Tabia za Kitanzania zinazonikera...

Kuongea na mtu mpaka umguse au neno unaliishia kati afu wewe ulimalizie.
Mfano akisema tutae.......basi wewe umjibu nda.Teh teh teh
 
Nimekuelewa kaka mkubwa...

Hapo kwa bold kuna siku utapokea kipondo kisicho chako kumbe mtu anajihami,dawa ukimaliza unamuuliza "Iko sawa nitume?"
 
Au ni za Kichina????

Habari nzima ya tabia za watu kwa nchi na kabila ni gross oversimplification.

Watu wachafu watakuwa wachafu tu, wawe Watanzania au Wachina, vivyo hivyo wajinga na wapumbavu.

Kuunganisha uchafu wao, ujinga wao na upumbavu wao na taifa lao hakuwatendei haki wale raia wengine wa hizo nchi ambao hawana tabia hizo.

Hii inaitwa "stereotyping". Ukiiendekeza unaingia kwenye bias and racism.
 
Kiranga ,hivi hakuna baadhi ya Watanzania wenye tabia hizo?
 
Last edited by a moderator:
Mmmh hii me pia inaniudhi sana utadhani liko kwake limekaa ktk kochi kubwa

Je mnaekaa siti moja kwenye daladala kisha anakuzungushia mkono kwenye siti uliyoegemea?
Au anasinzia halafu anakuegemea? Natamani nimtie konzi
 
Je mnaekaa siti moja kwenye daladala kisha anakuzungushia mkono kwenye siti uliyoegemea?
Au anasinzia halafu anakuegemea? Natamani nimtie konzi
dada Ennie upo jamani?
jana ulikatiza sana kwenye mind yangu. Nilikukumbuka sana. usikute ndo ulikuwa unataka kumtia konzi mtu, lol!
 
Kuna madogo sijui wanakuwa wamepewa magari ya mashamaji zao basi wanapiga mziki mkubwa hadi kwenye makusanyiko ya watu ili mradi wa draw attention......
 
Je mnaekaa siti moja kwenye daladala kisha anakuzungushia mkono kwenye siti uliyoegemea?
Au anasinzia halafu anakuegemea? Natamani nimtie konzi

Yaani..unaona kama unakumbatiwa hivi..na kwapa sasa ndo uuuuwi!!!!

Mkwapa una ramaniiiiiii...halafu analalamika duuunh leo jooootoooo!!!!!!!
 
Hahah...mpwa umenikumbusha mbali sana maana hii tabia tulikuwa nayo sana sisi ambao tumechaza basketball miaka ile ndio mchezo huo umeanza kushika hatamu hapa Tanzania haswa Dar es Salaam...
Mambo hayo yalikuwa common sana pale kota za Tanesco, Don Bosco na kwingineko...

Kuna madogo sijui wanakuwa wamepewa magari ya mashamaji zao basi wanapiga mziki mkubwa hadi kwenye makusanyiko ya watu ili mradi wa draw attention......
 
Kuongea na mtu mpaka umguse au neno unaliishia kati afu wewe ulimalizie.
Mfano akisema tutae.......basi wewe umjibu nda.Teh teh teh

hahahahaaaaaa!
Skiza nkwambie . . . Bla blah blah. . . .Skiza nkwambie . . . Blah. . . Blah. . . Blah . . . Skiza nkwambie. . .
 
Kiranga ,hivi hakuna baadhi ya Watanzania wenye tabia hizo?

Kuna Watanzania wenye tabia hizo, kuna Wakazakhstan walio na tabia hizo, kuna wa Romania walio na tabia hizo.

Na hatujui kama kukiwa na utafiti wa kuwalinganisha watu kwa mataifa, Watanzania wataibuka ndio washindi wa kwanza kwa tabia hizi.

Vilevile kuna Watanzania, Wakazakhstan, wa Romania wasio na tabia hizo.

Kwa nini uziite tabia zinazotokana na uchafu, ujinga, upumbavu etc "za kitanzania" kama vile wa Tanzania ndio wameshikilia kwa ukiritimba ugavi wa tabia hizi kama TANESCO walivyoshikilia kwa ukiritimba ugavi wa umeme Tanzania?
 
Kuna madogo sijui wanakuwa wamepewa magari ya mashamaji zao basi wanapiga mziki mkubwa hadi kwenye makusanyiko ya watu ili mradi wa draw attention......

Mtajuaje anaendesha gari?
 
Yaani..unaona kama unakumbatiwa hivi..na kwapa sasa ndo uuuuwi!!!!

Mkwapa una ramaniiiiiii...halafu analalamika duuunh leo jooootoooo!!!!!!!

Yaani! Unaweza ukainuka tu umuachie siti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…