Tabia ya kuzima data ni ushamba

Tabia ya kuzima data ni ushamba

505d427fc4a04c8f231422498fc621dd.jpg


Apo waliotengeneza cm wanakwambia *Using higher mobile speeds loads data faster but may decrease battery life*

Utakavotumia 2G...chaji italika lkn ukitumia 3G italika zaid kuliko kias kilicholika kwny 2G... na Ukitumia 4G kitalika zaid ya 2G na 3G.... Ulichojisahau Mtoa mada ni kua kuna zile apps ambazi zenyewe zinafanya Auto sync kila baada ya sec kadhaaa...hvo bs uwashaji wa data tu unaeza ukala chaji tofaut na ungekua umezima hlf uwashe badae.....
 
Ushamba kwako wengine ndo ujanja wetu huo.

Kwa taarifa yako: Unapozima Data unapata faida nyingi sana kuliko kuiacha ikiwa imewaka bila sababu za msingi.

Akili ni nywele kila mtu ana zake.

Aaf, kila mtu anajinunulia bundle mwenyewe. Tuheshimiane tusipangiane/kushawishiana namna ya kuzitumia.

Period!!!
 
Wewe jamaaa wewe...yaaani umenunua hicho ki itel chako ndo unakuja kutufundisha ujanja wa simu au???
Yaani mimi sizimagi data tu naiweka simu pia ktk ultra power mode kabisa
 
Sio kweli kama unavyofikiri, kuna app zinakula data constantly kwenye background hata kama haujapata msg wala notification.

Kwa mfano kama una email account hasa hizi za kawaida sio gmail huwa zinatumia polling yaani hakuna push kwa hiyo kila dakika kadhaa inaamka inafanya mawasiliano na server kucheki kama kuna email hili linakula data na battery.

Pia kuna app zina preload data kwenye background kuzifanye zionekane fasta unapofungua so kama instagram inaload picha na videos hata kama hauitumii ili ukifungua picha zionekane kwa haraka hii pia inakula data na battery.

Hata kwa vitu kama notification, kuingia kwa wakati mmoja hakuli betri/data kama kuingia kimoja kimoja so ni bora kuzima data na kuviacha viingie vyote kwa pamoja kuliko viingie kimoja kimoja.

Pia ile connection tu ya data kwenye mnara inaweza ikawa inakula battery yenyewe kutojali kama kuna data inaingia na kutoka.

Ndo maana Android mpya kuna technolojia inaitwa doze ambayo inazima data kama ikiona simu haitumiki i.e simu haijaguswa kwa muda mrefu.
 
Sio kila ukiwasha data ni kwa ajil ya wasap tyu akna mama mbn mnasumbua xkuhiz ndo tatzo lenu msiokua na kaz mda wote mnawaza kuchat tu umbea cjui instagram
Jifunze kuandika asee wewe kweli ni boy na sio gentleman
 
Tatizo watu wanazima Dada kuepuka usumbufu was miujumbe ya hovyo ya kila mara
 
Mkuu umewasilisha sawa lakini umekosea kitu kimoja kujiona mjanja akati wewe ndo mshamba wawa shamba mbele ya washamba.!!! Umeshindwa kung'amua kuwa kuzima data kuifanya simu kurelax na kuipa performance yake katika usanifu mzuri ni sawa nawewe unapopumzika baada ya kazi nzito mkuu USIFORCE TUFANANE AKILI/TUKOPI LIFE LAKO.
Nadhani hii mada ilibidi iishie kwenye hii post.
 
Baadhi ya solutions unazoweza kutumia!

1. Greenify

2. Zima Auto-Sync. (Kwenye settings)

3. Ikiwa umuweka tick kwenye option ya ku-back up data kwenda Google servers (kwenye Settings), usitafute mchawi nani!

4. Baadhi ya apps kila baada ya sekunde kadhaa zinatuma request online kwa ajili ya matangazo/ads, tracking, analytics, crash reports, etc.
Kama hutumii Adguard / DNS66 / Blokada / AdAway / NetGuard, bando & betri ya simu yako zita-suffer!

5. Zima & usithubutu kuwasha GPS, unless ikilazimika kufanya hivyo.

6. Washa Wi-Fi & Bluetooth pale tu itakapohitajika

7. Punguza mwangaza/brighteness kuwa wa kiasi. Usiweke "Auto"!

8. Ikiwa uko maeneo ambayo 3G/4G haishiki vizuri, weka 2G kiroho safi.
Kama pia 2G haishiki weka "Airplane Mode".

9. Vibrations nazo haziko mbali kwenye kula Charge. Turn 'em off!

10. Ikiwa simu yako ina apps ambazo huzitumii mara kwa mara / huna kazi nazo basi zifute au zi-Disable/Freeze kama inawezekana.

Kama umeipenda basi bofya/Gonga "like".
 
Utakuta mtu kama huyu ametumia siku kadhaa kufikiria hizi pumba alizo ziandika.pole sana kijana maana uwezo wako wa kufikiri ni mdogo zaidi ya ubongo wa mende.
Usinifanye n'cheke mkuu
 
Kama unakula ugali wa bure tulia acha kuperemba kazi zingine watu tunafanya hazihitaji ukaribu na usumbufu wa cm pia data inakula charge ila sana ni kazi kama upo tu kijiweni na washkaji zako unapiga zogo washa data alafu umuulize house gel chai tayari
Ana uelewa mdogo, ameshindwa kujua kwanini watu wanazima data?!
 
Umaskini mkuu ndo unasababisha yote haya. Hakuna anayependa kuzima data bali ni masuala ya cash tu yanasumbua..
Ungesema kwa 'baadhi' ya watu. Wengine tunazima kutokana na ubusy wa shughuli bundle sio issue.
 
Kwa siku 5 nimejaribu kuacha data ON naona kawaida tu.Aisee kumbe ulikuwa ushamba tu!amna cha chaji wala gharama,nashukuru kwa kunifundisha hili.Kukariri noma sana!!
 
Mi naona kama umechanganyikiwa halafu wewe ndo mshamba zaidi na pengine mswahili.
 
Wamekuckia mkuu... Siku nyingine uje na uzi unaosema 'kutumia power bank ni ushamba' mi ntatetea hoja
 
Back
Top Bottom