Tabia ya wanaume kuchelewa kurudi nyumbani

Tabia ya wanaume kuchelewa kurudi nyumbani

Trichuria

New Member
Joined
Aug 24, 2012
Posts
3
Reaction score
3
Hi wana forum ninahitaji sana ushauri nipo kwenye wakati mgumu na sijui cha kufanya. Mimi ni mama wa watoto watatu nimeolewa mtoto wangu wa tatu anaumri wa miezi miwili sasa.

Nina mume na tunaishi vizuri anatuhudumia kadri ya uwezo aliojaliwa na mungu kwa kila tunachohitaji kama kiko ndani ya uwezo wake.

Na kiukweli ninampenda sana mume wangu kuna wakati ninapata vishawishi ila ninavishinda kwa sababu ninampenda sana sweet wangu na siwezi kumsaliti. Sasa kuna kitu kinaniumiza sana mume anapenda sana kuchelewa kurudi akitoka asubuhi kurudi saa tano hadi saa sita ucku kila siku na sio mnywaji pombe.

Kiukweli sipendi tabia hiyo na inanifanya ninakosa raha hata kumkaribisha chakula na kumsaidia vitu vingine kama Mke wake ninaomba mnishauri nifanye nini ili ndoa yangu iwe na furaha na amani.
 
pole jaribu kuongea ujue anachelewa wapi isije kuwa foleni za jiji we unamwazia mabaya
 
Kaa naye chini uongee nae kwa upendo, naimani atakwambia sababu ya kuchelewa.
 
Kaa naye akiwa kwenye mood nzuri muulize kwa upendo tu kwanini anachelewa,akiwa mkali sana kuna namna itabidi umchunguze kiundani zaid.
 
Pole saana , ila.huenda pia wewe ni sababu

Huenda humkarimu vizuri akirudi, unamfokeaaa au vjembe

Huenda baada ya kujifungu umehamisha mapenzi kwa mtoto kuliko mume

Huenda umekuwa mchafuuu

So jiangalie kwanza wewe, kisha kaa nae muulize kwa upoleee tatizo nini..
 
Hi wana forum ninahitaji sana ushauri nipo kwenye wakati mgumu na sijui cha kufanya. Mimi ni mama wa watoto watatu nimeolewa mtoto wangu wa tatu anaumri wa miezi miwili sasa.

Nina mume na tunaishi vizuri anatuhudumia kadri ya uwezo aliojaliwa na mungu kwa kila tunachohitaji kama kiko ndani ya uwezo wake.

Na kiukweli ninampenda sana mume wangu kuna wakati ninapata vishawishi ila ninavishinda kwa sababu ninampenda sana sweet wangu na siwezi kumsaliti. Sasa kuna kitu kinaniumiza sana mume anapenda sana kuchelewa kurudi akitoka asubuhi kurudi saa tano hadi saa sita ucku kila siku na sio mnywaji pombe.

Kiukweli sipendi tabia hiyo na inanifanya ninakosa raha hata kumkaribisha chakula na kumsaidia vitu vingine kama Mke wake ninaomba mnishauri nifanye nini ili ndoa yangu iwe na furaha na amani.

Sema haki ya mungu!
 
utakua wamfanyia vitimbi ambavyo yeye hapendi arudipo mapema nyumbani
 
...siku hizi haya wanawake hawakai home, saa nne-tano ndio wanaingia home. Kwa hiyo ni 50/50.
 
Je tabia yake hiyo ameianza siku za karibuni au toka amekuoa huwa anachelewa? Kama jibu ameanza siku hizi basi jiulize kwa nini maana huenda na wewe una matatizo yako kwa hiyo anaona bora achelewe kurudi, kama ameanza kitambo basi hiyo tabia umelea mwenyewe.
 
hivi ndivyo si tunakuwanga saa zingine. labda ni kitu ataacha mkiendana lakini sijui jinsi ya kutubadilishia hili njaro..
 
yanachelewa kurudi halafu yanawahi KUFIKA mianaume ya siku hizi thnx god mi m one in millions if nt thousands yani tofauti nawahi kurudi halafu nachelewa KUFIKA .
 
Kuna mawili either wewe ni chanzo au kuna kitu kinachomfanya yeye achelewe kurudi.Kaa nae chini umuulize
 
...siku hizi haya wanawake hawakai home, saa nne-tano ndio wanaingia home. Kwa hiyo ni 50/50.

Nimejikuta tu nacheka...sasa Eli79 hii hoja yako umeiibua kutoka wapi aisee...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom