1.)Toyota Brevis - ai Series / Mark X
Madereva wa magari haya hujisikia very powerful and classic wawapo barabarani, hii inatokana na gari hizi kufungiwa engine kubwa mithili ya fuso ndogo na kuwa na muonekano ambao ni very commanding.
Wengi wao ni vijana wa kipato kizuri wenye kati ya miaka 25 - 40 hali inayosababisha gari hizi kuhusishwa na uporaji wa wake/ wapenzi wa watu, kiukweli kwa interior ya hizi gari ni ngumu kwa mtoto kuchomoa pindi aingiapo humo, akishakalia tu ile leather ni amekwisha.
View attachment 683387
2.) Toyota Altezza / Subaru Forester - Noisy Series
Asilimia kubwa ya madereva wa magari haya ni vijana wanyoa viduku wasio na staha barabarani; kwanza wanaweka milio mikubwa mno bila sababu za msingi na hupenda kuendesha kwa mihemko kutokana na kelele kubwa za magari hayo. Wengi huonyesha dalili za matatizo ya kisaikolojia, ambapo hu-compensate kushindwa kwao katika nyanja mbalimbali za maisha kwa ku-seek attention mabarabarani kwa kuendesha kwa fujo na makelele yasio na msingi.
View attachment 683389
3.) Toyota Harrier /Lexus - G Series
Kiwango cha juu cha madereva wa magari haya ni wanawake wa makamo wenye umri wa kati ya miaka 38 hadi 45; na nimebaini wengi wao hua ni wamehongwa hayo magari na waume zao ambao kimsingi ni wazee wenye miaka 50 kwenda juu. Madereva hawa huwa na mashauzi barabarani hasa wanapokutana na gari zenye caliber ndogo kama vitz na kujihisi wapo kwenye ndege, hii hujionyesha kwa tabia yao ya kupenda ligi za kijinga barabarani.
View attachment 683390
4.) Toyota Landcruiser - V8 series
Wengi wao ni madereva wa magari ya serikali au mashirika mbalimbali ya kimataifa. Wengi wao hujisahau na kufikiri kwamba muda wote wapo kwenye msafara wa kiongozi na hawapaswi kabisa kukaa foleni. Hutanua kwa fujo bila aib wala uoga, na matrafiki nao huyagwaya magari haya na huyaacha yatanue as if yapo kwenye msafara. Wengi wao hujihusisha na upigaji nyoka mafuta hasa yale yanayotumia diesel na kwenda kuyauza kwenye black market. Hulipwa vizuri japo wengi huwa hawatoboi kimaisha.
View attachment 683392
5.) Toyota IST, Vitz ect - Baby walker Series
Kigezo kikubwa cha watu kununua gari hizi ni ulaji mdogo wa mafuta, hivyo ni an inherent characteristic ya madereva wengi kama si wote wa IST/vitz like cars kuwa ni wabahili mno hasa wanapokuwa fuel station; ni kawaida sana kuwaona wakiweka hadi mafuta ya buku 5 kwa kujiamini kabisa.
Pia wana tatizo la kisaikolojia ambalo kitaalamu huitwa 'Inferiority complex', ni ile hali ya kujisikia unadharaulika hata kama hakuna aliekudharau, muda wote anahisi kama anapopita watu wanamnanga ..." check jamaa na kitoy chake...."
View attachment 683397
6.) Range Rover / Land rover - Discovery series
Nimebaini asilimia kubwa ya madereva wa magari haya ni wazungu wa balozi mbali mbali pamoja na waarabu koko waishio nchini; hupendelea sana kutumia njia kuu na kamwe hawapendi kutumia michepuko hata foleni iwe kali vipi. Pia hupendelea kuendesha mijini na high suburbs tu, as if waliambiwa wakipita Tandale wata tekwa flani hivi, it goes without say, huwa wanajihisi ni raia wa daraja la juu zaidi ya madereva wengine wawapo barabarani. Na tabia yao kubwa ni kuning'iniza suti kwenye seat ya nyuma, sijui maana yake nini, nisaidieni hapa.
View attachment 683406
7.)