Tabia za wanadamu mfanano na wanyama zenye kuua kikundi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,867
Wallah nakuapia kila mmoja wetu hapa hakosi tabia yake....!!!!

Haaa haaa n hatar hapa kuna baadh ya watu panatugusa inachekesha kisha inareflect ukiisoma

*Bata:* Kujivuta vuta, kufanya kazi polepole na kuendekeza uvivu mpaka mambo ya kikundi yanazorota au kufa kabisa.

*Bundi:* Mtu anayefikiria ana akili kuliko wote kwenye kikundi- hutumia lugha ngumu kueleweka

*Chura:* Rudia rudia kitu kile kile mpaka anawachosha wenzake kundini

*Kenge:* Hatumii akili sawasawa, ujinga mwingi na kufanya maamuzi ya ovyo yenye kuwakatisha tamaa wenzake

*Kiboko:* Kulala lala na kupiga miayo, wakati wenzake wanachacharika, yeye ni kukaa tu hafanyi kazi.

*Kifaru:* Yeye hushambulia wengine kwenye kikundi bila sababu

*Kinyonga:* Kigeugeu, akiwa kwa mwanakikundi huyu anasema hili na akiwa kwa mwingine anasema tofauti

*Kobe:* Hujitoa akiudhiwa, hana uvumilivu kwenye changamoto zinazoikabili kikundi.

*Kuku:* Kuvuruga palipotengenezwa, kwenda tofauti na maono ya kikundi kwa kujali na kuzingatia mambo ya muda mfupi tu.

*Mbuni:* Huficha kichwa na hufikiri hakuna shida kwenye kikundi hata kama zipo shida nyingi

*Nyati:* Kujihami tu kwa sababu ya woga, hakosolewi, ukimgusa tu anaazisha vita vya maneno au kupigana

*Nyoka:* Anajificha huku akiuma bila kusema. Mchonganishi

*Nyumbu:* Woga na kutotumia akili kabisa.

*Paka:* Yeye anataka ahurumiwe tu na wenzake, hana mchango wowote kwenye kikundi.

*Panya:* Hachangii chochote yeye hujificha tu na kujitokeza wakati wa neema.

*Popo:* Hana msimamo, Kwa wanaokubali hoja yupo na kwa wanaopinga hoja yupo. Haeleweki.

*Punda:* Wagumu kubadilika hata umuelimishe kwa namna gani misimamo yake ni yale yale ya zamani.

*Samaki:* Hachangii hajibu, kazi kuteleza, kukwepa na kutoweka tu na huonekana hali ikitulia na kuwa shwari.

*Simba:* Hupigana kama hakubaliwi mawazo yake na wanakikundi.

*Sungura:* Hukimbia kama kuna dalili za hatari na kwenda kinyume na makubaliano ya kikundi

*Tausi:* Yeye huringisha na mambo mazuri aliyonayo ambayo wanakikundi wenzake hawana.

*Tembo:* Hufunga njia bila sababu watu wasipite. Huzuia mawazo, maamuzi ya kikundi yasifanikiwe bila sababu.

*Tumbili:* Mizaha mizaha tu wakati wote hayuko makini hata kwa mambo muhimu ya kikundi.

ukiweza mtaje mwenye tabia mojawapo kati ya hizo... Mtaje unayemmudu yasije kuwa mengine
 
Hapo kwa "nyati" mpaka liwekwe sanduku la maoni ndipo niwe huru kuandika jina kubwa la mhusika, ili niweze kuwa salama, kidogo. Najua hata wewe unaye pita hapa umeishalijua, ole wako ulitamke.
 
Hapo kwa "nyati" mpaka liwekwe sanduku la maoni ndipo niwe huru kuandika jina kubwa la mhusika, ili niweze kuwa salama, kidogo. Najua hata wewe unaye pita hapa umeishalijua, ole wako ulitamke.
*Nyati:* Kujihami tu kwa sababu ya woga, hakosolewi, ukimgusa tu anaazisha vita vya maneno au kupigana
 
Kimada ni nyati ila anafikiri yeye ni simba

Salamu zimfikie genitaminini popote alipo
Hapo kwa "nyati" mpaka liwekwe sanduku la maoni ndipo niwe huru kuandika jina kubwa la mhusika, ili niweze kuwa salama, kidogo. Najua hata wewe unaye pita hapa umeishalijua, ole wako ulitamke.
 
Back
Top Bottom