1.)Toyota Brevis - ai Series / Mark X
Madereva wa magari haya hujisikia very powerful and classic wawapo barabarani, hii inatokana na gari hizi kufungiwa engine kubwa mithili ya fuso ndogo na kuwa na muonekano ambao ni very commanding.
Wengi wao ni vijana wa kipato kizuri wenye kati ya miaka 25 - 40 hali inayosababisha gari hizi kuhusishwa na uporaji wa wake/ wapenzi wa watu, kiukweli kwa interior ya hizi gari ni ngumu kwa mtoto kuchomoa pindi aingiapo humo, akishakalia tu ile leather ni amekwisha.
View attachment 683387
2.) Toyota Altezza / Subaru Forester - Noisy Series
Asilimia kubwa ya madereva wa magari haya ni vijana wanyoa viduku wasio na staha barabarani; kwanza wanaweka milio mikubwa mno bila sababu za msingi na hupenda kuendesha kwa mihemko kutokana na kelele kubwa za magari hayo. Wengi huonyesha dalili za matatizo ya kisaikolojia, ambapo hu-compensate kushindwa kwao katika nyanja mbalimbali za maisha kwa ku-seek attention mabarabarani kwa kuendesha kwa fujo na makelele yasio na msingi.
View attachment 683389
3.) Toyota Harrier /Lexus - G Series
Kiwango cha juu cha madereva wa magari haya ni wanawake wa makamo wenye umri wa kati ya miaka 38 hadi 45; na nimebaini wengi wao hua ni wamehongwa hayo magari na waume zao ambao kimsingi ni wazee wenye miaka 50 kwenda juu. Madereva hawa huwa na mashauzi barabarani hasa wanapokutana na gari zenye caliber ndogo kama vitz na kujihisi wapo kwenye ndege, hii hujionyesha kwa tabia yao ya kupenda ligi za kijinga barabarani.
View attachment 683390
4.) Toyota Landcruiser - V8 series
Wengi wao ni madereva wa magari ya serikali au mashirika mbalimbali ya kimataifa. Wengi wao hujisahau na kufikiri kwamba muda wote wapo kwenye msafara wa kiongozi na hawapaswi kabisa kukaa foleni. Hutanua kwa fujo bila aib wala uoga, na matrafiki nao huyagwaya magari haya na huyaacha yatanue as if yapo kwenye msafara. Wengi wao hujihusisha na upigaji nyoka mafuta hasa yale yanayotumia diesel na kwenda kuyauza kwenye black market. Hulipwa vizuri japo wengi huwa hawatoboi kimaisha.
View attachment 683392
5.) Toyota IST, Vitz ect - Baby walker Series
Kigezo kikubwa cha watu kununua gari hizi ni ulaji mdogo wa mafuta, hivyo ni an inherent characteristic ya madereva wengi kama si wote wa IST/vitz like cars kuwa ni wabahili mno hasa wanapokuwa fuel station; ni kawaida sana kuwaona wakiweka hadi mafuta ya buku 5 kwa kujiamini kabisa.
Pia wana tatizo la kisaikolojia ambalo kitaalamu huitwa 'Inferiority complex', ni ile hali ya kujisikia unadharaulika hata kama hakuna aliekudharau, muda wote anahisi kama anapopita watu wanamnanga ..." check jamaa na kitoy chake...."
View attachment 683397
6.) Range Rover / Land rover - Discovery series
Nimebaini asilimia kubwa ya madereva wa magari haya ni wazungu wa balozi mbali mbali pamoja na waarabu koko waishio nchini; hupendelea sana kutumia njia kuu na kamwe hawapendi kutumia michepuko hata foleni iwe kali vipi. Pia hupendelea kuendesha mijini na high suburbs tu, as if waliambiwa wakipita Tandale wata tekwa flani hivi, it goes without say, huwa wanajihisi ni raia wa daraja la juu zaidi ya madereva wengine wawapo barabarani. Na tabia yao kubwa ni kuning'iniza suti kwenye seat ya nyuma, sijui maana yake nini, nisaidieni hapa.
View attachment 683406
7.) Toyota Tacoma / Tundra ect - Off road Series
Madereva hawa ni wale wapendao kutumia ile misemo ya " A real man uses three pedals" , na hata slogan za magari haya utakuta zinasema " Acar that understands men". So ni watu wenye tabia ambazo kwa lugha ya malkia tunawaita 'Chauvanists', yaani wanajifanya wa kiumeni zaidi, needless to say wana mifuko mirefu sana coz hizi gari ni very expensive but powerful and luxurious with very good looks!
View attachment 683546
8.) Toyota pick-up(1984 - 1992)
Mara nyingi madereva wa gari hizi ni wamama wazee wa Kichagga ambao wengi wana tabia za kupenda ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na kilimo cha migomba ya ndizi hasa pembezoni mwa jiji, hii hupelekea magari haya ambayo mengi ni makuu kuu kutumika kubebea majani ya ng'ombe na mbolea. Wamama hawa ni 'wagumu' na ni ma-fighters sana katika masuala ya kiuchumi, na mara nyingi ni wanene wanene hivi na huwa ndio tegemeo la familia.
View attachment 683592
9.) Toyota Noah - Family Series
Madereva wengi wa magari haya ni wababa wa nyumbani (Family guys) wenye familia za atleast watoto wawili na kuendelea. Watu hawa wana tabia za kuonyesha upendo kwa watoto na wake zao kwa kupenda sana kuwatoa outing za beach nk, na ndio maana wakanunua 'daladala' yenye uwezo wa kubeba mke, watoto, housegirl, wakwe na mashemeji bila matatizo. Ni watu wa kipato cha kawaida ila wana moyo wa upendo kwa familia zao. Ila pia hupenda kuendesha biashara za stationery na pharmacy ambapo hutumia hizo noah kusafirishia bidhaa kama macounter book na madawa ya aina mbali mbali.
View attachment 683754
10.) Land rover - Defender Series
Asilimia kubwa ya madereva hawa ni mapolisi na hata kama gari haina namba za polisi bado kuwa makini, hawa polisi huwa wanatabia ya kubandua plate namba kila baada ya operesheni na kubandika namba nyingine randomly ili kukwepa kufuatiliwa na kigundulika kirahisi. Huwa wanatabia ya kutohudumia magari yao vizuri, huwa wanajisahau na kufikiri kwamba gari likiwa chafu chafu, lenye mikwaruzi mikwaruzo, pasi kila mahali na kuoza oza kwa kutu ndio linaonekana gari la kazi. Na pia wana tabia ya kutojaza mafuta hadi yakaribie kuisha kabisa; Tabia hii ya madereva hawa ndio imechangia magari mengi aliyopeleka Makonda kule Arusha kutorudi.
View attachment 683785