Tabia mbaya kumi zinazofanya ushindwe kuwa na akiba "savings"

Uzi umetulia.well said.Basi tujifunze au kujikumbusha namna bora za kuweka akiba kutokana na kipato chetu kidogo
 
Hapo kwenye namba9 nimepaondolea uvivu mwaka huu baada ya kumsomesha mdogo wangu wa mwisho nikasema sasa yatoshaaa!!
Asante kwa mkuu Bams kwa kibwagizo chako kama nyongeza no11. Kwangu ni kama signal note ya upambanaji wangu kwani initially niliumia kwa style hiyo ila i am now correcting myself na hakika mafanikio nayaona!
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kuwa umepatia zote kasoro no 9 sio sawa kabisa..hio ndio real investment ya mwanadam..
Life is about giving not accumulating..
If you want to die rich, give.
If you want to die poor, accumulate.
 
Kuna hili la michango ya harusi, send off, komunio, na bila kusahau kigodoro haya yanatufilisi sana mjini jamani mtu akitaka kuoa au kuolewa awashirikishe ndugu wa karibu yatosha mnatufilisi!
 
Kuna hili la michango ya harusi, send off, komunio, na bila kusahau kigodoro haya yanatufilisi sana mjini jamani mtu akitaka kuoa au kuolewa awashirikishe ndugu wa karibu yatosha mnatufilisi!

point noted mkuu, umenikumbusha nina kadi sita za michango na sijui nianze na ipi na nimalizie na ipi.
 
Namba 4,8 na 9 nimekula za uso, kuna umuhimu wa kumPM mleza uzi yawezekana ana suluhisho mujarabu.
 
Unaweza kuwa umepatia zote kasoro no 9 sio sawa kabisa..hio ndio real investment ya mwanadam..
Life is about giving not accumulating..
If you want to die rich, give.
If you want to die poor, accumulate.

Mkuu mleta mada hakusema tusisaidie bali ameshauri tusaidie kulingana na kipato chetu na kupima umuhimu wa shida ya msaidiwa, utakuta wewe una watoto wawili au watatu lkn alafu ndugu yako yupo kijijini huko ana watoto mpaka anapotea hesabu mbaya zaidi wanae wameshaanza kuzaa naye anaendelea kuzaa, sasa kila wiki ni simu tu mtoto anaumwa mjukuu hana uniform sasa hapo hao wanao utawasomesha vipi?
 
Kwa kweli nimetulia na dozi zimeingia kuanzia ya kwanza mpaka ya kumi …..na kwa dozi hizi lazima nipone
 
Well said mtoa post!. hilo namba 10 nimeshalifanyia kazi alfajiri hii.
Namba 4 ni ishu serious sana sababu sio tu inapoteza pesa lakini muhimu zaidi muda unapotea.
 
Sio lazima ujumbe huu uwe sahihi kwa 100%, lakini nadhani kuna mambo kadhaa ya kujifunza humu.

TABIA MBAYA KUMI ZINAZOFANYA USHINDWE KUWA NA AKIBA "SAVINGS"....HATIMAE UNAKOSA MTAJI WA KUFANYA MAMBO YAKO.

1. Unanunua nguo bila mpangilio.
Kuna watu wana nguo kama duka. Plz Kuwa na nguo chache Tu huwezi kushindana na fashion.

2. Unanunua Viatu bila mpango.
Viatu pia vinameza savings zetu. Nunua pea chache zenye ubora ili zidumu.

3. Unatoa ofa bar bila mpango.
Nenda bar kwa bajeti mahususi. Hakuna atakae kusifia kwa kutoa ofa hovyo. Kila mbuzi ale kwa urefu Wa kamba yake. Jifunze ubepari.

4. Unatumia hela nyingi kwenye simu ambazo sio productive. Unaweka vifurushi vya week vya sh 7000 au 1000 ili uchati na marafiki Fb au wasaap Huo ni ujinga. Badilika.

5. Unakopa hela banki na kununua vitu kama simu ya milioni na gari ambazo sio productive. Unakosa hela hata ya mafuta, gari la nini kwanini usingewekeza sehemu ili kuwe na mradi Wa kuzalisha ndio ununue gari?

6. Una marafiki wengi ambao ni mizigo kwako au hamuendani kivipato hivyo unajikuta unalazimika kutumia zaidi ya kipato chako ili uwa-impress. Meneja Wa TRA na mwalimu Wa sec unatarajia utoe offer mpaka umfurahishe meneja? Utabaki na sh ngapi toka kwenye salary yako?? Zinduka.

7. Huna timetable ya kudumu ya maisha yako, unajikuta unaburuzwa Tu na maradiki zako kwa kwenda sehemu mbalimbali za matumizi.Kuwa na ratiba za maisha yako na zisimamie kikamilifu, usiburuzwe!

8. Una michepuko inayokutegemea we we kwa kila kitu. Wanakuita ATM we we unakenua Tu huzinduki. Badilika.

9. Una huruma sana kuliko kipato chako. Yaani kila ukiombwa unatoa hata kama muombaji hana genuine need. Usiwe mkristo kuliko Yesu. Fanya hivyo kama ni lazima. Ila sio kila anaekupiga mzinga unapigika.

10. Unatembea na hela nyingi kwenye wallet au mshahara wote kwenye wallet au nyumbani kwako. Unapokuwa na petty cash nyingi unatengeneza mazingira ya kutumia hovyo. Jifunze kuweka hela benki. Tembea na hela Tu unayoihitaji kwa matumizi ya lazima.

Naamini tukizingatia kanuni hizi kumi tutaongeza savings zetu na kuwa na mtaji Wa kufanya vitu vikubwa endelevu.
Anza sasa...badilika.

Namba 9 na namba 10 zinapita bila kupingwa
 
Back
Top Bottom