mapipando
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 2,922
- 3,563
1. Unalipa nauli lets say unatoa elfu moja, na nauli ni mia nne, konda anakuuliza wangapi? Kama ninao watu/ mtu wa kumlipia si ningesema mweneyewe!
2. Unatoa shilingi elfu kumi, konda anaanza kulalamika oo unatoa hela kubwa mara kimepanda kimeshuka na maneno machafu kibao. Mimi akiniuliza huna hela ndogo hapo mpaka utoe hii, namwambia ninayo nachukua elfu kumi yangu nampa mia, maana ndio hela ndogo niliyonayo, konda anaona anadharauliwa. Unanipangiaje pesa ya kutumia? Kama huna chenchi mimi inanihusu nini?
3. Unatoa nauli mathalani elfu 2, 5 au 10, konda hakupi chenchi anasubiria sijui usahau ili a-make super profit! Huwezi fanikiwa kwa kuiba vi elfu mbili mbili vya abiria.
Ongezea na wewe kero zako.