Tabia za kuchora!

Tabia za kuchora!

Papa Mopao

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2009
Posts
4,161
Reaction score
2,668
Kuna siku nilipokuwa darasani nakumbuka ilikuwa form two, kulikuwa na mwalimu mwanamke alikuwa anafundisha Chemistry, basi siku hiyo nilichoka sana kusikiliza, nilichofanya ni kuamua kuchora, nilichukua kikaratasi(plain paper) na pen nikaanza kumchora mwalimu copyright kabisa bila ya watu kujua mpoaka michoro ya pale ubaoni na ngua hadi mandhari ya darasa, kumbe jirani yangu alicheka sana baada ya kuona namchora mwalimu darasani, aisee tangu siku hiyo watu walijua kiwango changu cha uchoraji form two hiyo.
Form III sasa, kulikuwa na kampeni ya kuwachagua viongozi, basi kuna jamaa akaniomba nimchore ili abandike picha yake kwenye notes board, nilimchora fresh akiwa amesimama na miguu yake kabisa ya kupinda kwa nyuma mrefu baada ya kumaliza, nikawauliza watu niliyemchora ni nani, wengi walicheka sana baada ya kumtambua ni nani mpaka mwenyewe hakuamini, alibandika picha kwenye notes board na kuandika jina lake, siku ya siku jamaa akatangazwa mshindi maana iliwavutia wengi kuangalia hiyo picha kitu ambacho kilimsaidia jamaa kupata ushindi. Vituko vingi nilivyovifanya kupitia uchoraji, nitaviongezea vingine baadaye. Karibuni kama mna vituko mlivyokumbana navyo katika pitapita zenu!
 
hongera kwa kipaji papaa...tutakutana kwenye chemsha bongo
 
Tubandikie hapa basi japo picha mbili tatu, ili tuone kipaji chako, si kujisifia tu.
 
Nakumbuka nikiwa form 3 nilichoka kusikiliza hotuba za mwalimu wa historia ambazo zilikuwa ni ndefu sana zisizoisha kwa muda tarajiwa. Nikawa busy nachora makalio ya mdada. Kumbe katika kuongea kwake akizunguka darasani kafika kwenye desk langu mi sina habari! alisikitika sana maana nilikuwa tegemeo la darasa kitaaluma. akafikiri ndio mwisho wangu sitafika popote. Pia wakati ndio najua kuandika nikiwa darasa la kwanza niliwahi kuchora kikatuni darasani halafu nikaandika jina la mwalimu. Baada ya wenzangu kutishiwa wakanitaja, nilichezea bakora kumi safi tu pamoja na udogo wangu. sitasahau zile bakora za mwalimu Tausi kwakweli. Nilifikiri angesifia kipaji changu!
 
Safi sana, natumaini siku moja utamchora 'mpora' then atakupa tunu.
 
mimi shule ya msingi (darasa la sita na saba) pocket money yangu ilikuwa inatokana na kuwachorea wanafunzi wenzangu picha za vichwa vya watu upande wa usoni (kucheka na kununa vyote nilivichora vizuri sana) na mabasi maarufu kama luxury coach wakati ule kwenye makaratasi makubwa wakawa wanapeleka kwao kupamba. nakumbuka picha moja nilikuwa nauza sh. 5/-!!

sio siri wapendwa, nilifaidi sana hizo daladala

Glory to God!
 
I wish ningekuwa najua kuchora hata kikaragosi........
 
aisee

nilichora babake mtu akiwa uchi nikiwa sekondari, nilikula kisago balaa jamaa alichukia hadi analia
 
mimi shule ya msingi (darasa la sita na saba) pocket money yangu ilikuwa inatokana na kuwachorea wanafunzi wenzangu picha za vichwa vya watu upande wa usoni (kucheka na kununa vyote nilivichora vizuri sana) na mabasi maarufu kama luxury coach wakati ule kwenye makaratasi makubwa wakawa wanapeleka kwao kupamba. nakumbuka picha moja nilikuwa nauza sh. 5/-!! sio siri wapendwa, nilifaidi sana hizo daladalaGlory to God!
Hahahahahaa! dah umenikumbusha mbaaali saana! Nakumbuka niliwachorea wenzangu ramani za darasani darasa la nne,tano, sita na la saba! Nilipata sana hela kipindi hicho, ramani moja nilikuwa nawachaji kwa sh. 10/- aisee maisha yalikuwa matamu sana!
 
Wekeni basi hata mchoro mmoja jamani mbona porojo nyingi? maana porojo hizi zanikumbusha enzi zile kila mtoto anadanganya wenzie kuwa mjomba ake au baba mdogo wake alipigana vita ya Uganda! Haahaahaaa......
 
Papa mopao hebu nichore na mimi nione kipaji chako.
 
Papa mopao hebu nichore na mimi nione kipaji chako.
Usiwe na wasiwasi nta upload picha za kuchorwa hapa! Nipeni muda kidogo mpaka niziscan alaf nizi upload inachukua muda kidogo!
 
Wekeni basi hata mchoro mmoja jamani mbona porojo nyingi? maana porojo hizi zanikumbusha enzi zile kila mtoto anadanganya wenzie kuwa mjomba ake au baba mdogo wake alipigana vita ya Uganda! Haahaahaaa......
Ntazi upload picha hapa!
 
Back
Top Bottom