Tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo

mimi niliyelelewa na bibi inakuwaje maana mama mwenyewe nimekuja kuwa na nikiwa mkubwa sana

hizi tafiti zingine bhana hazina hata miguu
 
Ni kweli hata ukitaka kuoa angalia mama anafananaje kama mwili wake na sura yake viko fit so your wife atakuwa hivyohivyo.

Mkuu nadhani hapa umekosea kidogo watu wanatofautiana sana! mama anaweza kuwa na bint 6 asifanane na hata mmoja!!!! au akafanana ns mmoja!
 
Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya nimegundua kwamba tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo upende usipende.kwahiyo kama una mpango wa kuoa usiishie kumchunguza mchumba wa kike ambaye wakati wa uchumba anakuwa anaishi maisha ya kuigiza bali pia angaika kumchunguza mama mkwe.
kwanini mama mkwe?
1. Mama mkwe ndie aliyemlea mkeo mtarajiwa kwahiyo mchumba wako atakuwa ameiga na kufundishwa kuwa na tabia kama mama yake
2.Mara mwanamke anapoolewa Mshauri mkuu ni mama yake mzazi(napenda uamini hili) kwahiyo maisha yake kwenye ndoa yatategemea ushauri wa mamaye
3.ikitokea mfarakano kwenye ndoa na kama mwanamke ndio tatizo mama mkwe ndie mtu pekee anayeweza kumbadilisha mkeo katika njia sahihi.

N.b mbasha kama angekuwa makini kumchunguza mama mkwe haya yote yanayomtokea asingeshangaa
Elimu yako mkuu kabla ya kuukubali au kuukataaa utafiti wako
 
Kwa hiyo tabia ya baba mkwe ndo tabia ya mumeo... kama baba mkwe ni baka baka jua mume atabaka watu mtaoishi nao hadi mifugo mtayofuga?
 
maelezo yako yana usahihi sana siwezi kuyapinga hata kidogo.ukweli ni kwamba tabia za binti zinakuwa influenced sana na tabia za mama yake,mtoto wa kike tofauti na mtoto wa kiume,mtoto wa kike mara nyingi huambatana mama,lakini mtoto wa kiume hana muda wa kuambatana wazazi,mara nyingi yeye hujali michezo na wakati mwingine hata wakati wa kula yeye hajali,kama mama anaheshima kwa mumewe basi hata mwanawe atakuwa na heshima mumewe.pili kama alizalia nyumbani kabla ya kuolewa basi baadhi ya mabinti zake lazima watazalia nyumbani.lakini tatu kama mama aliolewa halafu akaachika basi hata binti zake(wanaweza wasio wote) lazima wataachika tu,lakini nne kama mama alikuwa mwaminifu katika masuala ya unyumba hata binti yake atakuwa mwaminifu,hata mumewe ampe majaribu.tano kama mama alikuwa anasauti kwa mumewe hata binti yake atataka kumpanda mumewe na kuwa na sauti ya mwisho ktk maamuzi ndani ya nyumba.sita (hili linatokea mara chache),kama mama alipata ujauzito wakati akiwa kwenye masomo,inaweza kutokea kwa binti yake
 
Sisi wamama ndio walezi wa jamii husika kwa asilimia 100%obviosly mama akiwa m"bovu basi family pia hua mbovu
 
maelezo yako yana usahihi sana siwezi kuyapinga hata kidogo.ukweli ni kwamba tabia za binti zinakuwa influenced sana na tabia za mama yake,mtoto wa kike tofauti na mtoto wa kiume,mtoto wa kike mara nyingi huambatana mama,lakini mtoto wa kiume hana muda wa kuambatana wazazi,mara nyingi yeye hujali michezo na wakati mwingine hata wakati wa kula yeye hajali,kama mama anaheshima kwa mumewe basi hata mwanawe atakuwa na heshima mumewe.pili kama alizalia nyumbani kabla ya kuolewa basi baadhi ya mabinti zake lazima watazalia nyumbani.lakini tatu kama mama aliolewa halafu akaachika basi hata binti zake(wanaweza wasio wote) lazima wataachika tu,lakini nne kama mama alikuwa mwaminifu katika masuala ya unyumba hata binti yake atakuwa mwaminifu,hata mumewe ampe majaribu.tano kama mama alikuwa anasauti kwa mumewe hata binti yake atataka kumpanda mumewe na kuwa na sauti ya mwisho ktk maamuzi ndani ya nyumba.sita (hili linatokea mara chache),kama mama alipata ujauzito wakati akiwa kwenye masomo,inaweza kutokea kwa binti yake

Nashukuru kwa kufafanua zaidi
 
Hii inaweza kua kweli,ila kwangu siyo kweli,
kuna mabinti wamelelewa na akina mama wanaojiheshimu ila wao ni tofauti kabisa,.
Kuna wengine mam zao ni micharuko ila ni wapole sana kutofautisha na mama.
Wapo watoto wa kike wengi tu wanaovutiwa zaidi na mienendo ya baba kuliko mama.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom