe. Uzuri wa familia kubwa ilikuwa kwamba huwezi kujua umloge nani maana wengi wana pesa.

Wanyamwezi wengi walihama kabisa na hata sisi wenyewe ilikuwa tumuhamishe Baba kutoka Mkolye na ahamie Dar es salaam na nyumba ikajengwa ingawa hakufanikiwa kuhamia na akawa ametangulia mbele ya haki.

Nasikia kwa sasa hali imebadilika sana. Nyumbani mie nina siku nyingi sana sijafika na hivyo husikia tu habari za huko. Naambiwa sasa kuna Umeme. Kuna Mnyamwezi kaweka ghorofa lake zito sana kuwafunika hadi Waarabu wa hapo. Kuna Mahoteli, nyumba za kulala wageni etc. Hii inanipa picha kuwa vile vizee vichawi vimeisha na vinaendelea kuisha na hivyo watu uoga sasa umeisha na taratibu wanaanza kurudi nyumbani.

Pana wakati niliongea na kijana mmoja na akaniambia Prof. Kayumbo alikuwa mbioni na yeye kuja kijijini Mkolye kujenga maana hapo ndipo akina Kayumbo wanaishi. Na akaniambia na mtoto wake alikuwa kapewa kiwanja hapo ingawa anaishi nje ya Tanzania. Sijui iliishia wapi ila wengi wameanza kurudi taratibu.

Mie mwenyewe na ndugu zangu tumeamua kuirudisha nyumba ya Marehemu baba. Tunajipanga ili ule mji urudi kama ulivyokuwa na ikibidi zaidi ya ulivyokuwa. Ilikuwa dhambi kubwa sana kuhama pale na hasa ukichukulia kijiji hiki kilianzishwa na Marehemu Babu yetu Sambali na makaburi ya Wanangwa wote hadi leo yapo na tunayatunza. Sasa tukihama, nani ayajali? Mwee, hizi nyingine tulikuwa tunajipapalia tu vilaana visivyo na ulazima wowote.

Taratibu tu na sisi tutakuja juu. Uzeeni lazima nikazeekee zaidi Mkolye.
 
sikonge upo wapi ndugu yangu?
wanyamwezi...wagogo,warangi,wanyiramba,wamakonde,wasambaa na waluguru baragumu limepigwa AMKENI

Hayo makabila hapo wamesha jichokea wakipewa ubwabwa hao kula zote unachukua
 
Yote yameongelewa lakini hakuna hata mmoja aliekwenda kwenye mzizi wa matatizo ya Mji wa Tabora kwani ukiangalia mkoa mzima toka mkoloni mpaka leo hakuna MBUNGE au MKUU wa WILAYA au MKOA labda gama peke yake ndiye aliyeweza kuacha LEGACY mkoani kuonyesha uzalendo na mapenzi yake kwa MKOA huu,
 
Nikumbusheni, ni mpiganaji gani kutoka chama pinzani aligombea ubunge wa tbr mjini?
Njooni wagombea serious mnaojua jenga hoja, hasa wasomi, nauhakika hamtopata kura! Watu wamechoka huku!!
 
Buhange nakupongeza kwa juhudi zenu,ss huku tulipo tunawapa big up!!!lakini kata Imalamakoye bado inashikiliwa na CCM kupitia bw.Gembe,ambayo iligawanywa na kuzaa kata nyingine ya Nsenda ambayo inashikiliwa na CUF siyo CHADEMA,hata hivyo bado tuna mtaji mkubwa kwenye kata nyingi za jimbo!!!
 
shida ya unyamwezin(sio ulaya)i ni udini ndio maana kile chama chetu chap prof kina nguvu


Mkuu Inkoskaz acha kuongea kwa fikra naomba uweke facts mbele,mbona kwa historia wabunge wengi waliowahi kuwepo pale tabora mjini ni Wakristo?Mkiuweka udini mbele sidhani kama mnajenga picha nzuri mbele ya jamii ya watanzania ya sasa na ijayo!Prof Lipumba ni mnyamwezi na hicho ndiyo kinachowapa umaarufu tabora kama unabisha leo hii ahame chama au aachane na siasa utaona kama CUF itaendelea kuwepo tabora!Sina takwimu sahihi lakini siamini kama Tabora ni mji wenye waislamu wengi kupita wakristo kwasasa!

Halafu kusema hivyo mnazidi pandikiza chuki za kidini kwenye jamii na hilo litachelewesha maendeleo ya kweli tunayoyalilia wananchi pia mnakipunguzia kasi chama chenu cha CDM maana kitaonekana ni chama kisichokubalika kwenye waislamu wengi kitu ambacho si kweli maana kigoma kaskazini mbunge wake ni wa CDM lakini kuna waislamu wengi,hivyo hivyo kwa mh Mustafa Akonaay na kwa mh Arfi.
 
Mkuu Inkoskaz acha kuongea kwa fikra naomba uweke facts mbele,mbona kwa historia wabunge wengi waliowahi kuwepo pale tabora mjini ni Wakristo?Mkiuweka udini mbele sidhani kama mnajenga picha nzuri mbele ya jamii ya watanzania ya sasa na ijayo!Prof Lipumba ni mnyamwezi na hicho ndiyo kinachowapa umaarufu tabora kama unabisha leo hii ahame chama au aachane na siasa utaona kama CUF itaendelea kuwepo tabora!Sina takwimu sahihi lakini siamini kama Tabora ni mji wenye waislamu wengi kupita wakristo kwasasa!

Halafu kusema hivyo mnazidi pandikiza chuki za kidini kwenye jamii na hilo litachelewesha maendeleo ya kweli tunayoyalilia wananchi pia mnakipunguzia kasi chama chenu cha CDM maana kitaonekana ni chama kisichokubalika kwenye waislamu wengi kitu ambacho si kweli maana kigoma kaskazini mbunge wake ni wa CDM lakini kuna waislamu wengi,hivyo hivyo kwa mh Mustafa Akonaay na kwa mh Arfi.

Chuki za kidini wapi wewe mkuu? Mtu akisema ukweli eti anapandikiza chuki za kidini. Tabora bado itachukua miongo kadhaa kubadirika; uswahili, uvivu, mwamko wa elimu mdogo, majungu na kukumbatia magamba! Miaka 50 ya uhuru, wilaya zote za Tbr (Nzega, Urambo, Sikonge, Uyui na Igunga) kuunganisha na makao makuu ya mkoa (Tabora) ni vumbi tupu! Badirikeni Wanyamwezi.
 
Back
Top Bottom