Table manners

Huu uzi nimeufurahia sana na nampongeza mleta mada maana utatusaidia kujua pia tamaduni za wenzetu na ikiwezekana kupractise kabisa ingawa sio lazima. Kwa wale ambao hawajapendezwa na hii mada sio lazima sana mtokwe mapovu na kupinga, vingine viangalie tu kama hakikuhusu pita tafuta kinachokuhusu mtawafanya watu wawe waoga kila anapotaka kuleta jambo la maana. Kuna watu wanasomea maswala ya mahusiano ya kimataifa ambapo pamoja na mambo mengine hili pia wanahitaji kulifahamu na la muhimu kwao kujua tamaduni za wengine. Unasoma au kama umeshamaliza umesoma kwa kutumia lugha ya kiingereza ambayo siyo yetu waafrika hasa watanzania, kwa nini hukupinga au kuacha shule? sio kila kitu lazima kikuhusu au uchangie.
 
Dah...tunalewa vibaya hivi?? Vile vijiti viko wapi hapa? Au havitumiki? Tuache ujinga bana.. mbona juzi tu hapa tumeenda kwa shangazi faizafoxy katupa pilau mkekani tukalipiga kwa mikono tukaenjoy vizuri tu bana..
 
ila mama mimi nadhani kula na umma sio utaratibu wa huku nyumbani afrika sisi tulishazoeshwa kula na mkono na kwa upande wangu sijawahi kabisa kula kwa kutumia kisu.
 
Nakumbaka tulikaribishwa dinner nyumba flan hivi, wenyeji walikuwa wanaishi kizungu ila ni wabongo, mda wa msosi tukaanza wageni ....' Baada ya kuweka msosi wenye mboga saba bonge la mlima chura haruki....' Kufika kwenye vitendea kazi (kisu na uma).....' Wageni wote sita tuliishia kuchukua uma tu tena kwa shingo upande sababu chepe haikuwepo (kijiko)... Aiseee baada ya wenyeji kuchukua msosi kiasi wakadaka umma na kisu wakaànza kutumia kwa ufundi na kitable manner zaidi..: Ila nashukuru tulianza wageni ..maana wangeanza wenyeji kama unavyotujua wabongo tungecopy na kupaste hapo sasa tungeumbuka mezani ..' Mara kisu kidongoke...Mara kisu kigandane na umaa ..Mara umwagemwage menu
 
Mweeh mambo ya uma na kisu yalishaga nishinda mie full kutumia mikono
 
Asante kwa Elimu. Ila hii imekaa kikike zaidi, hii nafikiri inawafaa zaidi wanaume wa Dar. Kwa sisi wa mikoani haya ni maigizo, kwa style hii hata mke itakulazimu kumshughulikia kwa utaratibu huu na matokeo yake ni kupigiwa. Sipingani na mpangilio huo ila upo ktk familia chache sana hasa ukizingatia maisha ya Watanzania wengi kuwa pangupakavu.
 
Hapo kwenye umma na kisu ndipo patamu!!!

Haya madini wanawake wengi mjini hawayajui, kwanza kupika tu ni mziki sasa unatarajia haya atayajua??
wasiopika ndiyo wanaojua hayo mambo,.. muda mwingi appointment zinakua za hotel
 
hivi hizi taratibu aliweka nani?
binafsi nimefeli hili somo..
 


Cha kukumbuka pia unapomaliza kula hakikisha kiti unakirudisha mahala pake yaani pale ulipokitoa ukitaka kukaa
 
Mara viparticles vya chakula vinakurukia kwenye sahani😀😀
 
ha ha hahaha
 
Ni akiba ya maneno tu mkuu. Nilikwenda kusuka mitaa flani dar, nilikaa kwa msusi siku nzima, basi lunch wakaniuliza tukuletee chakula gani, kulikuwa na muuza chips pembeni, nikaagiza zege na mishikaki, basi sahani imeletwa na toothpick, nikauliza hakuna umma, nikaambiwa umma ni mmoja na ni kitendea kazi cha kukorogea mayai, nikipewa inamaana kazi itasimama. Niliienjoy kula zege kwa toothpick.
 
vizuri
na ni vyema wamama wakawafunza watoto wao haya mambo mapema sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…