Washkaji wamejipata mimi niko vilevile

Objective football

JF-Expert Member
Oct 21, 2023
1,055
2,458
Nimerudi nyumbani huu mwisho wa mwaka kama ilivyo jadi yetu tulio wengi.

Nimewakuta Baba na mama hali si shwari, nikicheki madogo all eyes on me, na mmoja anashughulikia mikopo ya elimu ya juu mwaka huu ila mambo bado tafrani.

Juzi tulivyoenda ibadani kukatokea mchango wa ujenzi na ukarabati wa nyumba ya ibada, daah washikaji wa rika yangu wamechangia mifuko ya cement 200, mmoja katoa cheque ya milioni 10 katika maongezi yake anamiliki kampuni ya clearing and forwarding huko mjini. Mwingine kaahidi tipa 20 za mchanga.

Hakika ibada ilifaana sana, mchungaji aliwaita wazazi wa wale washikaji pale madhabahuni na kutamka kwamba hakika mumezaa chema sana na MUNGU amebariki uzao wenu.

Hali ile ilinifanya nijiulize maswali yasiyo na mwisho kuhusu hatma ya maisha yangu pamoja na wazazi wangu.

Mungu why najitafuta lakini sijipati? Dunia hii ni ya wachache? Wazazi wangu wataishi katika umasikini huu wa kutisha hadi lini?

wakati narudi nyumbani na mama yangu kwa mguu, nikawa napitwa na wana wakiwa kwenye tinted za Black athlete crown, Ford ranger, Subaru nk, wakati mimi naendelea kupita kando ya barabara kukwepa tope la mvua hizi.
 
hali ya kiuchumi inasikitisha, usiombe kabisa.

umasikitini ni utumwa
Hauna pakulala -homeless
Unakosa Milo mitatu 3 kwa siku
Hauna Afya imara umelazwa au upo ICU
Hauna mavazi unatembea uchi


Kama una hivyo vitu na unalalamika kuwa wewe ni Masikini Basi huo umasikini unaouimba utakuvaa na utapoteza Kila kitu ikiwemo furaha
 
Hauna pakulala -homeless
Unakosa Milo mitatu 3 kwa siku
Hauna Afya imara umelazwa au upo ICU
Hauna mavazi unatembea uchi


Kama una hivyo vitu na unalalamika kuwa wewe ni Masikini Basi huo umasikini unaouimba utakuvaa na utapoteza Kila kitu ikiwemo furaha
mkuu not such easy to sustain under abject poverty condition.

kula yangu ni MUNGU saidia, milo yangu ni miwili nayo kwa mbinde.
 
56 Reactions
Reply
Back
Top Bottom