Tabia muhimu za kuzijenga kwa watoto

Oct 5, 2018
33
58
Wazazi/walezi wengi hutamani kujenga tabia mbalimbali nzuri kwa watoto lakini hujikuta katika njiapanda ya kuchagua tabia ipi waiwekezee nguvu zaidi ya nyingine. Katika kuhudumia kwangu wazazi kwa kuwapa ushauri kwa miaka zaidi ya sita sasa nimekutana na wazazi wengi ambao wanajua tabia gani hawazitaki kwa watoto wao ni wachache sana wanajua ni tabia gani wanataka kuzijenga kwa watoto wao.

Zifuatazo ni tabia ambazo kutokana na uzoefu wangu naona ni za muhimu sana wazazi kuzijenga kwa watoto wao. Nitazitaja tabia na kueleza kwa ufupi sana jinsi gani unaweza kuzijenga kwa mtoto/watoto wako.

  1. Tabia ya usafi na unadhifu. Usafi na unadhifu ni tabia ambayo mtoto hujengewa tokea akiwa mdogo kabisa. Tokea akiwa bado anapewa huduma za kusafishwa kama vile kuogeshwa. Tabia hii ni muhimu sana kwani ni tabia ambayo humpa mtu muonekano wa jinsi watu watampokea na kumuhukumu duniani. Mtoto akiwa msafi na nadhifu atakuwa na funguo ya kwanza ya kukubalika na watu kwenye jamii yake. Kwenye kitabu changu cha "Mfundishe Mtoto Wako Kuishi” nimeeleza ya kwamba “..mtu ni jinsi anavyofikiri, anavyoonekana na anavyotenda” hivyo hata kitu kimoja kikikosekana kati ya hivyo uthamani wa mtu hupotea. Ni muhimu mzazi au mlezi uhakikishe unamjengea mtoto tabia hii ya usafi kwa kumfundisha, kumshirikisha na kumsimamia katika kufanya usafi wa mwili wake na makazi.
  2. Kujiamini. Mtu asiyejiamini hawezi kufanya jambo lolote lile maishani mwake. Kujiamini ni tabia ambayo hujengwa kwa watoto. Mtoto huandaliwa kujiamini kwa kupitishwa kufanya mambo mbalimbali, kupendwa na kuheshimiwa, kusemewa vizuri na wazazi au kujengewa tabia ya kupenda kujifunza vitu mbalimbali. Tabia hii ni lazima wazazi muijenge kwa watoto ingali wakiwa wadogo na wakue nayo na kuizoea kama majina yao.
  3. Ukweli na uwazi. Dunia tuliyopo sasa inachangamoto ya kukosa watu wakweli na wawazi. Watu kusema uongo na kutokuwa wawazi limekuwa ni jambo la kawaida kabisa. Ni vyema wazazi mkacheza nafasi yenu hapa kwa kuwaandaa watoto mapema kabisa ili waje kuwa ni watu watakaosema na kusimamia ukweli. Watoto wahimizwe kusema ukweli, wapewe uhuru wa kuona kuwa ukisema ukweli hauwezi kupata madhara, waoneshwe furaha iliyopo kwenye ukweli. Mtoto atakayejengewa tabia hii atakuwa amepewa nyenzo kubwa sana ya kuenda nayo popote kwenye maisha yake.
  4. Kujali. Kujali nafsi yake, kujali watu wa karibu naye, kujali watu wa mbali au kujali mazingira. Tabia ya kujali ni muhimu sana kuijenga kwenye maisha ya mtoto. Haijalishi mtoto wako atakuwa ni mwenye mafanikio kiasi gani, kama hatojengewa uwezo wa kujali, hakuna mtu atajali nini anaweza kufanya au nini anacho. Jenga tabia hii kwa mtoto ili kumuhakikishia maisha yenye tija sasa na hapo baada.
  5. Heshima. Siku zote nasema heshima ndiyo ufunguo wa watu kuishi pamoja kwenye jamii. Mjengee mtoto wako tabia ya kujiheshimu na kuwaheshimu wengine kwa utu wao. Tabia hii itamuandalia njia mtoto kuheshimika pia kwenye jamii yake.
  6. Usikivu. Kwenye jamii kwa sasa kila mtu anataka kusikilizwa, ni wachache sana wanaosikiliza wenzao. Wengi wameziba masikio na kusikiliza sauti zao tu. Mtoto atakayejengewa tabia ya usikivu atakuwa ni mtu atakayejifunza kwa kusikia kwa watu wengine. Ni rahisi sana kujifunza kwa kusikiliza watu. Mjengee mtoto tabia hii.
  7. Uaminifu. Mjengee mtoto tabia ya kuwa muaminifu katika kila jambo analolifanya. Kuwa mfano wa uaminifu kwa mtoto mapema. Himiza uaminifu kwa mtoto kila mara. Tabia hii ni ya thamani sana kwenye dunia ya sasa.
  8. Kujituma kwenye kazi. Tabia hii hujengwa kwa watoto kwa kuwafanya washiriki katika kufanya kazi mbalimbali kwa mikono yao wenyewe. Jenga tabia hii kwa kuweka ratiba ya nyumbani, kuweka sheria za nyumbani na kutoa usimamizi thabiti wa kumsukuma mtoto kufanya kazi kwa kujituma mapema. Mara nyingi kazi haipendezi kufanya, ni lazima watoto wasukumwe mapema ili kujenga tabia hii.
  9. Kujifunza kila siku. Tabia hii ya kupenda kujefunza kwa watoto hujengwa na wazazi. Mtoto aanze kusomewa vitabu mapema, apewe maswali mengi ya kijamii, binafsi, mtoto apewe kazi ya kutafiti juu ya mambo mbalimbali, mtoto apewe nafasi ya kuelezea mambo anayoyajua n.k mtoto mwenye tabia ya kujifunza kwenye dunia ya sasa ni mtoto mwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa.
  10. Uwajibikaji. Ni muhimu mtoto ajengewe tabia ya kuona kila kitu kinachomuhusu yeye anapaswa kukifanya mwenyewe. Mtoto lazima ajengewe tabia ya kutolaumu watu wengine juu ya mambo yanayomuhusu. Tabia hii itamjengea mtoto tabia ya kutafuta suluhu ya matatizo yake mwenyewe badala ya kuwanyoshea wengine vidole.
Hizi ni baadhi ya tabia muhimu za kuzijenga kwa watoto. Tujifunze zaidi juu ya jinsi ya kuzijenga. Nimezidokeza ili kuwapa changamoto ya kutafuta ni tabia gani mngependa kuziona kwa watoto wenu badala ya kukazania kuziona tabia ambazo hamzitaki.
 
IMARA SANA HII MKUU
 
Hizo nguzo kuna baadhi ya watu wazima wanatakiwa wajifunze .. uzi bomba MKUU
 
Back
Top Bottom