Fanya hivi unapoingia kwenye sehemu za starehe

Fanya hivi unapoingia kwenye sehemu za starehe

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,902
Reaction score
19,648
Salaam jamiiforum.

Leo ni siku ya ijumaa tulivu,siku ya mwisho wa wiki Kwa wafanyakazi na hata wasio wafanyakazi.

Ndiyo siku maalumu wengi wanaenda sehemu mbalimbali za starehe iwe clubs,bar na kwenye makasino.

Lakini mara nyingi tunapoenda sehemu hizi kwaajili ya kufurahi mara nyingi furaha hugeuka majuto kutokana na namna ulivyo either ukilewa au ukiwa sana au tu ukishindwa kutumia busara

Hebu chukua hizi notes

1.Tenga pesa ya kutosha.

Kwa mfano,umepanga ukatumie laki mbili ,basi uwe na laki moja pembeni kwaajili ya dharula,kuna kukutana na marafiki mliopotezana muda mrefu,kuna bidhaa kupanda bei na wewe hukujua.na dharula nyingine nyingi.

2.Tulia soma mazingira Kwanza.

Usikimbilie kuagiza vitu Kwanza badala yake agiza hata maji, kwasababu huenda ukabahatika kununuliwa na Ile kampani yako ambayo huwa unainywesha siku zote.kuagiza harakaharaka washikaji wataona unazo hivyo za kwao watabana.

3.Usikimbilie kutafuta mademu,awe muhudumu au mteja.

Unajua wanaume wengi huumia,au kupoteza maisha kwasababu ya mademu,yaani Yule barmaid unayehisi ni Malaya,kuna wanaume wameweka moyo wao wote ,so ni vema kuchukua tahadhari.

4.Usiingilie ugomvi labda Kwa unaowafahamu,

Kuna mbinu mpya ya kumuibia mtu Kwa kuanzisha ugomvi utainuka Kwa Nia njema lakini utaishia kuibiwa simu na wallet yako,kuumia,kufa,au kuishia mahabusu.

5.Usisubiri ulewe Sana kisha ulipe bili.

Wewe nunua vinywaji lipa kabisa,kama Una washikaji zako ni vema wakajua umelipa kuliko kulipa kimyakimya.unaweza Tumia laki na nusu ukaletewa bili ya laki sita tena wahudumu wanapanga njama kabisa kukuibia huku wakiwa na ushahidi feki

6.Acha sifa na mashindano

Kuna mtu ananunua pombe ya gharama ili watu wajue ana hela jambo ambalo linaweza kukugharimu,kuibiwa,kuzidishiwa bili,pamoja na kutumia pesa zaidi nje ya bajeti.

7.Epuka kutembea na cash nyingi.

Badala yake lipa Kwa njia ya mtandao iwe simu na njia nyingine,Kwanza SMS zinabaki kama ushahidi kwako,cash kubwa ni kujihatarishia maisha.

8.Ukilewa Sana usidrive.

Mmmh hapa sijui nilie au nifanyaje,Mimi hapa nimepoteza marafiki wanne ,ambao vifo vyao vyote ni ajali baada ya kuendesha wakiwa wamelewa.

Nawatakia weekend njema.
Castle lite beer for life
 
Back
Top Bottom