Tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo

Tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo

Atakuwa anamtoa out mara mojamoja na kuchunguza simu zake, kuongea na marafiki zake ikiwa ni pamoja na kumdadisi baba mkwe wake na ma x wake.

Mmmh jaribu uone kama itawezekana
 
Na ambao wameishi na baba zao tu inakuaje?au unamchunguza baba mkwe?
 
maelezo yako yana usahihi sana siwezi kuyapinga hata kidogo.ukweli ni kwamba tabia za binti zinakuwa influenced sana na tabia za mama yake,mtoto wa kike tofauti na mtoto wa kiume,mtoto wa kike mara nyingi huambatana mama,lakini mtoto wa kiume hana muda wa kuambatana wazazi,mara nyingi yeye hujali michezo na wakati mwingine hata wakati wa kula yeye hajali,kama mama anaheshima kwa mumewe basi hata mwanawe atakuwa na heshima mumewe.pili kama alizalia nyumbani kabla ya kuolewa basi baadhi ya mabinti zake lazima watazalia nyumbani.lakini tatu kama mama aliolewa halafu akaachika basi hata binti zake(wanaweza wasio wote) lazima wataachika tu,lakini nne kama mama alikuwa mwaminifu katika masuala ya unyumba hata binti yake atakuwa mwaminifu,hata mumewe ampe majaribu.tano kama mama alikuwa anasauti kwa mumewe hata binti yake atataka kumpanda mumewe na kuwa na sauti ya mwisho ktk maamuzi ndani ya nyumba.sita (hili linatokea mara chache),kama mama alipata ujauzito wakati akiwa kwenye masomo,inaweza kutokea kwa binti yake

chukua like mkuuuuu,
ni shahidi mkubwa juu ya ilo
 
Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya nimegundua kwamba tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo upende usipende.kwahiyo kama una mpango wa kuoa usiishie kumchunguza mchumba wa kike ambaye wakati wa uchumba anakuwa anaishi maisha ya kuigiza bali pia angaika kumchunguza mama mkwe.
kwanini mama mkwe?
1. Mama mkwe ndie aliyemlea mkeo mtarajiwa kwahiyo mchumba wako atakuwa ameiga na kufundishwa kuwa na tabia kama mama yake
2.Mara mwanamke anapoolewa Mshauri mkuu ni mama yake mzazi(napenda uamini hili) kwahiyo maisha yake kwenye ndoa yatategemea ushauri wa mamaye
3.ikitokea mfarakano kwenye ndoa na kama mwanamke ndio tatizo mama mkwe ndie mtu pekee anayeweza kumbadilisha mkeo katika njia sahihi.

N.b mbasha kama angekuwa makini kumchunguza mama mkwe haya yote yanayomtokea asingeshangaa

Wanaobisha sijui wanabisha nini wakati hii ipo tangu kale.ukipata mchumba watu wanachunguza mama zake na shangazi zake.tabia za hawa wawili ndo tabia za mkeo mtarajiwa.na kwa wanaume chunguza wajomba na madingi zake.hawa ndo huwa role models wa karibu zaidi.
 
Ah...sasa ukikomaa kujua tabia za mama njee si ndio utaambia una mmendea na kumtaka mama mkwe wako....?
 
Huwezi kuokota embe chini ya mchungwa afu ujilie tu bila kutilia shaka limetokea wapi....
 
Kwa hiyo tabia za baba mkwe ndio tabia za mumeo

Ukiona baba mkwe haeleweki

Nyumba harijojo

Cha pombe

Michepuko kedekede

Ujue hatari...
 
Back
Top Bottom