Tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo

Tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo

mtvbase

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2014
Posts
1,243
Reaction score
563
Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya nimegundua kwamba tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo upende usipende.kwahiyo kama una mpango wa kuoa usiishie kumchunguza mchumba wa kike ambaye wakati wa uchumba anakuwa anaishi maisha ya kuigiza bali pia angaika kumchunguza mama mkwe.
kwanini mama mkwe?
1. Mama mkwe ndie aliyemlea mkeo mtarajiwa kwahiyo mchumba wako atakuwa ameiga na kufundishwa kuwa na tabia kama mama yake
2.Mara mwanamke anapoolewa Mshauri mkuu ni mama yake mzazi(napenda uamini hili) kwahiyo maisha yake kwenye ndoa yatategemea ushauri wa mamaye
3.ikitokea mfarakano kwenye ndoa na kama mwanamke ndio tatizo mama mkwe ndie mtu pekee anayeweza kumbadilisha mkeo katika njia sahihi.

N.b mbasha kama angekuwa makini kumchunguza mama mkwe haya yote yanayomtokea asingeshangaa
 
Sasa sio wanawake wote waliolelewa na mama zao!!


Halafu jamani kosa kubwa kwenye ndoa ni usaliti,, hatuna uhakika kama kweli mr. Alibaka au hakubaka.
Mi nadhani tusihukumu, bali tuiombee hii ndoa,,,mungu awarejeshee amani na watubu kwa wakati wao.
 
Mbona mademu wa siku izi wanadai ranger rover wakati dingi yake hana hata baiskeli?
 
Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya nimegundua kwamba tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo upende usipende.kwahiyo kama una mpango wa kuoa usiishie kumchunguza mchumba wa kike ambaye wakati wa uchumba anakuwa anaishi maisha ya kuigiza bali pia angaika kumchunguza mama mkwe.
kwanini mama mkwe?
1. Mama mkwe ndie aliyemlea mkeo mtarajiwa kwahiyo mchumba wako atakuwa ameiga na kufundishwa kuwa na tabia kama mama yake
2.Mara mwanamke anapoolewa Mshauri mkuu ni mama yake mzazi(napenda uamini hili) kwahiyo maisha yake kwenye ndoa yatategemea ushauri wa mamaye
3.ikitokea mfarakano kwenye ndoa na kama mwanamke ndio tatizo mama mkwe ndie mtu pekee anayeweza kumbadilisha mkeo katika njia sahihi.

N.b mbasha kama angekuwa makini kumchunguza mama mkwe haya yote yanayomtokea asingeshangaa

hiyo research umeifanya kwa wakwezo wangapi?
 
Naona utafiti wako umejikita katika malezi ya wazazi asa wa kike , swali ni vipi wale waliolelewa na baba au babu tabia zao zitakuwaje ? Si kila mke ulelewa na mama ake, take it from me.
 
Kwanza nikiri hili c jukwaa ninaloingiaga. Ila mleta mada yupo sahihi 99%. Mimi ni muhanga wa hii kitu. Mama mkwe wangu ameachika. Mimi nimemwacha mke wangu, naye ana dada zake wawili wote wameachika. Ukiangalia kwa karibu tabia zao zinafanana kabisa.

Yule mama amezaa na zaidi ya mwanaume mmoja. Tayari wale shemeji zangu wawili walioachika, mmoja mjamzito, mmoja tayari ana mtoto, na wote walipoachika tayari walikuwa na watoto kwenye ndoa zao za mwanzo. Mkuu mtvbase upo sahihi sana. Ahsante nitarudi kuona wengine wana maoni gani.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom