Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimeelimika na naomba nimpongeze mleta mada
Japo siyo siasa LAKINI tunashukuru, haya ni mawazo ya kujenga. Jambo jingine ambalo ni muhimu kuongezea:
11. Usikimbilie kuanzisha miradi ambayo huna uhakika nayo, mara nyingi miradi ya kuiga. Fanya utafiti wa kutosha, na unaporidhika na kuamua kuanzisha mradi, wekeza pesa kiasi kidogo, ile tu ya kuuwezesha mradi usimame, na kisha pima maendeleo ya mradi wenyewe kabla hujaingiza pesa yote uliyo nayo.
12. Weka vigezo vya kukusaidia kutambua kama mradi ni viable or not. Ukiridhika kuwa mradi hauna faida, chukua maumuzi magumu ya kuufunga kabla haujakuingizia hasara kubwa lakini pia usiwe mwepesi wa kufunga mradi kama una jibu la kwa nini mradi haukutoa faida, na hicho kilichosababisha una uwezo wa kukitatua.
Dah, hayo yote me siyafanyi but at the end of the day sina kitu. Hata sijui ni kwanini ingawa I'm a middle income earner!