nitonye
JF-Expert Member
- Dec 18, 2011
- 7,349
- 3,910
Nitonye asante, Kabla ya ndoa muda wote aliokuwa free alitaka tuwe pamoja, kitu ambacho kilinifanya nimzoee na yeye kuwa kila kitu kwangu rafiki yangu, mshauri wangu baada ya ndoa ndio akaanza kuwa bize na marafiki zake na urafiki wetu ukapungua ilikuwa inaniuma nikimuambia atabadilika muda mfupi halafu anarudia. Sasa mwanzo alikuwa anarudi saa mbili tatu ucku baada ya kujifungua ndio ninaona hali inazidi inafikia hadi saa sita Ucku. Kiukweli akirudi mapema huwa ninafurahi nitafanya chochote atachohitaji. Ila anaporudi hiyo saa sita hata nikiwa macho hata kumuambia karibu ninashindwa ninamuangalia tu ndio nikaona niitoe humu nipate ushauri.
Nimekuelewa vizuri, mda mwingine sisi wanaume huwa tunashauriwa vibaya na marafiki na hivyo kujikuta tunazisahu familia zetu. Mara nyingi wengi wetu tukishawazalisha wanawake au wakiwa kwenye ulezi tunawaona kama kinyaa hivi. Kitu cha msingi muulize ni sababu ipi hasa inayomfanya achelewe kurudi nyumbani ila usimpangie mda wa kuwepo nyumbani. Mweleze jinsi unavyojisikia unapoona anachelewa kurudi nyumbani naye ajue kuwa mke wangu hapendi tabia hii na sio kununanuna na ukiona habadiliki basi nenda kwa wazazi wenu ukawaleze hili jambo