Tabia ya kutofuata miiko ya matumizi ya silaha, Aliyoyafanya "Ukiwaona" almanusura nifanyiwe mimi

SlimFit

JF-Expert Member
Mar 29, 2016
1,821
2,648
Salamu na Utangulizi

Waungwana naamini mpo salama nami kwa kudra zake Muumba nipo salama. Tuwaombee wenzetu ambao kwa namna moja au nyingine afya zao si nzuri zipate kuimarika na warudi katika shughuli zao. Binafsi si muandishi wa mada humu jukwaani, ila ni mdau mzuri wa kuchangia hoja zinazoletwa humu ndani. Naomba musome mkasa wangu huu mwanzo mwisho na kama kuna la kujifunza tujifunze, pia kama mtu atakua na mawazo mbadala ni ruksa kutiririka ili tujifunze sote.

Mimi ni kijana ambaye miezi michache ijayo nitakua natimiza miongo 3 ya kuwepo katika ulimwengu huu. Ni kijana wa 1 katika familia ya watoto 4. Katika kukua kwangu nikiwa darasa la tano mzee alianza kuwa karibu sana na mimi na mara nyingi alikua akiniambia/kunihusia "wewe ni kaka mkubwa nakukasimisha majukumu yangu katika huu mji naomba ujiamini mimi nakuamini usiyumbishwe na mtu yeyote yule katika jambo unalo amini liko sawa".Katika ule umri mzee kuniambia yale maneno niliona kama ananikweza na sikusistahili. Kimuonekano mimi ni mwembamba kupita maelezo ila mkakamavu.

Hayo maneno hapo juu baba yangu alikua akiniambia kila anaporudi na tulikua tunaongea mambo mengi sana kuhusu maisha kila alipopata nafasi japo umri wangu ulikua ni mdogo. Aliendelea kunihusia hivyo hadi nilipo enda chuoni hakusita kutia neno kila alipopata muda. Mwanzoni niliona kama baba ananigasi kwa kunipa majukumu ambayo yapo nje ya uwezo wangu, lakini hii kitu ilinijengea uhodari wa hali ya juu sana si darasani hata katika jamii inayonizunguka. Yaani ilifika mahali ile sauti ya kimamlaka ya mzee ikawa ndio ipo kwangu huku busara ikitawala kupita maelezo pale ninapo ongea na watu.

Mkasa na malimbukeni wawili wasio na maadili;

Kwa mnaoifahamu njia ya Bagamoyo rd kama unaenda Tegeta, Ukitoka tu pale darajani Makonde kuna njia ya kwanza kushoto halalafu unakamata “service road” kwa mbele upande huohuo kushoto kuna Carwash sikumbuki jina, baada ya iyo carwash kuna njia inapandisha kushoto kwenda Primrose Hall, sasa hapo kwenye T inayopandisha Primrose mbele yake kuna wamama wanauza matunda na dizaini flani kuna bodaboda ndipo Mkasa huu ulipotokea.

Ilikua hivi mimi nilitoka service road na kausafiri kangu, nikaenda kuegesha upande wa carwash ili nikanunue matunda niendelee na safari yangu kwenda kusalimia mgonjwa maeneo ya shule kule. Baada ya kuchukua matunda nikachukua kausafiri kangu, ile naingia tu service road kukawa na roli haya ya mchanga nalo likawa linakuja napo tokea mbele yangu kukawa na gari nyingine 2 sasa katika hizi gari 2 kuna gari ”funCargo” iliyokua katikati (yaani mie nyuma, Funcargo kati na nyingine mbele), Funcargo baada ya kuona lile roli na yeye yupo kati sijui alipata wenge kutoka wapi, lori lilipo karibia kwake gari ‘’funCargo” ikaanza rudi nyuma, mie nikaanza kumpigia honi kama gari moshi jamaa wapi hadi gari yake “Funcargo” ikafika kwa usafiri wangu usawa wa plate number ndio ikasimama.

Kwa haraka nikawa nimegundua kua usafiri wangu haujapata uharibifu wowote, kwahiyo nikawa nimetulia tu ndani. Jamaa wa Funcargo wao wakashuka na jazba za hatari wakaja kugonga kioo changu kuonyesha ishara kua nifungue mlango nikashuka. Ile kushuka tuu, si wakalianzisha bana kwamba kwa nini nimegonga gari yao ”Funcargo”, mie kimya. Wakaanza unadharau sana we dogo, mie kimya. Ikabidi niende mbele kuangalia damage iliyotokea, kwangu kukawa hakuna damage wao kwao ipo kumbuka wapo wa 2 na mie nipo peke yangu. Sasa watu wakawa wanaona kinachoendelea pale. Wale jamaa ukiwaangalia kimuonekano ni kama walikua wanajiamini sana na walikua tayari kwa lolote

Mie kwakua nilikua sahihi, ile sauti ya kimamlaka ikaja huku nikimtumainia Muumba nikasema kwamba nanukuu “ watu wote hapa sio wapumbavu hasa hawa wamama wafanyabiashara, wameona tukio zima mwanzo mwisho sasa kama muna la ziada ongeeni kama hamna mjue mnapoteza muda wangu, ama sivyo nitaondoka na nyie na msiamini kitakachotokea”. Baada ya hapo nikaona jamaa jazba zimepungua, mmoja akasema “lakini hapo ni kama mie nilichubua so haijadhurika’’ tuondoke. Hao wakaondoka dizaini kama paka wale wa bar wanapokosa mabaki.

Hapa ndio Dhumuni la Uzi huu lilipo.

Nikiwa bado nimepigwa na bumbu wazi katika eneo lile mama mmoja akasema nanukuu ”Kijana wasamee bure tumeona kilichotokea, tena yule aliyekua abiria alikua na bastola kiunoni na aliiseti akiwa anashuka kutoka kwenye gari (funCargo), hili eneo yaani sijui likoje na mkasa wa "Ukiwaona" nao ulikua sio mbali na eneo hili”. Nami nahitimisha kwa kuwauliza nyie waungwana, ujuaji na kutofuata miiko ya matumizi ya silaha za moto kwa baadhi ya watu ambao ni limbukeni, je ilikuaje na uliwezaje kujinasua katika saga hiyo?
 
Mimi kuna mmoja namvizia anajikutaga mtabe sana akishakunywa.
Nitapita nayo kama kipanga ili akajibu ofisini kwao kwa huyo RSO wao kama wanakabidhiwa pistol kwa ajili ya kuja kufanya mauzo bar au waende nazo msaada malindoni!
 
Tatizo ushamba tu.

Yaani mtu ana silaha, hajui hata ni wapi atakaa aitoe itumike, mwisho wa siku anatolea watu wasiohusika nayo.
sasa gari limegongwa unatoa silaha ya kazi gani???

Ilitakiwa upige picha plate number unafungua kesi, mtu ananyang'anywa silaha,pumbavu.
 
tatizo ushamba tu.

yaani mtu ana silaha, hajui hata ni wapi atakaa aitoe itumike, mwisho wa siku anatolea watu wasiohusika nayo.
sasa gari limegongwa unatoa silaha ya kazi gani???

ilitakiwa upige picha plate number unafungua kesi, mtu ananyang'anywa silaha,pumbavu.
Exposure nayo ni shida, yaani wanajua kila mtu anaogopa hizo pistol zao. Nawashuru sikugundua mapema hilo la pistol
 
Mimi kuna mmoja namvizia anajikutaga mtabe sana akishakunywa.
Nitapita nayo kama kipanga ili akajibu ofisini kwao kwa huyo RSO wao kama wanakabidhiwa pistol kwa ajili ya kuja kufanya mauzo bar au waende nazo msaada malindoni!
unataka mtu akufate na magoti blaza, silaha ya kazini isikie tu.
 
Nami nahitimisha kwa kuwauliza nyie waungwana, ujuaji na kutofuata miiko ya matumizi ya silaha za moto kwa baadhi ya watu ambao ni limbukeni, je ilikuaje na uliwezaje kujinasua katika saga hiyo?
Ni miaka kama sita sasa huenda imepita, tuko kwa Mama Kamche, Ng'ambo ya pili ya barabbara ukiwa Kanisa la Kakobe! Usiku wa saa tatu hivi au nne!

Miaka ile kwa Mama Kamche palikua panajaza sana, sasa ikatokea kutofuatiana kiswahili tu, jamaa wakaanzisha vurugu, mmoja akatoa bastola! Hahhaahahh ninachokumbuka ni kwamba aliingia kwenye gari na kuondoka na hata pombe yake hakumaliza! Alijua wote pale tumekaa vilaza na walevi. Ukiwa na silaha kamwe usiitumie kumtisha mtu
 
Mimi kuna mmoja namvizia anajikutaga mtabe sana akishakunywa.
Nitapita nayo kama kipanga ili akajibu ofisini kwao kwa huyo RSO wao kama wanakabidhiwa pistol kwa ajili ya kuja kufanya mauzo bar au waende nazo msaada malindoni!
Hakikisha mikonoyako ipo shap sana vinginevyo tutakuja kula ubwaubwa msibani huku wewe ukiwa kwenye jeneza
 
Salamu na Utangulizi

Waungwana naamini mpo salama nami kwa kudra zake Muumba nipo salama. Tuwaombee wenzetu ambao kwa namna moja au nyingine afya zao si nzuri zipate kuimarika na warudi katika shughuli zao. Binafsi si muandishi wa mada humu jukwaani, ila ni mdau mzuri wa kuchangia hoja zinazoletwa humu ndani. Naomba musome mkasa wangu huu mwanzo mwisho na kama kuna la kujifunza tujifunze, pia kama mtu atakua na mawazo mbadala ni ruksa kutiririka ili tujifunze sote.

Mimi ni kijana ambaye miezi michache ijayo nitakua natimiza miongo 3 ya kuwepo katika ulimwengu huu. Ni kijana wa 1 katika familia ya watoto 4. Katika kukua kwangu nikiwa darasa la tano mzee alianza kuwa karibu sana na mimi na mara nyingi alikua akiniambia/kunihusia "wewe ni kaka mkubwa nakukasimisha majukumu yangu katika huu mji naomba ujiamini mimi nakuamini usiyumbishwe na mtu yeyote yule katika jambo unalo amini liko sawa".Katika ule umri mzee kuniambia yale maneno niliona kama ananikweza na sikusistahili. Kimuonekano mimi ni mwembamba kupita maelezo ila mkakamavu.

Hayo maneno hapo juu baba yangu alikua akiniambia kila anaporudi na tulikua tunaongea mambo mengi sana kuhusu maisha kila alipopata nafasi japo umri wangu ulikua ni mdogo. Aliendelea kunihusia hivyo hadi nilipo enda chuoni hakusita kutia neno kila alipopata muda. Mwanzoni niliona kama baba ananigasi kwa kunipa majukumu ambayo yapo nje ya uwezo wangu, lakini hii kitu ilinijengea uhodari wa hali ya juu sana si darasani hata katika jamii inayonizunguka. Yaani ilifika mahali ile sauti ya kimamlaka ya mzee ikawa ndio ipo kwangu huku busara ikitawala kupita maelezo pale ninapo ongea na watu.

Mkasa na malimbukeni wawili wasio na maadili;

Kwa mnaoifahamu njia ya Bagamoyo rd kama unaenda Tegeta, Ukitoka tu pale darajani Makonde kuna njia ya kwanza kushoto halalafu unakamata “service road” kwa mbele upande huohuo kushoto kuna Carwash sikumbuki jina, baada ya iyo carwash kuna njia inapandisha kushoto kwenda Primrose Hall, sasa hapo kwenye T inayopandisha Primrose mbele yake kuna wamama wanauza matunda na dizaini flani kuna bodaboda ndipo Mkasa huu ulipotokea.

Ilikua hivi mimi nilitoka service road na kausafiri kangu, nikaenda kuegesha upande wa carwash ili nikanunue matunda niendelee na safari yangu kwenda kusalimia mgonjwa maeneo ya shule kule. Baada ya kuchukua matunda nikachukua kausafiri kangu, ile naingia tu service road kukawa na roli haya ya mchanga nalo likawa linakuja napo tokea mbele yangu kukawa na gari nyingine 2 sasa katika hizi gari 2 kuna gari ”funCargo” iliyokua katikati (yaani mie nyuma, Funcargo kati na nyingine mbele), Funcargo baada ya kuona lile roli na yeye yupo kati sijui alipata wenge kutoka wapi, lori lilipo karibia kwake gari ‘’funCargo” ikaanza rudi nyuma, mie nikaanza kumpigia honi kama gari moshi jamaa wapi hadi gari yake “Funcargo” ikafika kwa usafiri wangu usawa wa plate number ndio ikasimama.

Kwa haraka nikawa nimegundua kua usafiri wangu haujapata uharibifu wowote, kwahiyo nikawa nimetulia tu ndani. Jamaa wa Funcargo wao wakashuka na jazba za hatari wakaja kugonga kioo changu kuonyesha ishara kua nifungue mlango nikashuka. Ile kushuka tuu, si wakalianzisha bana kwamba kwa nini nimegonga gari yao ”Funcargo”, mie kimya. Wakaanza unadharau sana we dogo, mie kimya. Ikabidi niende mbele kuangalia damage iliyotokea, kwangu kukawa hakuna damage wao kwao ipo kumbuka wapo wa 2 na mie nipo peke yangu. Sasa watu wakawa wanaona kinachoendelea pale. Wale jamaa ukiwaangalia kimuonekano ni kama walikua wanajiamini sana na walikua tayari kwa lolote

Mie kwakua nilikua sahihi, ile sauti ya kimamlaka ikaja huku nikimtumainia Muumba nikasema kwamba nanukuu “ watu wote hapa sio wapumbavu hasa hawa wamama wafanyabiashara, wameona tukio zima mwanzo mwisho sasa kama muna la ziada ongeeni kama hamna mjue mnapoteza muda wangu, ama sivyo nitaondoka na nyie na msiamini kitakachotokea”. Baada ya hapo nikaona jamaa jazba zimepungua, mmoja akasema “lakini hapo ni kama mie nilichubua so haijadhurika’’ tuondoke. Hao wakaondoka dizaini kama paka wale wa bar wanapokosa mabaki.

Hapa ndio Dhumuni la Uzi huu lilipo.

Nikiwa bado nimepigwa na bumbu wazi katika eneo lile mama mmoja akasema nanukuu ”Kijana wasamee bure tumeona kilichotokea, tena yule aliyekua abiria alikua na bastola kiunoni na aliiseti akiwa anashuka kutoka kwenye gari (funCargo), hili eneo yaani sijui likoje na mkasa wa "Ukiwaona" nao ulikua sio mbali na eneo hili”. Nami nahitimisha kwa kuwauliza nyie waungwana, ujuaji na kutofuata miiko ya matumizi ya silaha za moto kwa baadhi ya watu ambao ni limbukeni, je ilikuaje na uliwezaje kujinasua katika saga hiyo?
Umenikumbusha Mzee UKIWAONA RAMADHAN MWINSHEHE DITOPILE MZUZURI.
 
Ni miaka kama sita sasa huenda imepita, tuko kwa Mama Kamche, Ng'ambo ya pili ya barabbara ukiwa Kanisa la Kakobe! Usiku wa saa tatu hivi au nne!

Miaka ile kwa Mama Kamche palikua panajaza sana, sasa ikatokea kutofuatiana kiswahili tu, jamaa wakaanzisha vurugu, mmoja akatoa bastola! Hahhaahahh ninachokumbuka ni kwamba aliingia kwenye gari na kuondoka na hata pombe yake hakumaliza! Alijua wote pale tumekaa vilaza na walevi. Ukiwa na silaha kamwe usiitumie kumtisha mtu
Kilitokea nini hasa
 
Mkuu tupe mkasa alipewa dozi gani hadi akashika njia? Je ni 1sec × 1 ndoo
 
Hakikisha mikonoyako ipo shap sana vinginevyo tutakuja kula ubwaubwa msibani huku wewe ukiwa kwenye jeneza
bro, kumkwapua huyo boya chuma ni easy sana tu, nataka nimfunze adabu, akaandike maelezo kwa RSO wake, maana pistol za malindon wamezigeuza za kuja kuvimbia bar. Hawa viusalama vya siku hizi kenge kweli, wanadhan kushika pistol ndo wamewin maisha
 
Duh
 
Ina maana huangaliagi muvi za kichina hu haa,, fasta unasepa na mguu wa kuku unamgeuzia yeye,,
 
Kizazi cha juzi tu mimi basi nimechukua muda kweli kuelewa hapo kwenye "Ukiwaona"
 
Back
Top Bottom