Tabia za Kitanzania zinazonikera...

Tabia za Kitanzania zinazonikera...

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
76,320
Reaction score
108,378
1. Kwenda haja ndogo na kubwa hovyo...
Hivi huwezi kuwa mstaarabu na kutafuta msala wa karibu walau hata kwenye bars au hata gas stations?
Yaani kuna sehemu ni maarufu kwa watu kumwaga oil zao tena bila hata aibu...Hebu tuwe wastaarabu bhanaaa...

2. Watu wanayopayuka ndani ya daladala, ndege na vyombo vingine vya usafiri...
Utakuta mtu anaongea kwa sauti kubwa kama Sued Mwinyi anatangaza mechi baina ya Yanga na TP Lindanda wana Kawekamo ya kina George Masatu...
Mmoja yupo nyuma na mwingine yupo mbele kabisa, wanasogoa weee wakati huenda mbali na kutumia lugha zao za asili...omba Mungu kisiwe Kisandawe au Kimasai(huu ni mfano tu)...

3. Wanaume ambao hata wakikuona upo na dada yako wanadhani ni kimada...
Hawa huwa wananikera hakuna mfano, "shemeji kapendeza" mara nyingi hiyo ni moja ya kauli za watu kama hawa...
Pia wapo wale wengine ambao huenda mbali zaidi na kuazna kupiga miluzi au kutoa machombezo yenye kuashiria matamanio ya kingono...

4. Wale wote wanaotupa hovyo uchafu...
Mtu umemaliza kunywa maji yako ya uhai, au Kiroba n.k...kwa nini usihifadhi hicho kifungashio na ukakiwage sehemu stahiki mbele ya safari...
Yaani sisi Watanzania sijui lini tutajifunza kutumia akili....ndio maana kuna vitu vingi nadhani Mungu kaamua kutunyima kwa sababu ya tabia zetu za ajabu ajabu...

5. Makonda waonyanyasa wanafunzi...
Hawa watu sijui hawajawahi kwenda shule au ni ulimbukeni! Yaani wasimuone mwanafunzi anasogelea gari, kirahisi tu utasikia "Oyaa limeshajaa"...
Magari yenyewe hata sio yao na wala hawana ndoto za kuwa na magari miaka 900, lakini ni watata zaidi ya utata wenyewe...

Ninayo mengi ya kuandika ila hayo machache ndio huwa yananikera sana labda na wenzangu mna ya kuongezea....
 
Oops!
Hivi umefanya research na kugundua kuwa ni Watanzania pekee wenye tabia hizi?
 
Ongezea hizi;
'
Wanaopenga kamasi hovyo tena bila vitambaa
'
Wanaojisaidia vyoo vya umma na kukifanya kinyesi kuwa wino wa kuandikia ukutani!
 
Hizo tabia mwenyewe czipendi,hasa hyonumber mbili jaman,yanî mtu daladala nzîma anasikika yeye ampaka anashuka ktk dalaadala umejua mambo meng kuhusu yeye
W
 
Nimelenga Watanzania tu hata kama kuna wengine wenye kufanya hayo wapo...

Oops!
Hivi umefanya research na kugundua kuwa ni Watanzania pekee wenye tabia hizi?
 
Usiombe awe anaongea na simu halafu anashindwa kusikizana na huyo aongeaye naye...

Hizo tabia mwenyewe czipendi,hasa hyonumber mbili jaman,yanî mtu daladala nzîma anasikika yeye
ampaka anashuka ktk dalaadala umejua mambo meng kuhusu yeye
W
 
Ongezea hizi;
Wanaojisaidia vyoo vya umma na kukifanya kinyesi kuwa wino wa kuandikia ukutani!


Hii niliiona sana shule zetu za Boarding haswa kwa wanafunzi waliokuwa wakihitimu
 
Hii niliiona sana shule zetu za Boarding haswa kwa wanafunzi waliokuwa wakihitimu

Hii kidogo afadhali japokua afadhali ni afadhali ya kijinga,lakini jambo hili linapofanya na limtu lenye watoto is disaster!!
 
Kuna wale wenye tabia ya kuweka music/radio loudspeaker alafu anaingia kwenye gari ama mkusanyiko wa watu, very comfortable, sielewi huwa wana maana gani, kujulisha watu kuwa wanamiliki simu zenye memory card/radio ama hawafahamu matumizi ya hearphones.:help::help::help::bored::bored::bored:
 
yuck. nahisi kichefuchefu, is this true??

Very true...waliokuwa wakifanya hivyo ni ile kuonesha retaliation baada ya maisha magumu na pengine mateso ya shule
 
Kuna wale wenye tabia ya kuweka music/radio loudspeaker alafu anaingia kwenye gari ama mkusanyiko wa watu, very comfortable, sielewi huwa wana maana gani, kujulisha watu kuwa wanamiliki simu zenye memory card/radio ama hawafahamu matumizi ya hearphones.:help::help::help::bored::bored::bored:

halaf sim ikiwa mchina yaani ni full makelele let say
ni ktk daladala
 
Back
Top Bottom