KERO Tabia ya Shule ya Sekondari Sikanda (Tabora) kuwalipisha Wazazi mifuko ya Cement sio jambo sahihi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Tabora, kuna hoja naomba nishee na Wana JF, ipo hivi, Watoto ambao wanasoma Shule ya Sekondari Sikanda kama akichelewa kuripoi hata kama ni siku moja tu, mzazi wake anatakiwa kulipa hela ya faini ambayo ni mfuko wa cement.

Bila kufanya hivyo hawezi kuruhusiwa kuingia kuendele na masomo bila kujali kama uchelewaji ulitokana na mzazi kukosa ada au la.

Ukiwaleza kuwa mtoto alichelewa kwa kuwa alikuwa anaumwa wanakwmabia wanahitaji cheti cha Daktari Mkuu wa Hospitali husika.

Mzazi au mlezi wa mtoto ukiwa haina hela ya kulipa faini uongozi wa Shule unakuletea Askari Polisi na wanakwambia wanakukamata kwa kosa la kutompeleka mtoto shule.

Inawezekana ni jambo zuri lakini nawashauri viongozi wa Shule hiyo kuwa wanawaumiza wazazi na walezi kwani sio kila mzazi anapenda kuona mtoto wake anachelewa kuingia shule.
 
Mzazi au mlezi wa mtoto ukiwa haina hela ya kulipa faini uongozi wa Shule unakuletea Askari Polisi na wanakwambia wanakukamata kwa kosa la kutompeleka mtoto shule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhimiza mahudhurio ya mwanafunzi yawe vizuri ni jambo jema.Lakini,wawe na kiasi cha adhabu.Hivi shule hiyo ipo katika kata gani na inamilikiwa na serikali au ya binafsi?
 
Back
Top Bottom